Naomba nisaidie kuendelea kumshukuru Mungu kwa wingi wa rehema katika maisha yetu. Naamini umeamka ukiwa mwenye afya njema na tayari kuianza siku kwa shauku kubwa ya kufanya makuu.
Karibu katika wazo la leo ambapo tunakwenda kujifunza tabia tatu muhimu zinazotenganisha matajiri na masikini ambazo natamani wewe rafiki yangu uweze zijua na hatimae unajua nini faida yake katika maisha yako kwani wahenga walisema kumjua adui ni nusu ya ushindi.
Kwanza kabisa natanguliza wazo lenye kukufanya uchangamke unapolitafakari – Hivi ni kwa nini wale walio ajiriwa (wafanyakazi) na kumtumikia mwajiri wao, wengi wao hawana shughuli za ziada kuwasaidia kufupisha safari ya mafanikio? Wengi wamebweteka na uhakika wa msharahara.
Naomba nitoe angalizo kwa walioajiriwa wote.
1. Uhusiano wako na mwajiri wako ni kwa vile una siha nzuri kuweza kumzalishia na hivyo anahakikisha anakurubuni na vitu mbalimbali ili ujione umefika kama vile posho, pesa ya ziada kwa kazi za ziada, mikopo, pesa ya likizo, bima ya afya, NSSF orodha inaendelea kwani kila mwajiri ana namna yake ya kupofusha nguvu kazi yake iendelee kumuangalia yeye tu ndio kama suluhisho suluhisho. Amka huo ni umangimeza Lakini kumbuka pia kuna kitu kimoja muhimu sana ya kuwa yeye ndiye anayekudhibiti. Ngoja nikupe mfano kidogo – Mama yako anaumwa sana na unaona umuhimu wa kwenda kuomba ruhusa ili kumjulia hali na kuona namna ya kumsaidia. Sasa wakati wa kuomba ruhusa unaambiwa hakuna ruhusa kwa kuwa kazi zako hujamaliza na tena kuna ripoti ya kutuma makao makuu. Kinachouma zaidi huenda unayeongea naye ni sawa na mwanao lakini ndio boss wako. Hakika inaliza. Sasa umenielewa ya kuwa huna udhibiti na maisha yako. Utaendelea kucheza mziki autako kama hutaki toka. Mimi niliwahi kusoma historia ya utumwa. Moja ya kigezo cha mtu kuitwa mtupwa ni pale anapopokonya udhibiti. Na endelea kumwomba Mungu usije pata maradhi maana mahusiano yako yataanza kuingia matatani. Waajiri karibia wote hawapendi mfanyakazi mgonjwa na hata kama amekuwa mfanyakazi bora kwa zaidi ya miaka kumi kwao si suala la maana, lamaana kwao uwe mzima ufanye kazi afaidike na akili zako, muda wako na nguvu zako basi. Kulithibitisha hili hebu upate maradhi ya kushindwa kwenda kazini sema kwa takribani miezi sita na daktari anasisitiza usiende kazini. Unajua kitakachotokea – Unaanza kupewa nusu mshahara. Swali – Ni wakati gani mtu anatakiwa kusaidiwa fedha zaidi? Je akiwa mzima au Mgonjwa? Huhitaji kuwa na digrii kulijua hili. Mgonjwa ndiye anatakiwa pesa zaidi. Sasa mwajiri ankupunguzia kwa asilimia 50 na ukiendelea kuugua ikafika mwaka basi anakuachisha kazi hakutaki tena. Nini maana yake? Mwenye akili na atambue hilo. Sasa kwanini umebweteteka hutaki kuwa na shughuli ya pembeni hata kama inakuletea shekeli kidogo ni bora kuliko sifuri. Kazi kwako, mimi najisemea tu kwa sauti ya juu.
2. Kumbuka haya maisha tunayoishi hatujui ya kesho. Wako marafiki zetu wamepoteza viungo maalum kwa ajali mbalimbali na kushindwa kuendelea kufanya shughuli kwa waajiri wao na hivyo kupumzishwa kazi. Bado tu Hujastuka – Kalaga bao na ubosi wako.
3. Amani ni sawa na bahari tulivu lakini ziko siku za tufani ambapo bahari huchafuka pasi kuitamani. Vivyo hivyo na mahusiano kazini kwani kuna nyakati waajiri wanaonekana kunyanyasa wafanyakazi na hapo sitofahamu hutokea na kupoteza kibarua. Je ulijua ya kuwa siku hiyo ingefika? Sasa umepoteza kazi pasi kutarajia na unachanganyikiwa kwani huna pa kwenda. Lakini kama unagalikuwa na shughuli zako za pembeni, ingalikuwa rahisi sana kuziimarisha. Hadi hapa bado tu hujastuka. Kweli mkataa pema pabaya pana mwita. Usininukuu vibaya. Sikushauri uache kazi usije zua tatizo lingine maana huna maandalizi. Kama unatamani kuwa na shughuli zako binafsi ninakuomba tuwasiliane ili nikuelekeze maandalizi unayotakiwa kuyafanya kufikia kuacha kazi. Si jambo la kukurupuka usije itaambisha familia yako kwa machungu ya kulala na njaa na wakati mwingine watoto kufukuzwa kwa kukosa ada. Nakuomba sana tuwasiliane tupange mpango mkakati.
Naomba nikuulize swali – Utajisikiaje ukijua ya kwamba shughuli yako ya pembeni inakuzalishia maradufu ya mshahara wako wa kazini na kwa hakika umeanza kuiona barabara ya kuelekea kwenye utajiri au umilionea? Ninaposema utajiri au umilionea ninamaanisha kuanza kumiliki pesa ambayo huna matumizi nayo kuanzia Tshs. 2,300,000,000 ambayo kuitamka tu nataabika niitamkaje uweze nielewa. Naomba wafanyakazi wa bank kama sio BOT nisaidieni kuitamka hiyo tarakimu kwani mnyakyusa mie nimeshikwa na kigugumizi – Kyala atutule.
Naomba kwa leo niishie hapa kwa kusema kama utafika mahali na kutamka kwa kinywa chako na kusema “Ninajishughulisha si tu kukamilisha mahitaji yangu na familia bali nina mpango mkakati wa kuelekea kwenye utajiri/umilionea, kwa hakika utakuwa mtu wa hamasa kila wakati kiasi kwamba nyakati zingine unapata muda mgumu kuelekea kitandani kulala maana akili zako tayari zimekwisha kuanza kuona kule unako elekea.
Muda si rafiki tena kwangu. Nitaendelea na somo kesho maana huu ni utangulizi tu.
Kwa wale ambao wanasema wamechoka na hali za kiuchumi walizo nazo, naomba niwakaribishe kwenye kundi maalum la watssAp lijulikanalo kwa jina la “KARAKANA YA UBONGO”
Kumbuka: Kuingia kundi hili ni lazima kwanza ufanyiwe udahili/interview ili kubaini je wewe kweli una muelekeo? Usije tuletea virusi. Karibuni na Mungu awabariki.

Maoni
Chapisha Maoni