Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UBONGO

Wazo La Leo:

Tunaishi nyakati ambazo Ninaziita ni nyakati za habari (Information age). Taarifa vidoleni. Ukweli ni kwamba upande mmoja wa shilingi ni jambo Jema sana lakini upande wa pili ni jambo baya sana. Kwa nini tuseme hayo. 1. Ni nyakati nzuri kwa sababu sasa hutumii nguvu na gharama nyingi kupata taarifa kwani ziko kiganjani. 2. Kipindi hichi ni kibaya kwa sababu taarifa nyingi ni mbaya kusikiliza na hata kuangalia, hivyo sehemu ya pili ya ubongo wako inayoitwa subconscious mind inaathirika sana. Na kumbuka sehemu hii ya akili kwanza huna udhibiti nayo lakini ndiyo eneo unalolitegemea kwa 90%. Kazi ya eneo hili ni kurekodi kila kitu unachosikia na unachoona na pili inaamsha matendo ambayo wewe huna udhibiti nayo. Nitakupa mfano mdogo na kwa kuwa site ni watu wazima tutaelewana. Chukulia mtu anayependa kuangalia Picha za ngono sana. Kinachozalishwa ni kwamba tabia za mtu huyu zitaanza kujifunua kwa kufanya ngono sana mpaka jamii ikamtambua hivyo lakini mwenyewe akifanya anajutia kwa kuwa ...