Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kukuza akili/ufahamu(mind development)

Habari ya leo mpendwa msomaji wa Makala zangu za kila siku sijulikanazo kwa jina la Wazo La Leo.
Ni kawaida kusikia watu wakilalamika ya kuwa wanapenda sana kufanya biashara lakini tatizo hawana mtaji kuwawezesha kuanza biashara. Yawezekana hata wewe usomaye hii makala ni mmojawapo. Hili limewafanya walio wengi washindwe kuona mtaji wa kwanza ambao kila binadamu amezaliwa nao.
Ikumbukwe na kuamini ya kuwa mwenyezi Mungu katika uumbaji wake alihakikisha kila binaadamu aliyemuumba alimkabidhi mtaji wa kuendesha maisha yake pasi shida yoyote. Mtaji ninaoongelea hapa ni AKILI. Akili ni kila kila kitu linapokuja suala la mchakato wa kutatua matatizo (changamoto).
Shida kubwa kwa tulio wengi huwa hatutengi muda wa kufikiri na mbaya kuliko vyote hatuna tabia ya kukaa eneo tulivu ambalo ni muafaka kwa zoezi la kufikiri.
Kuna nyakati akili zetu hutupa mawazo (Ideas) nzuri sana kutekeleza na kufanikisha kile tumekuwa tunakitafuta kwa muda mrefu lakini kwa kujua au kutokujua mawazo haya huja na kuondoka kutokana na tabia yetu mbaya ya kutokua na utamaduni wa kuyaandika mawazo yote yanayotujia na kinachotokea mawazo haya hupotea na kamwe hatuwezi yakumbuka.
Katika Makala yangu ya jana nimeongelea suala la mtu kuwa na noti buku yenye ukubwa wa kuenea mfuko wa shati na leo naendelea kusisitiza ya kuwa hilo ni hitaji muhimu sana kwa kila anayetaka kubadili maisha yake. Hii itakuwezesha kuyapakua mawazo yako kirahisi kwa kuyaandika kwenye hicho kinoti buku.
Ikumbukwe kuwa ili kukuza akili yako/ufahamu, yakupasa kuifanyisha mazoezi mbalimbali kama ilivyo miili yetu tunapoifanyisha mazoezi na kujikuta tu wakakamavu na maradhi mbalimbali kutuachilia.
Nimalizie kwa kuanisha aina ya mazoezi ambayo akili haina budi kushughulishwa ili iweze kukua na kukusaidia kuendesha maisha yako kirahisi.
1. Kujisomea vitabu sahihi kutoka kwa watu mashuhuri
2. Kusikiliza video/audio zilizosheheni hotuba au mafunzo kutoka kwa watu waliofanikiwa
3. Kuhudhuria mafunzo sahihi, maana siku hizi vituko haviishi. Mafunzo mengine huharibu akili badala ya kujenga.
4. Kutengeneza mazingira ya kuwa unakutana na watu waliofanikiwa ili kupata wasaa wa kuwauliza na kupokea ushauri wao inapobidi.
5. Kushikamana na watu chanya na kuachana watu hasi kabisa.
6. Kuanza kuweka katika matendo mambo yote mazuri unayojifunza na kubwa zaidi ni kuendelea maana wengine ni moto wa mabua. Unakuta mtu amehamasika kwa siku tatu na baadae anarudia tabia zake zilezile alizozizoea (comfort zone). Hii ni sawa na kuchimba shimo na kulifukia au kujenga nyumba ya miti hewani. Yaani hakuna kinachofanyika. Kikubwa ukijifunza kitu kifanyie kazi mpaka kimekuwa sehemu ya maisha yako na hapo ndipo utaanza kuona mabadiliko.
7. Orodha inaendelea, lakini uhakika nilionao, akili yako itapevuka/itakua vizuri na kugeuka kuwa mtaji wako nambari moja katika maisha yako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...