Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO JUU YA FEDHA /SHEKELI (SEHEMU YA 26)


Somo Juu Ya Fedha/Shekeli Sehemu Ya 26

Habari za leo mfuatiliaji wangu wa makala zangu za kila siku.

Bado tunaendelea na somo letu pendwa juu ya fedha/shekeli
Leo tunakwenda kujifunza juu ya kwa nini uko jinsi ulivyo.

Kwa nini uko njinsi ulivyo – Kuna mambo unatakiwa kuyajua ambayo yanachangia sana kukutengeneza na kuonekana jinsi ulivyo. Leo tunakwenda kuangalia jambo la tatu linalomtengeneza mtu:-

UMEZUNGUKA NCHI YAKO/DUNIA KWA KIWANGO GANI? – Kitendo cha kuzalia, kukulia, kusoma na kisha maisha katika nchi yako bila kuona sehemu nyingine ya dunia ikoje kumembupaza wengi na mbaya zaidi wengine wamezaliwa kijiji X wamesoma kijiji X wameoa kiji X na maisha yote hadi kuzeeka na kufa wangali kijiji X. Niambie mtu wa jinsi hiyo atakuwaje kuchukulia mambo maana ayajuayo ni ndani ya mipaka yake na wala hajui upande mwinge wa dunia mambo yakoje. Watu wa jinsi hii wameishia na maisha yasiyoridhisha na kuwa na mtazamo usiozidi mipaka yao.
Mithali 4:7

Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.

Ashukuriwe Mungu kuzunguka dunia haikuhitaji tena mpaka usafiri, waweza kutembea na kujifunza vitu vingi na kukubadili na kuwa mtu wa manufaa sana kupitia kusoma vitabu, kusikiliza vitabu, tapes,magazeti, videos, maandiko mbalimbali, wasifU wa watu mashuhuri, kufahamiana na watu mbalimbali nk. Vitu vyote hivi vinatusaidia kupata udhoefu wa maeneo mbalimbali kana kwamba tumekuwa tukisafiri sana kumbe la hasha.
Kile unachokichukua ili kikusaidie kukuza ufahamu wako kinahitaji uchaguzi maana vingine si vizuri. Hivyo yakupasa kuwa mwangalifu na kama huelewi bora uulize usaidiwe.
Chukua tahadhali kutojihusisha na vitu vitakavyoharibu hatima ya maisha yako.

 Mithali 23:23
Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.
Lini ilikuwa mara ya mwisho kujisomea kitabu?
Lini ilikuwa mara ya mwisho kwenda kutembelea nchi au mkoa tofauti na uishipo ili kupumzika na kujifunza?
Lini mara ya mwisho uliweza kujifunza kitu kipya kupitia kitabu, au video au magazeti au tapes au mafunzo nk?
USIKUBALI KURUHUSU KUTO JIFUNZA IWE KWA KUTOKA NJE YA MIPAKA YAKO AU AKUJISOMEA NK KUKUNYIME KUPANUKA KIMAWAZO. MUNGU ATUSAIDIE.
Acha kwa leo niishie hapa tutaendeleza somo hili katika Makala ijayo. Usikose kunifuatilia katika Makala zinazofuata.
Karakana ya ubongo tunatengeneza ubongo wako
Kwa wasioijua karakana ya ubongo ni watu waliojikusanya pamoja katika kundi la watsapp kwa lengo la kuondoa takataka kwenye ufahamu na kuanza kujifunza pamoja na kukutana angalau mara moja kwa mwezi ili kuwa chachu ndani na nje ya nchi.
Ili kujiunga yakupasa kuwasiliana nami ili kuweza kukufanyia udahili kama unavigezo vya kuwa mmoja wa wanakarakana ya ubongo.
Na kwa sasa tuna kitabu maarufu kiitwacho ‘KOPE ZAKO BAHARI YAKO’ na kama wewe ni mmoja ya wanaojipenda hiki kitabu si cha kukosa. Tuwasiliane na kuona jinsi ya kukipata.

Seth Simon Mwakitalu
Senior Auditor, Entrepreneurship Consultant, Coach and Lifestyle Trainer.
Tel:- +255 754 441325; +255 788 493836
Email: ssmwakitalu2013@gmail.com
Websites:www.karakanayaubongo.blogspot.com;
Instagram: karakana_ya_ubongo
Facebook: https://www.facebook.com/karakana-YA-Ubongo-109000130642880/?referr=whatsapp
You tube: karakanayaubongo
               
We empower people:-
1. Achieve life and Career goals through part-time business venture.
2. Acquire life changing business skills.
3. Prepare for retirement.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

Siri ya Maisha ni nini?

Siri ya mafanikio inaishi wapi? Wewe unajitambua? Muda wako wa kujiweka huru umefika. Ninakuweka huru kuanzia sasa. Je, uko tayari? Anza na maswali haya: 1) Huwa unalisha tumbo lako kila siku? 2) Huwa unalisha ubongo wako kila siku? 3) Huwa unalisha moyo wako kila siku? Ninakuweka huru kwa kukulipa sarafu yenye pande tatu kwa majina yake ni: #1. Jana yako #2. Kesho yako #3. Sasa yako Mwendo wa jaribio (experiment) Kwanza. Leo ni leo. Anza kutembea kuelekea kwenye mafanikio yako. Unaijua njia? Anza kutembea kwa miguu yako miwili. Kama huna miguu na uanze kufanya kile unachoweza utoke hapo ulipo hadi sehemu nyingine. Tembea kama vile maisha yako yote yanategemeana na kutembea huko. Kiuhalisia kutembea kwako ndo muujiza wa kujiweka huru. Unashangaa? Ni hivi: Miili yetu inashibishwa sumu kibao kwa hewa tunayopumua na vyakula tunavyokula. Hewa ina Carbon dioxide kutoka kwenye moshi wa magari (pollution) na viwanda. Vyakula vina dawa za mimea(pesticides). Itapendeza k...