Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kujenga mfumo wa maisha wenye tija.

Habari za asubuhi mfuatiliaji wa masomo ya kila siku kwa jina maarufu la wazo la leo.Leo nimeonelea vyema nigusie juu ya kujenga mfumo wa maisha wenye tija.
Ninapokwenda kuelezea hili napenda kila mmoja atambue jambo moja ya kuwa mwanadamu kwa asili ni mvivu au kwa lugha nyingine miili yetu kwa asili inapenda kustarehe au kwa msisitizo kubweteka. Wahenga walisema, kumjua adui ni nusu ya ushindi kwani inakuwia rahisi kupanga mikakati ya maangamizi.
Shida kubwa kwa mwanadamu ni kwamba vita hii ni ya kila siku na mbaya Zaidi adui huyu unaye kila uendako na achelei kukusemesha. Mwili unaongea sana na ukiuendekeza utakuletea madhara maishani. Lugha kama nimechoka, siwezi, acha nipumzike, raha jipe mwenyewe na mengine mengi yanadhihirisha asili ya mwili na hapo mwili unakusemesha mpaka uutimizie.
Wapo watu wametengeneza tiba kuhakikisha mwili unatia adabu. Mfano – Kimsingi mwanadamu anayejitambua ni lazima awe nje ya kitanda kabla au saa 11 asubuhi. Nachelea kusema hiyo ni kama kanuni, uwe umeajiriwa au la. Hapa wengine utasikia, hata sasa wewe usomaye unajisemesha ya nini kujitesa asubuhi yote na kausingizi katamu tena nimejiajiri. Ni aibu unakuta mtu kaamka saa nne kajifunga taulo ati ndio katoka kitandani. Mungu atusaidie tujitambue maana dunia kamwe haitatuacha salama. Hivyo wengine wanaweka alam (kishitukizi) ili wajilazimishe kuamka. Hapo sasa ni vita, mwenzangu na mimi wasiojielewa utakuta akifunua shuka au blanket akakutana na kabaridi anajisemea ngoja nilale kidogo kausingizi katamu na wengine huzima alam na kuendelea kulala.
Naomba nikueleze, yakupasa kutengeneza mfumo wa jinsi siku yako itakavyoanza na kumalizika. Kuna baadhi ya vitu utavipanga kutekeleza kila siku mpaka mwili uzoee. Hii inasumbua sana na mara nyingi watu huanza kwa hamasa na kisha uacha walichojipangia na kurudia uzembe uleule. Wanasaikologia wanasema; tabia mpya huchukua siku 21 mfululizo kuamrisha mwili ukubali. Kwa lugha nyingine kuushinda mwili juu ya vijitabia lukuki vya uvivu na kuanzisha tabia ya ukokomavu na kujibidisha kwa kila utakachopenda kufanya maishani, itakulazimu kurudia rudia angala mara 21 pasipo kuacha ndipo mwili husaklimu amri na tabia mpya kuanza.
Mfano, suala la kuamka kabla au saa kumi na moja. Dawa ya muda mfupi ni alam. Hapa inabidi ujisemeshe iwe isiwe alam ikipiga nitakurupuka bila kufikiria niamke au nisiamke kwani mwili utakushinda ukianza kujifikirisha, wewe kurukupuka kitandani kila siku na siku 21 sikipita kwa kufanya hivyo - shangilia ushindi utakuwa umepatikana kwani sasa utakuwa unajikuta muda ule wa alam ukifika unaamka upende usipende na hapo sasa unaanza kujenga tabia mfumo ya kwanza ya kwamba utakuwa unaamka kila siku saa 11 na wakati mwingine kabla na mara moja kuanza na vijidabia ulivyojijengea vya kila siku kuvifanya.
Leo nitakupa mifano ya kutosha kujijengea vitabia vya kila siku. Nawe utachagua na kujiongezea katika orodha yako na ikifika jioni unajisahihishia kuona kana kwamba ushindi juu ya mwili wako unapatikana. Mifano ni kama ifuatavyo:-
1. Kuamka saa 11 asubuhi kila siku bila visingizio.
2. Kujisomea kitabu walau kwa 30 dakika. Kitendo hichi ni muhimu sana kuiongezea akili maarifa. Utasaidika sana kwani itakurekebishia namna unavyofikiri na kuchukulia mambo. Jenga tabia ya usomaji kila siku walau kwa dk 30.
3. Kuhakikisha unafanya mazoezi kabla siku yako haijaanza. Nisemapo mazoezi namanisha kama vile kutembea tembea angalau dk 30, kuruka ruka kamba angalau dk 30, kuendesha baiskeli walau dk 30, kupiga push up angalau dk 30, kuchezesha viuongo angalau dk 30, kukimbia, kurukaruka na mengine mengi. Ukifanikisha hili utaifanya akili yako iwe sharp.
4. Kutahajudi (Meditation) asubuhi na usiku. Kama hujui kutahajudi. Naomba tuwasiliane maana ni somo tosha na ni la muhimu. Vipengele nambari 1 hadi 4 hufanyika kabla hujatoka nyumbani. Kimpangilio anza na kutahajudi kisha kujisomea na mwisho mazoezi. Hapo tayari utakuwa muda umefika wa kuanza siku. Utakachokiona ni mabadiliko makubwa yenye hamasa. Kazi kwako.
5. Kutokuwa mchelewaji wa makubaliano ya kukutana – utakuwa unawahi mfano dk 15 kabla wakati wowote mkiahidiana na mtu au ukiwa na kikao. Fanyia mazoezi mpaka inakuwa tabia yako.
6. Kuhakikisha kila wiki unawandikia angalau watu wawili kuwashukuru kwa yale waliyokutendea. Watu wengi huwa wanaishi pasi shukrani naomba wewe usiwe mmojawapo.
7. Kuweka msimamo mkali kupendelea matunda Zaidi kuliko vitu vya sukari ka ice crème, soda, pipi nisaidie kuendeleza orodha. Mwili utapenda ule vitu vitamu tamu. Kimsingi si vizuri vinachangia kuchakaza mwili na kukaribisha magonjwa kwa haraka. Au kuacha chipsi na ukala kipande cha muhogo uliochemshwa au kuachana na vyakula vya mafuta au tumia mafuta salama kama mafuta ya mzeituni au alizeti au kula michemsho tu. Kimsingi kujenga tabia sahihi ya ulaji inakubidi ujikane sana, ila ukifanikiwa ni njema mno kwa mstakabali wa afya yako. Soma sana na kuvijua vyakula vyenye manufaa na kuanza kuachana na vyakula vinavyodhorotesha mwili. Chagua maji badala ya soda nakuendelea.
8. Kunywa maji ya kutosha kila siku. Hakikisha kila siku unakunywa hitaji la mwili wako na ikiwezekana zidisha kidogo. Unajiuliza ninywe kiasi gani ili nijue nimetimiza hitaji la mwili? Jibu - Jipime uzito wako kwa kg kisha ugawanye kwa 24. Jibu utakalopata ni kiwango cha maji kwa lita kinachohitajika mwilini ili mwili ufanye kazi vizuri. Kipimo chake ni kuwa na mkojo mweupe ukojoapo. Mkojo ukiwa si mweupe tafsiri yake kama ni gari linachemsha.
9. Kujitathimini jinsi siku yako ilivyoisha. Pata sehemu tulivu anza kutembea kimawazo jinsi siku ilivyoisha.
10. Kutahajudi (Meditation)
11. Kupangilia vitu 6 muhimu vya kufanya siku inayofuata. Hili ni muhimu sana kwa kuwa linachukuliwa na ubongo uliofichika na hivyo ni msaada mkubwa wa utekelezaji kesho yake maana ubongo huu huwa kazini masaa 24. Ipo tofauti kubwa ya kimatokeo kwa mtu anaepanga kila siku na asiye panga usiku hata kama watafanya mambo yale yale. Hakikisha unajenga tabia ya kupangilia mambo ya kufanya angalau mambo 6 muhimu ya siku inayofuatia. Unashauriwa muda mzuri wa kupangilia mambo ya kutekeleza siku inayofuata ni kabla ya kulala.
Nini kifanyike? Unahitaji maamuzi magumu kama unapenda maisha. Binafsi nimeamua kusaidia watu kupitia kundi maalum la watsAp. Wanaoruhusiwa kuingia huko ni watu wanaotafuta namna ya kutoka katika maisha. Kama wewe unapenda tuwasiliane maana kuna mchujo kuona kama unafaa au la. Nitakufanyia udahili/interview na nikijiridhisha nakuingiza kwenye kundi. Huko kamwe hutaona selfie, wala kulingishia watu aina ya chakula unachokula, wala mambo ya mapenzi nk.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...