Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi.
Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako.
Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu.
Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako.
Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo.
Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu?
Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:-
NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO:
Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ akamaanisha kuwa situ naipenda gofu, bali pia mimi mwenyewe ni gofu.
Watu waliofanikiwa huwa wanapenda kwa dhati mambo wanayoyafanya, ni ngumu sana kufanikiwa katika jambo unalolichukia.
Swali la msingi ambalo ningependa ujiulize leo ni ‘’Nitajuaje kuwa hili ninalolifanya ni kusudi langu?’’ Hili ni swali muhimu ambalo wengi huwa hawataki kujiuliza kwani ni ni kati ya maswali magumu ambayo si rahisi kupata majibu yake.
Leo ningependa nianze na njia kuu mbili za kukusaidia:
1. Jambo linalo gusa moyo wako kupita yote.
Nakumbuka kisa cha Dr Cycle (MD), kijana ambaye alifanikiwa sana katika fani yake ya udaktari. Alipokuwa mtoto hakupenda kuwa daktari alipenda kuwa mwanamuziki lakini kwa sababu baba yake alitamani sana kuwa daktari na akashindwa, akataka ndoto hiyo aitimize mtoto wake.
Ni kweli Dr Cycle alikuja kuwa daktari maarufu sana aliyesifika, na siku moja taasisi ya daktari ikaandaa tuzo na kumtunuku kwa mafanikio yake.
Alipoitwa jina lake jukwaani kila mtu alisimama kwa shangwe na heshima kwake na alipigiwa makofi.
Mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake alitakiwa kuzungumza maneno machache lakini alipoanza tu sentensi ya kwanza, alianza kutoa machozi na akashindwa kuendelea.Watu walijua kuwa amejawa na furaha na akashindwa kuongea, akakaa kimya tangu wakati huo hadi walipoingia kwenye gari.
Baba yake alipomuuliza kwanini alishindwa kuongea ndipo akaanza kusema:
’’Baba, mimi kuwa daktari haikuwa ndoto yangu, bali ilikuwa ndoto yako. Ingawa kila mtu ananisifia lakini sisikii kuridhika ndani ya moyo wangu, nasikia kuusaliti moyo wangu. Miaka hii yote nimeishi maisha yako sijawai kuishi maisha yangu, naomba uniache baba nianze kuishi maisha yangu,mimi nataka kuwa mwanamziki na sio daktari, na hilo ndilo jambo litakalonipa furaha ya kudumu maishani’’
Ni vyema kutambua kuwa kusudi lako huanzia ndani yako na sio nje yako.
Kwa vyovyote vile jambo uliloambiwa kulifanya ni jambo ambalo litausumbua moyo wako kupita kawaida, haliwezi kupita mbele yako bila kuligundua kwamba limepita. Unaweza kuwa kwa sasa unafanya jambo fulani na kila mtu anakuona umefanikiwa, lakini ndani ya moyo wako unajua kabisa kuna jambo ambalo siku ukifanikiwa kulifanya ndio utafurahi zaidi. Huwezi kupata amani ya moyo ya kudumu kama unachofanya sicho ambacho umeletwa duniani kukifanya, unaweza kufumba macho na kuziba masikio kwa muda usiusikilize moyo wako lakini kila wakati sauti itakurudia ndani yako,’’Unatakiwa kufanya lile na sio hili, hapa ulipo si mahali sahihi’’
Hebu jiulize swali hili – kama ungeambiwa utalipwa mshahara wa kiwango chochote unachotaka na ukapewa fursa ya kuchagua utakuwa unafanya shughuli gani, utachagua kufanya jambo gani? Bado utaendelea kufanya unachofanya sasa? Jibu la swali hili ndilo kusudi linaloridhisha moyo wako, ndio kitu unachotamani na kukifurahia kukifanya. Je,uko tayari kuishi kwa kuusaliti moyo wako hadi lini? Utaendelea kuishi maisha ya wengine hadi lini? Je,unataka kuwa kama Dr Clyde baada ya miaka kadhaa kuanzia leo? Kaa chini leo na ujiulize swali hilo hapo juu mara nyingi uwezavyo na ujipatie majibu yake.
John Mason mwandishi maarufu katika kitabu chake aliandika;’’You were born original, don’t die a copy’’,akimaanisha ulizaliwa ukiwa halisi, hivyo usife ukiwa bandia. Amua kuchukua hatua kuishi maisha yako ’’original’’ kuanzia leo.
2. Chunguza uwezo wako
Nilipokuwa mdogo, mama yangu alipata tenda ya kuwafundisha Kiswahili Wazungu wamisionari nyumbani kwao, na alikuwa akinichukua nifuatane naye.Kila wakati tulipofika kulikuwa na watoto wawili wadogo ambao walikuwa wanamwagiwa vifaa mbalimbali kama vile nyumba, ndege, magari, vitanda vya hospitali, n.k.
Siku moja mama yangu alipouliza kusudi la ule mchezo wale wamisionari wakasema ;’’Kwa kuangalia uwezo wa kila mtoto anaweza kuunganisha vitu gani,huwa tunaweza kujua tuanze kumuelekeza katika masomo gani yatakayoendana na kipaji chake. Na ukweli ni kuwa hata ukiwapa vifaa vingi kila wakati kila mmoja ataunganisha aina fulani ya vifaa’’.
Kila kitu kilichoumbwa kimeumbwa ili kukamilisha kusudi lililofanya kiumbwe.
Ndege ameumbwa kama kiumbe cha kuruka juu, ukiangalia umbo lake na wepesi wa mifupa yake ni ushahidi tosha wa kusudi lake. Ukiangalia kisu kimetengenezwa kukata ndio maana hakina umbo la kikombe.
Nawe pia kabla hujaumbwa tayari ulikusudiwa kufanya kitu fulani maishani.
Ni vyema ukajiangalia ni uwezo gani ambao umewekewa unaoweza kuwa ni mwelekeo ‘’pointer’’ kwenye kusudi lako. Kazi kubwa ya uwezo unaopewa ni kurahisisha kutekeleza lile kusudi ulilonalo.
Mara nyingi mambo unayoyapenda utakuta umewekewa uwezo ndani yako wa kuyatekeleza kwa ufanisi zaidi.
Ni hatari sana kujaribu kuishi maisha yako yote katika mambo ambayo hujapewa uwezo wa kipekee kuyafanya, unaweza kufaikiwa lakini hutakuwa na furaha ya kudumu.
Jaribu kuorodhesha ni uwezo gani na vipawa gani ambavyo unaona ni vya kipekee maishani mwako? Je,vipawa hivyo vinakuelekeza katika kufanya mambo gani?
Kila uwezo unaopewa upo hapo ili kurahisishia kutimiza makusudi fulani ya maisha yako. Jikague na ujiulize: ’’Hivi nina uwezo gani wa kipekee?’’Chukua kipande cha karatasi na andika. Ni vyema ufanye maamuzi kuanzia leo kuishi katika kile ulicholetwa duniani kufanya.
Mwandishi baada ya kuelezea mbinu hizo mbili, amezidi kuongezea zingine ili kuweza kukupa uelewa zaidi. Endelea kumfuatilia kama nilivyonukuu hapa chini:
3. Mbinu ya tatu
Kuna maswali mawili muhimu sana katika maisha ambayo lazima kila mtu awe na majibu nayo, ukikosa majibu yake ni kizuizi tosha katika kuelekea mafaniko yako. Maswali haya mawili yamekuwa ndio mwongozo kwa kila aliyefanikiwa maishani katika kile anachofanya. Baadhi ya watu hawajui kabisa lakini hawako tayari kutumia muda wao kuyatafutia majibu yake na kuyafanyia kazi.
SWALI LA KWANZA: Nilizaliwa kwa kusudi gani?
Kusudi la kitu ndio sababu iliyofanya kitu hicho kiundwe kwa namna kilivyoundwa.
Ukiangalia muundo wa kijiko ulivyo unakuelekeza namna ya kutumia na ukitaka kukitumia kama kisu hutafanikiwa kabisa.
Ukimuangalia ndege alivyoumbwa amepewa umbo na uwezo wa kuruka angani na ukijaribu kumweka baharini mbwembwe zote zitaisha na atakufa mara moja.
Kila mtu ameumbwa kwa kusudi maalum la kuja kufanya hapa duniani na amepewa uwezo wa kipekee ndani yake ili kulitimiza kusudi hilo kwa mafanikio.
Ukijaribu kufanya jambo nje ya kusudi uliloletwa kulifanya duniani utafeli kila wakati.
Ni kama ukijaribu kumshindanisha tai kuogelea pamoja na samaki papa, pamoja na sifa na uwezo wote alio nao tai maishani mwake, atafeli kila wakati.
Tatizo sio kwamba huna uwezo ila ni kwa sababu umemshindanisha katika eneo ambalo hajazaliwa kwa kusudi hilo na hivyo hana uwezo na umbo la kumfanya awe mshindi wa kuogelea.
Watu wengi wamefeli maishani si kwa sababu hawana uwezo wa kuwafanya wafanikiwe bali ni kwa sababu wako sehemu ambazo sio kusudi la kuumbwa kwao.
Ukimchukua golikipa ukamweka kuwa beki wa timu yenu, usishangae kila wakati mkapigwa penati kwenye lango lenu kwani badala ya kutumia miguu, utashangaa atavyojisahau na kutumia mikono kuzuia mpira.
Leo, tumia muda kujiuliza; Je, nimeumbwa kwa kusudi gani? Ninachofanya kinaendana na kusudi langu?
SWALI LA PILI: Nakwenda wapi?
Kila mtu anaamka asubuhi na anaelekea kazini, shuleni, kwenye biashara n.k. Ingawa kila mtu anaonekana yuko bize lakini si kila mtu anajua anaelekea wapi katika maisha yake. Kuna watu wengi baada ya umri kwenda sana ndipo huja kugundua kuwa walipoteza muda wao kwa mambo ambayo hayakuwapeleka walikokuwa wanataka. Je, unachofanya leo kinachangia kukupa mwelekeo wa unakokwenda?
Swali ni kuwa; Je, umeshawai kufikiri kupitia unachofanya leo kesho utafika?
Kama hujui unakokwenda kila mahali ulipo patakuwa sahihi.
Kama unaona unachofanya leo hakitakupeleka kule unakotaka kwenda,tafuta namna ya kubadilisha.
Hakuna maana yoyote ya kuishi maisha usiyoyapenda kisha kuja baadae uzeeni kugundua umepoteza muda wako.
Usihangaike kuwa bize tu, unaamka unaenda ofisini, kwenye biashara, shuleni, kisha unarudi nyumbani - Je, unajua unakokwenda? Baada ya Miaka 10 au 20 unataka uwe umefika wapi?
Anza leo kutafuta majibu ya maswali haya,kwani hakuna mafanikio bila kujua kusudi la maisha yako na kule unakokwenda.
4. Mbinu ya nne
MAMBO MAWILI YA KUFANYA ILI KUBADILISHA HALI YAKO KABISA
Taasisi ya afya ya nchi Scotland ilifanya utafiti kwa miaka kumi [10] na kugundua kuwa watu wanaokufa kwa sababu ya magonjwa ya moyo siku ya Jumatatu asubuhi ni wengi kwa asilimia ishirini [20%] ukilinganisha na siku nyingine za wiki.
Pamoja na kuwa na sababu nyingi sana kwa jambo hili, ila sababu mojawapo ni kuwa Jumatatu asubuhi ni siku mbaya ya wiki kwa watu wengi sana duniani.
Watu wengi huamka na kujikuta wanalazimika kwenda kufanya kazi ambazo hawazipendi, sio ndoto zao na kama wangepewa fursa ya kufanya kitu kingine basi wangeacha kazi hizo.
Wengi wanagundua wanalazimika kurudi katika ofisi zilezile wanazozichukia, watakutana na watu walewale ambao wasingependa kuwaona na wataendelea kulipwa mshahara kiasi kilekile ambacho wanaona ni chini ya kiwango chao cha huku wakikumbuka madeni wanayotakiwa kulipa na majukumu ya kifedha yanayowakabili.
Katika hali kama hizi wengi huanza siku ya Jumatatu asubuhi kwa majonzi na kukosa furaha na mawazo huwa mengi hadi wanapata msongo na kupelekea matatizo ya moyo.
Jambo la kutambua ni kuwa hali yako haitabadilika hadi ufanye mambo haya mawili:
a. Amua kuamini kwamba inawezekana kubadilisha hali yako ya sasa.
Watu wengi ukiwauliza kwanini wanaendelea na hali ambazo hawazipendi watakuambia ni kwasababu hawana fursa nyingine yoyote ama hawana pesa. Lakini nilichokuja kugundua ni kuwa wengi bado hawajakata shauri kwa dhati ndani ya mioyo yao kuwa wanataka mabadiliko kweli; wengi ukiongea nao ni kama vile wamekubaliana na hali hiyo na wameamini kuwa hawana cha kufanya. Ukiamini hivyo basi hali yako haitabadilika.
Law of attraction [kanuni ya kuvuta vitu] inasema unavutia kwako watu, rasilimali na fursa zile ambazo unaziamini na unaziwaza ndani yako kila wakati.
Kuanzia leo usiamini katika kutowezekana, panga mikakati yako, amua kubadilisha usichokipenda na anza kuchukua hatua.
b. Chukua hatua ya mabadiliko bila kujali utafeli mara ngapi
Unatafuta kazi, usitume maombi mara mbili tu usipopata unakata tamaa.
Unatafuta mkopo, usiende benki moja tu au kwa mtu mmoja tu eti akikataa basi unasema haiwezekani.
Umefeli mara moja unasema sitafaulu tena wakati Jack Ma, bilionea nambari moja nchini China alifeli chuo mara tatu na leo ni tajiri mkubwa. Jaribu mara nyingi uwezavyo ili kujitengenezea uwezekano mkubwa zaidi.
Watu wanaofanikiwa ni wale ambao kila wakiambiwa haiwezekani wanatafuta njia nyingine ya kufanya iwezekane.
Umeshawai kumuona mwanaume anampenda mwanamke kwa dhati? Hata akiambiwa ‘’NO’’ mara kumi atatafuta mbinu nyingine ya kufanya iwezekane. Mara ataleta maua,mara atatuma meseji kutwa mara saba…. Ili mradi tu apate namna ya kukubaliwa.
Upendo wa kweli wa kweli hauruhusu kukataliwa mara moja ukoshe mke.
Kwenye kufanikisha ndoto zako ni vivyo hivyo; usikubali kukataliwa kwako mara moja kukukoseshe kutimiza ndoto yako uipendavyo.
Inawezekana, leo jaribu tena kile kilichoshindikana huko nyuma.
5. Mbinu ya Tano
JAMBO MOJA MAHSUSI KWA KUONGEZA UWEZO WAKO ILI UFIKIE KILELE CHA MAFANIKIO
Larry Bird alijulikana kuwa mchezaji wa kawaida sana katika mpira wa kikapu hadi pale alipoamua kuwa yeye si mtu mwenye kipaji cha kipekee sana katika mpira wa kikapu, aliamua kufanya kitu cha ziada ili kuhakikisha ndoto yake inatimia.
Aliamua kuwa kila siku asubuhi kabla hujaenda shule awe anarusha mipira mara mia tano [500] akijaribu kufunga katika mazoezi yake binafsi .
Baada ya muda, Larry alijulikana kama ni mchezaji hodari wamitupo ya mipira [consistent free-throw shooter] na aliisaidia timu yake ya Boston Celtics kushinda taji la dunia mara tatu.
Hivi ndivyo nidhamu na juhudi inavyoweza kumfanya mtu afanikiwe. Wengi wetu tunafikiri kuwa uwezo na mafanikio ya kipekee huja kwasababu tuna kipaji fulani, na hii imesababisha wengi kufikiri kuwa hawawezi kufanikiwa kwasababu hawana kipaji kabisa.
Kuna wengi wana vipaji ila hawana nidhamu na wameshindwa kufanikiwa, kuna wengi wenye vipaji vyao ni vidogo ila nidhamu yao imewasaidia kufika mbali. Kuna wengi wenye sauti nzuri ila wamepitwa kwa mafanikio na wenye sauti zisizo nzuri kama wao ila wana juhudi kubwa kuliko wao.
Mimi si mchambuzi hodari wa masuala ya mchezo wa mpira wa mpira wa miuguu, ila katika majadiliano fulani ya uchambuzi wa uwezo wa wachezaji nilisikia wakisema kuwa Messi anang’ara kutokana ya kipaji chake na Ronaldo anang’ara kutokana ya juhudi zake.
Jambo la msingi hapa ni kuwa mara unapogundua unapungukiwa uwezo fulani, fanya juhudi mara mbili kuliko mtu wa kawaida.
Mambo matatu ya kuzingatia katika kujenga uwezo wako:
a. Tambua uwezo wa muhimu unaohitaji
Hebu jiulize,ni uwezo gani ambao ukiuongeza leo utafanya thamani yako iwe maradufu katika biashara yako, kazini kwako, shuleni n.k?
Ukishatambua uwezo huo, anza kuufanyia kazi kila siku,utashangaa baada ya muda umekuwa ’’master’’ [mtaalamu] katika jambo hilo na mafanikio yako yanaanza kuonekana.
b. Usiache hadi umeona matokeo
Kumbuka kuwa uwezo tunaotafuta huwezi kujengeka kwa siku moja, ni mchakato wa muda mrefu,usiache kuongeza uwezo wako hadi utakapoona matokeo ya kile unachokifanya.
c. Usihangaike kutafuta kukubalika,toa matokeo
Usiwe mtu wa kuhangaika kutaka kuonyesha na kuonekana kwa kile unachoweza kukifanya. Kubali kutoonekana kwa muda kidogo ili ujenge uwezo wako utazungumza kwa niaba yako.
Watu wengi wamekufa wakiwa bado hawajafikia kiwango chajuu cha mafanikio yao kwasababu hawakuwa tayari kufanya alichofanya Larry. Kila unapoanza siku yako usikubali kuyumbishwa na jambo lolote,weka mkazo katika kujenga uwezo wako bila kukata tamaa.
Hayo ni machache tu niliyonukuu. Kitabu kina kurasa 248 nami nimefanya nukuu ya kurasa 11 tu ili yumkini upate radha ya mwandishi na uweze agiza nakala yako.
Bei @ Tshs. 15,000 nami ni msambazaji wa hicho kitabu.
Kama uko Dar utaletewa ulipo bila gharama ya nauli.
Kama uko mikoani, naomba tuwasiliane namna rahisi ya kupata ila utachangia nauli ya bus.
ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2017 INAISHIA NA 2018 INAINGIA. HIZO NI NAMBA TU NA HAZINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.

Maoni

  1. nahitaj nakala ya kitabu hicho, je kwa njia ya Email inawezekana?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836

      Futa
  2. Naiataji kitabu nipo Zanzibar namba zenu nimetafuta cjapata naitaji mnitafute 0673311741 then mniambie wapi ntakipata

    JibuFuta
    Majibu
    1. Seth Simon Mwakitalu
      Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
      Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
      :www.bereadytolearn.org
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      We empower people:-
      1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
      2. Acquire life changing business skills.
      3. Prepare for retirement.

      Futa
  3. Nimependa sana na nahitajinkujua jinsi ya kukipata kitabu

    JibuFuta
    Majibu
    1. Tuwasiliane:-

      Seth Simon Mwakitalu
      Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
      Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
      :www.bereadytolearn.org
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      We empower people:-
      1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
      2. Acquire life changing business skills.
      3. Prepare for retirement.

      Futa
  4. Nimependa sana na nahitaji kukipata kitabu

    JibuFuta
    Majibu
    1. Seth Simon Mwakitalu
      Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
      Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
      :www.bereadytolearn.org
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      We empower people:-
      1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
      2. Acquire life changing business skills.
      3. Prepare for retirement.

      Futa
  5. How can I get a copy of this amazing book through email.

    mandarejames97@gmail.com

    JibuFuta
    Majibu
    1. Seth Simon Mwakitalu
      Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
      Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
      :www.bereadytolearn.org
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      We empower people:-
      1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
      2. Acquire life changing business skills.
      3. Prepare for retirement.

      Futa
  6. Asanteni, Nisaidie kitabu

    JibuFuta
    Majibu
    1. Seth Simon Mwakitalu
      Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
      Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
      :www.bereadytolearn.org
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      We empower people:-
      1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
      2. Acquire life changing business skills.
      3. Prepare for retirement.

      Futa
  7. Mpo wap? Nahitaji Kitabu Nipo Dar 0758063747

    JibuFuta
    Majibu
    1. Seth Simon Mwakitalu
      Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
      Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
      :www.bereadytolearn.org
      Tel:- +255 754 441325; +255 714 051174; +255 788 493836
      We empower people:-
      1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
      2. Acquire life changing business skills.
      3. Prepare for retirement.

      Futa
  8. Kitabu bado kipo nakihitaji

    JibuFuta
  9. Asante sana Kwa ujumbe mzuri

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...