Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mwonekano Wako ‘Unaongea’

Siku zote hakikisha mwonekano wako unakuongelea chanya.
Kamwe usiondoke nyumbani kwako bila kuwa na hisia ya kwamba mwonekano wako ndio unaokuelezea unavyo hitaji kujitambulisha ya kuwa wewe ni mtu wa namna gani.
Tangazo pekee lililo la ukweli duniani kupata kutokea kubandikwa linasomeka ‘VAA SAHIHI’.
Ni rahisi kuonyesha dosari ya aina fulani kwa mtu kwa jinsi anavyonekana tu.
Kiukweli si haki, lakini ndio ukweli wenyewe. Upende usipende ndio mambo yanayoendelea kila siku kwenye maisha yetu.
Kuwa sharp kwani faida yake ni kukusaidia kufikiri kwa usharp (Look sharp because it will help you think sharp).
Unajua hata tembea ya kizembe inaathiri ufikiri. Tembea ukijiamini. Watu wengine wanatembea utadhani muda wowote ule anaanguka.
Mwonekano wako kwa nje una athari ya jinsi unavyofikiri na kujisikia kwa ndani.
Mwonekano wako unaongea kwako; lakini pia unaongea kwa wengine.
Heshimu mwonekano wako. Ili kujihakikishia unajiheshimu jiulize swali moja tu – Je nauzika. Wewe ni bidhaa. Jua hilo kuanzia sasa.
Asikudanganye mtu mwonekano ni muhimu.
Siku zote lipa mara mbili na nunua nusu ya idadi ili kulinda mwonekano. Nini maana ya usemi huu?
Maana ya usemi huu ni kwamba ubora ni wa maana sana kuliko idadi. Mfano, badala ya kununua viatu 5 ambavyo sio vya ngozi halisi ni bora kununua kiatu kimoja cha ngozi halisi.
Huoni ya kuwa ni dhahiri kwa walio wengi kuendelea kuishi pasipo kupiga hatua katika maisha kwa sababu tu ya namna wanavyofikiri. Linda ufikiri wako kwa mwonekano sahihi kwani viwili hivi vinahusiana sana.
Hebu fikiria tabia moja tu ya watu waliofanikiwa ‘HAMASA KUBWA’
FANYIA MAZOEZI YA KUJIKUBALI NA KAMWE USIRUHUSU KUTOJIKUBALI KWANI KWA KUFANYA HIVYO UTAKUWA UNAJIADHIBU.
Weka mikakati na ingia kazini. Ukishindwa kupangilia mambo ya kufanya kufikia malengo maana yake umepanga kushindwa kufikia malengo yako (If yo do not plan, you plan to fail).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...