Ninamshukuru Mungu kuiona siku nyingine tena. Leo nataka niongelee maswali muhimu maishani yampasayo kila mtu kujiuliza.
Ikumbukwe kwamba tunakaribia kuanza Mwaka mpya kwani tumebakiwa na mwezi mmoja tu. Hivyo nimeonelea vyema niongelee maswali manne muhimu mwanadamu anayejitambua hana budi kujiuliza katika maisha haya tuliyo nayo:-
1. Ni nini
2. Lini
3. Kwa nini
4. Kwa namna gani
Kimsingi kila mmoja wetu hana mudi kujua kusudio la yeye kuruhusiwa kuwepo hapa duniani. Kumbuka hatukuja kupumua tu tukapita. Liko kusudio maalum ambalo Mungu ameweka ndani yako ambalo anataka ulitimize.
Mimi na wewe yawezekana kabisa hatujawahi kukutana ana kwa ana ila uhakika nilio nao ni kwamba wewe ni mtu wa thamani sana kwani una uwezo mkubwa ajabu wa kuweza badilisha kabisa maisha yako na ukabaki kuwa simulizi. Hivyo kujua kwa hakika kusudio lako la kuwepo hapa duniani ni jambo kuu na la maana kwa kila mmoja wetu.
Kujua ni nini unahitaji si mwisho na kiuhakika hupoteza maana hadi pale utakapojua muda au siku maalumu ya hicho unachokitaka kuwa nacho. Hivyo ni vyema kabisa ukajua ni nini unahitaji na lini ukipate hii hukusaidia wewe kuulazimisha ubongo ufanye kazi kwa kasi kukamilisha hayo mawili. Haya ni maswali mazuri yanayotambulisha nini na lini.
Sasa baada ya kujua nini na lini unataka, ni muhimu kuelezea kwa undani ni kwa nini hicho unachohitaji ni muhimu. Hapa ni mithili ya gundi kushikamanisha nini, lini a kwa nini. Unapoelezea sababu za kuhitaji unacho hitaji, kiwango chako cha hamasa huwa juu maana unagusa hisia zako. Tendo hili mara moja huzalisha nguvu ya utekelezaji kwa umakini. Ninachomaanisha hapa ni kwamba kuwa na sababu kimsingi hukufanya ufanye kazi kwa kujituma.
Mwisho, ni kwa namna gani unaweza fanikisha ni swali lingine litakalokufanya sasa upange mikakati ambayo ni muhimu sana kukamilisha mduara wa nini, lini, kwa nini na kwa jinsi gani/namna gani.
Rafiki, anza sasa kuamsha ubongo wako kwa kujiuliza maswali haya muhimu ili uweze zalisha hamasa na juhudi kubwa ya utendaji na hivyo uzalishaji wako utaongezeka maradufu na thamani yako katika jamii itapanda.
Nikutakie siku njema na yenye Baraka tele.

Maoni
Chapisha Maoni