Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Matumizi ya whatApp na simu.

Habari za leo rafiki na mfuatiliaji wa Makala zangu zijulikanazo kwa jina la wazo la leo. Leo nimeona vyema nizungumzie juu ya matumizi ya na whatApp na simu.
Maendeleo ya technologia yametuletea ulimbukeni uliokithiri. Utakuta mtu kutwa nzima yuko kwenye watsApp utafikiri ni mfanyakazi wa mgodi wa Buswagi amepangiwa shift na haruhusiwi kutoka inamlazimu akazane kuchimba madini.
Ukifuatilia kwa makini unagundua tayari mtu amekwisha kuwa teja wa watsApp maana haipiti dk mara kujiselfie na kutuma mara kapokea picha ya mwenzake anakula, mara katumiwa picha za watu waliokufa kwa ajali mara Diaomond mara nini yaani taja uwezayo. Akilala usiku ni mang’amung’amu maana mapicha mchanganyiko kichwani yanaanza kumsumbua. Utakuta kakurupuka kitandani ati anaota wanataka kumua na vituko vya kila aina. Huo ni ulimbukeni na uteja wa hali ya juu.
Ukifuatilia hali ya uchumi utakuta hoi bin taabani. Unakuta mtu ni rafiki tu wa facebook hata hamjawahi onana anakuomba pesa ya bando. Tunakwenda wapi?
Naomba niongelee madhara ambayo mtu anayapata kwa kujiendekeza huko.
Kimsingi mwanadamu ana ufahamu uliogawanyika katika maendeo makuu mawili. Eneo la kwanza ni ubongo wa nje (Conscious mind) na ufahamu wa pili ni uliojificha (Subconscious Mind). Bongo hizi zinafanyaje kazi?
1. Ubongo wa nje – Hapa ndipo kujifikirisha hufanyika. Hata maamuzi yote hufanywa na sehemu hii ya akili. Utaposema kesho nitakwenda mwanza kununua dagaa wa biashara, ukweli ni kwamba uamuzi umetokea kwenye eneo hilo la ubongo. Unaposema nimechoka ngoja niende nikasome tena. Yote yanafanyika katika eneo hili la ubongo ulio wazi. Kikubwa ninachotaka ukijue ni kwamba, mchango unaotolewa na eneo hili la ubongo katika kufanikisha maisha yako hapa duniani ni 10% tu na iliyobaki hutoka kwenye ubongo uliofichika ambao hukupatia 90% ya mafanikio yako hapa duniani. Hivyo huhitaji kuwa na degree kujua eneo lipi uelekeze nguvu zako ili kuwa mwanadamu unayejitambua. Hivyo nisikucheleweshe, ngoja nianze kudadavua juu ya ubongo uliofichika.
2. Ubongo uliofichika – Kazi kubwa ya ubongo huu ni kunakili na kutuhifadhi. Inanakili nini? Eneo hili linanakili yote unayoyaona na kuyasikia pasi wewe kujua. Sasa inategemea wewe unapenda sana nini? Basi hivyo vinajazwa katika ubongo uliofichika. Sasa nini kinatokea katika yale yote yanayonakiliwa kwenye ubongo huu? Kimsingi hapa ndipo yanapozaliwa matendo yajulikanayo kama YASIYOKUSUDIWA. Yaani mtu hujishangaa nimefanyaje hili? Na ukimwambia arudie hawezi, utakuta anaishia kusema ni Mungu tu. Sikatai uweza wa Mungu lakini kikubwa ninachotaka uelewe ni kwamba matendo yote yasiyokusudiwa huzalishwa na eneo hili la ubongo. Na mchakato huanzia kwenye ubongo wa nje kisha huachilia kwenda kwenye ubongo wa ndani au uliojificha.
a. Watu wote waliotambua hili tayari wamestuka na kuanza mikakati ya kujilinda ya nini wanaangalia na kujisikilizisha. Mimi nimekataa kuangalia TV maishani. Nikiangalia ni kwa bahati mbaya na si ridhaa yangu. Nimekuwa nikilala hotel mbalimbali lakini kamwe huwezi nikuta nimefungua TV. Utaniuliza hata taarifa ya habari huangalii?. Jibu ni kwamba hakuna taarifa ya habari duniani kote bali kujuzwa yaliyojili sehemu mbalimbali yaani mabaya na mazuri. Cha kushangaza mabaya huwa takribani 90% na mazuri !0%. Sasa kwanini nijikoroge kwa ajili ya asilimia 10%. Waandishi wa habari wote wanajua namna nzuri ya kuuza habari ni kuleta habari mbaya mbaya na zinauzika kweli. Mfano kafumaniwa, Fulani atembea na.., Ajali mbaya yaua - tusamehe kwa picha hizi na wewe unakenua mimacho kuangalia pasipo kujua unajiharibu kupitia ubongo uliofichika. Au unakuta mtu anakupa habari za kukukatisha tamaa na wewe unampa nafasi ya kumsikiliza, hujui unajimaliza. Ukitaka habari, sio kusoma gazeti au kuangalia TV. Habari kwa kiingereza inaitwa breaking news (watoto wa mjini wanasema ndio habari ya mjini) yaani itaongelewa ovyo ovyo na utaipata tu maana watu wanawashwa washwa kujulisha wengine ya nini kimetokea. Hiyo ndio habari na huhitaji kugharimika ili kuipata. Itakukuta ulipo. Nitawapa mfano live kutoka kwangu. Kumbuka siangalii TV na sisomi magazeti, lakini jana mtu anajiongelesha wala sijamuuliza ati ZITO kasema sana kwani polisi wamemvamia na kumpokonya computer na simu. Hiyo ndio ilikuwa breaking news. Nikamwambia asante na nakuomba usiendelee maana sihitaji kujua. Ninalinda ubongo wangu wa ndani uweze kunizalishia 90% ikayonifaidisha maishani.
b. Nini kifanyike? Unahitaji maamuzi magumu kama unapenda maisha. Binafsi nimeamua kuzaidia watu kupitia kundi maalum la watsAp. Hapo ni karakana ya kushughulika na bongo za nje na zilizofichika ili kubadili maisha. Wanaoruhusiwa kuingia huko ni watu wanaotafuta namna ya kutoka katika maisha, basi hawana budi kuingia katika hiyo karakana. Kama wewe unapenda tuwasiliane maana kuna mjchujo kuona kama unafaa au la. Nitakufanyia interview nikijiridhisha nakuingiza kwenye kundi. Huko kamwe hutaona selfie, wa chakula wala mapenzi nk ni karakara ya ubongo tu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...