Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hakuna Eneo Salama

Ashukuriwe Mungu kwa pumzi aliyotupa siku ya leo. Ombi langu kwako ni moja tu asubuhi ya leo – TUKAITENDEE KAZI HII PUMZI KWA MAAMUZI YETU NA ZAIDI SANA MATENDO YETU YA SIKU YA LEO.

Yawezekana wewe ni mmoja wa watu wasio wepesi kujaribu vitu kufanya ukihofia labda kupata hasara au kuumizwa na mengine mengi ambayo ni vikwazo kwako kuchukua hatua. Kifupi ni mtu unayejipenda sana kiasi cha kuona kwamba hutaki kitu kiwayo chochote kibaya kikutokee na hivyo umebeba tabia ya kuwa mwangalifu kupitiliza (Overcautious behaviour).

Naomba nikuonye – HUTOFIKA MBALI.

Ukweli wa maisha ni huu – Tangu tunazaliwa hadi tunakufa hakuna sehemu yoyote iliyo salama. Mimi nakushangaa wewe unayetafuta sana kujilinda usipatwe na hasara/mabaya.

Mifano michache upate kunielewa:-
1. Tendo la wewe kuzaliwa tu lilijawa na hatari/hasara kibao, mojawapo ungeweza kuyatoa maisha ya mama akafa na ukaishi pasipo kumwona mama yako. Lakini hilo halitoshi, hata wewe mwenyewe ungeweza kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa au hulijui hilo. Waulize wazazi wakujuze.


2. Utoto wako wakati wa makuzi ni shiiiiiida maana ulikuwa ukijaribu kila kitu yumkini ungekunywa sumu ukafa. Niseme nini upate kuelewa nikuelezacho? Hakuna mahali salama katika maisha.

3. Kwenda kitandani tu kulala ni hatari maana unaweza potelea usingizini. Wangapi umeshuhudiwa kama si kuambiwa ya kuwa fulani alifariki akiwa amelala. Sasa unatakaje baada ya kujua hata kulala ni hatari. Nakuona unawaza ya kwamba kuanzia leo utakuwa macho hutataka kulala ili usije kufa kitandani. Naomba nikupe pole kwani hata kukesha ni hatari kwani waweza kupoteza maisha ukiwa unakesha maana utakuwa unapambana na usingizi na kitendo hicho chaweza sababisha mapigo ya moyo kwenda kwa kasi na ukafa. NINACHOTAKA UKIELEWE HAKUNA MAHALI SALAMA PA KUJIFICHA UKASALIMIKA.

4. Nakuona unasema wewe u muumini mzuri na una uhakika unaenda mbinguni. Ni vyema kabisa na nakuunga mkono. Lakini ukiulizwa je leo Mungu akuchukue maana duniani ni shiiiiiida utaruka na kusema du mbona bado sijatenda aliyokusudia niyafanye duniani. Lakini unajua huwezi kwenda mbinguni ukiwa hai; lazima ufe. Du kumbe ni hatari kiivyo kufa bila kujiandaa. Wapendwa wetu wengi wametutoka pasipo kutarajia. Hakuna sehemu salama.

5. Mtu mmoja alinichekesha akasema – Anahitaji kuishi miaka mia hivyo anatafuta kona ya kuishi ili asikumbane na hatari/hasara zilizopo duniani. Kikubwa atahitaji apelekewe chakula kwenye kona atakayochagua kuishi. Mpendwa hata kwenye kona ni hatari. Utajisaidia wapi? Mbona utaoza ukiwa hai. Maana kisichotumika hupotea. Mungu atusaidie.

Ni bora kuishi maisha ya matukio mbalimbali yaliyojaa furaha, huzuni, kutapeliwa, kupata hasara, kufilisika kabisa, watoto kufukuzwa shule ati hawajalipa ada, kutolewa vyombo nje kisa hujalipa kodi, kutembea kwa mguu kwa kukosa sh. 400 za dalala, kulia kwa kuumizwa kwenye mahusiano, kudhalilishwa kwa kudaiwa madeni na kupitia hayo ukakomaa na kuwa mtu bora sana kuishi duniani. Kwa lugha ya wenzetu unakuwa UNSTOPABLE au niseme unakuwa sugu.
Maisha ya jinsi hii ndiyo haswa yamfaayo mwanadamu kwani kupitia hali hizo hata ubongo huamka na kuanza kuangalia njia mbadala za kuishi na huko ndio kukua kwenyewe. Wazungu wana msemo usemao ‘BETTER TO LIVE 30 YEARS FULL OF ADVENTURE THAN A 100YEARS SAFE IN THE CORNER’

Acha kumbwela mbela, chukua hatua, ukipata hasara utakuwa umejifunza. Hizo ndizo staili za kuelekea mafanikio. Kifupi unatakiwa kupigika sana ili ufanikiwe sana. Hakuna chuma imara duniani ambacho hakijapitishwa kwenye moto mkali.
Ushuhuda wangu wa maisha nikisimulia mkanda mzima wengine mtatoa machozi. Kifupi nilifika mahali hata sh. 400 ya dalada mfukoni hakuna nikiwa na watoto watatu, mke, na dada wa kusaidia nyumbani.
Kuna wakati nilishindwa kutoka nje ya chumba changu nikiwa kitandani nagalagala na ndipo nikajifunza nikiwa kitandani ya kwamba kamwe nisiseme WHY ME bali niseme TRY ME kwa hiyo yoyote utakayopitia ni ili kukuthibitisha ya kuwa wewe ni ngangari yaani si wa kawaida. Acha kulia lia chukua hatua.

Nimalizie kwa kukomba anza kusoma vitabu na kutushirikisha kwenye kundi la karakana ya ubongo hicho utakachokuwa umesoma angalau kurasa kumi kila siku kitakushangaza matokeo utakayoanza kuyapata. Kikubwa utaanza kubadilika namna ya kufikiri Ukiweza kufanya hili nakuhakikishia taratibu fikra taka zitaanza kukutoka. Anza leo.

Nataabika hapa nilipo ili unielewe unachokosa kwa kutosoma vitabu. Mafanikio huja kwa kuwa na maarifa mbalimbali ambayo njia rahisi ya kuyapata ni kupitia vitabu. Bill gate hadi leo ni msomaji mzuri wa vitabu.


Swali – Wewe na Bill Gate nani kafanikiwa? Mwenye kunielewa kanielewa.

Tenga muda kila siku angalau nusu saa asubuhi na nusu saa jioni kwa ajili ya kufanya tendo adimu la KUFIKIRI tena jizoeze kufikiri kwa ubora wa hali ya juu. Tabia hii itakurahisishia mambo mengi bila kutumia nguvu nyingi. Maisha ni mafupi tenda kila lililo jema.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...