Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wazo La Leo:


Tunaishi nyakati ambazo Ninaziita ni nyakati za habari (Information age). Taarifa vidoleni.
Ukweli ni kwamba upande mmoja wa shilingi ni jambo Jema sana lakini upande wa pili ni jambo baya sana.
Kwa nini tuseme hayo.
1. Ni nyakati nzuri kwa sababu sasa hutumii nguvu na gharama nyingi kupata taarifa kwani ziko kiganjani.
2. Kipindi hichi ni kibaya kwa sababu taarifa nyingi ni mbaya kusikiliza na hata kuangalia, hivyo sehemu ya pili ya ubongo wako inayoitwa subconscious mind inaathirika sana. Na kumbuka sehemu hii ya akili kwanza huna udhibiti nayo lakini ndiyo eneo unalolitegemea kwa 90%. Kazi ya eneo hili ni kurekodi kila kitu unachosikia na unachoona na pili inaamsha matendo ambayo wewe huna udhibiti nayo. Nitakupa mfano mdogo na kwa kuwa site ni watu wazima tutaelewana.
Chukulia mtu anayependa kuangalia Picha za ngono sana. Kinachozalishwa ni kwamba tabia za mtu huyu zitaanza kujifunua kwa kufanya ngono sana mpaka jamii ikamtambua hivyo lakini mwenyewe akifanya anajutia kwa kuwa nguvu aliyoitengeza kumsukuma kufanya ngono ni kubwa mno na imefikia hatua hawezi kudhibiti. Hii ni hatari.
Mfano wa pili ni pale MTU anapopenda sana kuangalia Picha za kivita watu wakiuana sana. MTU wa jinsi hii katika maisha yake ana uwezekano mkubwa wa kuua na ikasemekana ameua bila kukusidia. Ushauri wangu kwa mfano huu wa pili kwa kukilinda kizazi chetu ni vyema tukawakataza kabisa watoto wetu na kuwaambia madhara. Hebu tuanze mapema kuwasaidia maana ndio wamezaliwa nyakati hizi sio sawa na sisi wahenga.
Kwa hiyo ni LAZIMA TUWE WACHAGUZI SANA WA NINI TUNASIKILIZA NA NINI TUNAANGALIA ILI TULINDE SUBCONTIOUS MINDS ZETU.
TVs NA MAGAZETI VINAONGOZA KUHARIBU subconscious MIND - utafiti unaonyesha 90% ya habari zake si nzuri kabisa zinatuharibu. Binafsi kwa ridhaa yangu siangalii TV na sisomi magazeti kabisa ikitokea labda Niko Restraurant na kuna TV au rafiki kanisisitiza kusoma habari fulani kwenye gazeti fulani, basi nitasoma hapo tu na kuliacha gazeti. Ushauri wangu chagua vipindi bora tu japo ushawishi wa kuangalia usivyochagua pia ni mkubwa. Mungu atusaidie.
Naomba niishie hapa kwa Leo nikikusihi kujilinda na unayoyasikia ili tujenge maisha bora.
Ni mimi mwalimu/coach - Seth Simon Mwakitalu 0788 493836/07140574/0754441325 


KARAKANA YA UBONGO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

Siri ya Maisha ni nini?

Siri ya mafanikio inaishi wapi? Wewe unajitambua? Muda wako wa kujiweka huru umefika. Ninakuweka huru kuanzia sasa. Je, uko tayari? Anza na maswali haya: 1) Huwa unalisha tumbo lako kila siku? 2) Huwa unalisha ubongo wako kila siku? 3) Huwa unalisha moyo wako kila siku? Ninakuweka huru kwa kukulipa sarafu yenye pande tatu kwa majina yake ni: #1. Jana yako #2. Kesho yako #3. Sasa yako Mwendo wa jaribio (experiment) Kwanza. Leo ni leo. Anza kutembea kuelekea kwenye mafanikio yako. Unaijua njia? Anza kutembea kwa miguu yako miwili. Kama huna miguu na uanze kufanya kile unachoweza utoke hapo ulipo hadi sehemu nyingine. Tembea kama vile maisha yako yote yanategemeana na kutembea huko. Kiuhalisia kutembea kwako ndo muujiza wa kujiweka huru. Unashangaa? Ni hivi: Miili yetu inashibishwa sumu kibao kwa hewa tunayopumua na vyakula tunavyokula. Hewa ina Carbon dioxide kutoka kwenye moshi wa magari (pollution) na viwanda. Vyakula vina dawa za mimea(pesticides). Itapendeza k...