Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Makundi manne ya watu

Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa siku nyingine nzuri yenye baraka ambayo tunakwenda kuitumia vizuri ili kuboresha maisha yetu.
Leo tunakwenda kujifunza kwa pamoja juu ya makala inayokujia kila siku ijulikanayo kwa jina la “Wazo La Leo”. Hivyo kwa leo nitajikita zaidi kuelezea makundi makubwa manne ya watu linapokuja suala la muda na fedha/kipato/shekeli. Nini maana ya haya makundi? Na je we uko kundi lipi. Sipendi na wala sihitaji unitajie kundi lako acha ibaki kuwa siri yako. Lakini upande wa pili wa shillingi nakuuliza iwapo kila kitu kingekuwa sawia kiasi cha kujichagulia kundi mubashara, je wewe ungejichagulia kundi lipi kati ya hayo manne?
Majibu yote juu ya maswali hayo manne yanabaki ndani ya nafsi yako usije nizulia kesi ati nimekwambia uko kundi flani acha ibaki kuwa msala wako. Kikubwa ufanye nini kutoka kundi ulilopo ambalo pasipo kumung’unya maneno uko kundi la hasara au kwa lugha nyepesi hujatambua ulikuja duniani kufanya nini? Wengi hudhani lengo la Mungu kuwaruhusu kuja duniani ni kutembeatembea tu na kuvuta hewa maridhawa na kisha kutoweka hapa duniani. Sipendi na wala sitamani wewe rafiki yangu uwe wa namna hiyo. Maana ukiwa ndivyo ulivyo basi wewe ni maiti inayotembea. Mungu atusaidie.
Umeendelea kuwepo mahali ulipo kwa kuwa tu hujui kujiweka katika kundi sahihi (POSITIONING RIGHTLY). Rafiki yangu mpendwa nimemwomba Mungu atusaidie tuhame huko tunakoshambuliwa na chawa wa umaskini na tujiweke mahala sahihi.
Nakuona unatokwa na mate kama fisi aliyekosa nyama huku mate yakikutoka ukitaka kujua hayo makundi ili ujijue utafikiri uko makini kumbe unacheza mdundiko na kusahau sufuria la kuchemshia maji ya kupikia dona kwenye jiko la umeme tangu saa sita hadi saa kumi na mbili jioni na kukuta nyumba imewaka moto kwa tatizo la moto uliotokana na sufuria kuyeyuka hadi kusababisha moto ulioteketeza nyumba nzima. Je umakini wako uko wapi?
Makundi manne ya watu tunapohusisha pesa na muda ni kama yafuatavyo:-
1. Watu wenye muda lakini hawana pesa, kila siku kuombaomba.
2. Watu wenye pesa lakini hawana muda
3. Watu wasio na pesa wala muda – kila siku na kila saa wako busy.
4. Watu wenye pesa na muda
Naomba niyaelezee haya makundi ili uweze jua kwa hakika kundi lako na uweze anza kuchukua hatua za kujongea kwenye kundi sahihi.
1. WATU WENYE MUDA LAKINI HAWANA PESA – Hili ni kundi la watu ambao nakosa lugha sahihi ya kuwaelezea. Ni watu wanashabikia vijiwe kama kucheza karata, mara Magufuli mara Lowasa, mara Mbowe nakadhalika, kulala chini ya vivuli vya miti, kushinda nyumbani wakiangalia tv wengine kwa kisingizio cha kumpenda Mungu kwa kusikiliza nyimbo za injili kutwa nzima lakini kanisani sadaka ni shida. Wengine waishia kuwa mateja ya kuangalia mpira kwenye channel maalum za kuonesha mpira ukiwauliza watakwambia wana ndoto ya kuwa kama Mbwana Samata siku moja. Wengine vijiwe vya kusukana nywele kusikoisha. Ukifuatilia wamejawa na habari kibao utadhani ni waandishi maarufu wa habari kama ilivyokuwa kwa wakati huo marehemu Ben Kiko wa Tabora. Wahenga wenzangu watanisaidia kumkumbuka mwandishi machachari marehemu Ben Kiko. Wengine ni kuchat siku nzima utadhani mazezeta maana ukiongea naye yeye anachat na huku anaitikia ndio kila kitu. Ukimwambia acha simu anasema unafikiri sikusikii na ukimuuliza nimesema nini anasema tuko pamoja. Hawaishi kutumatuma picha na kuforwad message mara Lulu kafungwa mara Tundu Lisu mara lile kifupi ni shida. Mkikutana tu anaomba pesa ya bando. Acha niseme kidogo hapa. Hivi inawezekana vipi simu ya mkononi ikufanye wewe teja? Ni kivipi huwezi zima simu ukafanya jambo la maana. Unasingizia baby atakutafuta na akikukosa utajuta kuzaliwa. Huyo si mume wako bali mwamkosea Mungu kwa ujinga mnaotendekeza. Nisiwachoshe, wahenga walisema usimwamshe aliyelala..
2. WATU WENYE PESA LAKINI HAWANA MUDA – Kundi hili la watu wana pesa. Namaanisha wana pesa. Kwao pesa si shida hata kidogo. Kifupi wanazo. Tatizo kubwa hawana muda. Kuondoka nyumbani ni asubuhi sana kabla watoto hawajaamka na kurudi watoto wakiwa wamelala. Wao ibada yao ni kusaka pesa mpaka wamekuwa watumwa wa pesa. Dili zote za mjini wanazijua na huwakosi. Kwenye orodha ya makonda wamo, makinikia wamo sijui uwatafute wapi wasipopatikana. Maisha ya jinsi hii yanapoteza ladha ya kuishi. Mara nyingi walio wengi mahusiano na wenzi wao ni shida.
3. WATU WASIO NA PESA WALA MUDA – Kundi hili ni kundi la ajabu sana maana hujishughulisha na shughuli za hovyo au kwa lugha nyingine hushughulishwa na vitu visivyo na tija. Unakuta mtu kutwa nzima yuko mara kariakoo mara manzese mara kimara suka lakini hawajulikani wanafanya nini. Ukimhitaji anakuambia niko busy. Unajiuliza huko busy ndio wapi? Ukimwambia niazime Tshs. 100,000 anakwambia aliyekupa wewe ndiye aliyeninyima mimi. Ni shiiiiiiiiiiiiiiiiiida.
4. WATU WENYE PESA NA MUDA – Kundi hili hawafanyi kazi ili wapate pesa bali hufanya kwa kuwa wanapenda kufanya kazi kwani kwao - wafanye kazi wasifanye pesa inazidi kuwafuata maana wana vitega uchumi lukuki. Hivyo wana muda wa kutosha kukaa na familia, kupata muda wa likizo ndani na nje ya nchi kwao si tatizo wakati wenzangu na mimi likizo ni mpaka afiwe. Mungu tusaidie kujitambua na kubadirika
Kazi kwako. Najua japo hujaniambia kundi lako si la 4 ni hayo kati ya matatu. Karibu tuanze safari kuelekea kundi la nne. Wenzako tuliisha anza huko kwenye kararakana ya ubongo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...