Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka.
Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja?
Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo?
Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta.
#1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua.
Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini?
Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali.
Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Akili zisizoonekana na pia utashindwa kujua haki zako.
Makala ya Leo ya kwa ajili ya maandalizi kama hayo.
Watu wanaojitambua vizuri hawana tabia ya kulalamika. Hutawakuta wakidhalilisha wengine wala wakifanya mambo ambayo siyo. Ni watu wanaojipenda na wanawapenda wenzao.
Watu wanaojitambua vizuri wanazijua hisia zao, hisia za wale watu waliowazunguka kwenye mazingira yao Ama nyumbani au makazini mwao.
Je, ungependa kuwajua watu wanaojitambua vizuri?
Zipo njia nyingi kidogo. Ila kwa leo tutaangalia chache. Mojawapo nimeshaisema ambayo ni kutoa au kuomba mrejesho. Kuna mrejesho nyuma na mrejesho mbele. Mirejesho yote ni muhimu. Kwa lugha ya wenzetu ni feedback na Feedfoward.
Mwana Karakana ya Ubongo aliyeulizia kuhusu ukurasa maalumu alitoa mrejesho mbele (feedfoward) maana alitaka kuona yaliyoko mbele. Kwa namna moja au nyingine ametumia akili hisia zake kuleta mageuzi.
Je, umeshawahi kujicheka?
Sehemu ya akili hisia ni kujitania na kujicheka (make fun of yourself and get a laugh at it). Unajichukulia vipi pale unapojicheka?
Hapo kuna siri nzito jinsi ya kujiongezea akili hisia kwa kujitambua. Tutaona hivi punde.
Huwezi kujiona jinsi ulivyo peke yako. Huwezi kujitambua kila kitu. Kwa hiyo siri nzito ili uweze kujitambua vizuri ni kuomba kupewa mirejesho kwa watu kadhaa katika mazingira yaliyokuzunguka. Ukifanyia kazi mirejesho unayopewa na watu wengine wenye nia njema na wewe kwa ufanisi mkubwa, utaona akili hisia zako zinaongezeka vizuri.
Mfano ukiomba mrejesho kwa watu kumi (10) tofauti utajikuta kwamba watu 6 au 7 watakuwa wanajirudia rudia kitu fulani cha kuacha, kufanya au uanze kukifanya. Hapo kuna siri nzito, maana haiwezekani watu wote 6 au 7 waone kitu kwa namna moja (patterns) bila sababu maalumu.
Katika mazingira ya kawaida tunajua baadhi ya watu ambao wanajijua ni wajinga wa aina fulani lakini bado wanaendekeza huo ujinga wao hata baada ya kuambiwa.
Hapo ni sawa kabisa na kuitupa akili hisia yako kwenye shimo la taka.
Hapa Karakana ya Ubongo na Be Ready To Learn inabidi sasa tuache kutupa akili hisia zetu kwenye shimo la taka.
Tujiongeze.
Tumia nafasi hii kwa kujitambua na kujinufaisha kuongeza akili hisia yako. (Increase your emotional intelligence).
#2. Hatua ya Pili ni Kanuni za kibinafsi au kwa lugha nyingine ni self-Regulation.
Kuna wakati watu wanatuambia tuna hisia nzito (strong emotions). Tunaweza kudhania kwamba tunapokuwa na hisia nzito inamaanisha tunazo akili hisia kibao. Lahaula. Sivyo.
Utaishia kuwa mlalamishi kama wajinga wapumbavu wasiojua chochote na wala hawajui kama hawajui chochote. Mtu ambaye yuko kihisia zaidi (high emotions) hana akili hisia kubwa. Ni mjinga mpumbavu kama nilivyosema na pia ni mlalamishi.
Siri nyingine nzito ni pale mtu anapoweza kuzitawala hisia zake kwa ufanisi wa hali ya juu. Watu wenye hekima na busara - Hawa ni watu ambao wanaliangalia jambo lolote kwa umakini mkubwa kabla ya kukurupuka. Akili hisia zao zinafanya kazi vizuri.
Tuna jazba za kibayolojia (impulses) ambazo zinatupelekesha kihisia. Hatuwezi kuziondoa au kuziacha hisia za namna hii bali tunaweza kuzituliza na kuzitawala.
Kwa kutumia kanuni zetu binafsi tulizo nazo kupitia mchakato wa ndani na kujishauri wenyewe haswa tunapotulia na kufikiria vizuri ni sehemu ya mchakato unaotuwezesha kujitoa kwenye magereza yaliyopo ndani ya vichwa vyetu.
Unajua kuna watu kama yule mjinga mtakatifu mmoja aitwaye Nelson Mandela? Mwili wake uliwekwa gerezani lakini kwa sababu alikuwa tayari amejiongezea akili hisia kwa wingi, kichwa chake hakikuwahi kuishi gerezani hata siku moja.
Mwili pekee ndo ulikuwa Gerezani. Kichwa chake kilikuwa huru siku zote. Ndo maana wabaya wake hakuwalipia kisasi. Aliwasamehe Makaburu. Akili hisia siyo mchezo, ni kila kitu.
Watu wote wana akili hisia, shida ni namna ya kuziongeza na siri kali ni kuweza kuzitawala zile hisia zenye jazba ( emotional impulses). Hisia kama hizo zikitawaliwa na kupelekwa katika idara nyingine za mwili zinaleta manufaa makubwa.
Mfano mzuri unatoka katika kitabu cha Think and Grow Rich cha Napoleon Hill. Anasema hivi, nanukuu:
"Sex transmutation is the most powerful tool in existence when it comes to creation, invention, accomplishment, creativity, advancement, and achievement."
Kwa maana nyingine nguvu hizo zinaweza kufanya mambo makubwa sana. Ukifanya utafiti unaweza kugundua viongozi wengi walioshindwa kugeuza hizo nguvu kufanya mambo mengine wameishia kuwa na wake wengi na watoto wengi.
Kusoma kuna faida maana tunafundishwa namna ya kubadili nguvu zetu na kuzitumia kwa namna tofauti yenye manufaa. Faida za akili hisia ni nyingi sana.
Mtu anapoweza kuzitawala hisia zake kwa ufanisi wa hali ya juu anakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi, yenye tija na hana tamaa. Kama ni kiongozi hatakumbana na kashfa zisizo na kichwa wala miguu.
Kwa hiyo sasa angalau Umeanza kujitambua and kujitawala kwa kanuni zako binafsi.
Akili hisia inatumia nguvu tulizo kufanya mambo kulingana na tabia zetu. Kazi kubwa ni kufanyia kazi tabia zetu.
#3. Hatua ya tatu ni Motisha
Motisha ni sehemu ya akili hisia. Lakini, nitoe maelezo kwanza. Unapokuwa nakazi halafu unajiwekea lengo la kupandishwa Cheo au mshahara kwa njia za ujanja janja, hiyo siyo sehemu ya akili hisia.
Kuna aina mbili za motisha. Motisha unayotoka nje (extrinsic motivation) na ile ya ndani (intrinsic motivation).
Watu wengi wanapata motisha ile inayotoka nje kama vile mshahara mkubwa au Cheo. Pia kufanya kazi na Makampuni makubwa au watu wenye hadhi fulani.
Motisha inayotoka ndani ipo kwa watu fulani ambao wana akili hisia inayowawezesha kufikia malengo bila kuwa na tamaa au sababu za kutaka kupata sifa au kujionesha ili wapate umashuhuri.
Kwa hiyo tufanye nini kujiongezea motisha? Tumia diary au journal kuandika mafanikio yako. Utajikuta unajijengea motisha na kuongeza mara dufu akili hisia zako.
Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Harvard Teresa Amabile alisema ya kuwa kitu pekee cha msingi kitakachokupa motisha ni zile hatua unazopiga (progress) katika kutenda kazi unayoamini ni muhimu kwako. Kwa hiyo hatua mbele, hakikisha umeweka kila kitu kwenye kumbukumbu zako.
Leo tumalizie kuhusu akili hisia na hayo mambo matatu ambayo yamejikita zaidi katika utawala binafsi wa mtu au mazingira ya ndani.
Siku nyingine tutamalizia kuhusu akili hisia kwa kuangalia jinsi tunavyohusiana na mazingira ya nje, nay a watu wengine:
#4. Uelewa (Empathy)
#5. Ujuzi wa Kijamii (Social Skills)
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia, maana najisikia vizuri sana ninapoweza kuwa msaada kwa mtu. Mimi ni mtumishi wenu. Na kwa vile umeamua mwenyewe kuwemo humu basi huna budi kuhakikisha tunajadili kwa pamoja na kufikia suluhisho muafaka kwa maisha yetu.

Maoni

  1. Nashukuru kwa somo natamani na mimi niweze kutumia hisia zangu

    JibuFuta
  2. Nashukulu kwa au au au au

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...