Namnukuu Jim Rohn ‘ Mafanikio ni pale unapokua umebadilika kiasi cha kuwa sumaku ya kuvuta mafanikio na wala usijidanganye kwa kufanya kazi sana kwa bidi ili kupata mafanikio. Mafanikio huvutwa na mtu aliyebadilika kiasi cha kuwa sumaku ya kuvuta mafanikio. Kubadilika ni shughuli pevu kushughulikia. Kazi kubwa ni kubadilika kifikra na hakuna njia nyingine Zaidi ya:-
1. Kujisomea vitabu kila siku na kupata maarifa mapya na unapochukua hatua ya kuyafanyia kazi mawazo mapya ndipo badiliko kamili kwako hutokea. Kwanini nasisitiza vitabu. Unaposoma kitabu kimoja unajifunza mambo ambayo yu mkini aliyekiandika imemchukua miaka 30 kuweza kuwa na hayo aliyoamua kuandika ili watu wengine waweze kujifunza. Hivyo kama utasoma kitabu kimoja kwa mwezi tafsiri yake ni kuwa umeweza kujifunza udhoefu wa mtu wa miaka 30 kwa mwezi mmoja. Sasa niambie utakapokuwa umesoma vitabu hamsini utakuwaje? Badiliko ni lazima na linanzia na fikra kwa kujaza mambo yenye tija na fikra taka kuondoka.
2. Kusikiliza/video/tapes za mafundisho kutoka kwa magwiji wa mafanikio kama kina Jim Rohn, Less Brown nk.
3. Kuhudhuria semina hata ikibidi kulipia pesa. Hua inaniuma sana pale mtu unamwambia semina ni Sh 20,000 na mtu analalamika ati kwa nini isingalikuwa bure. Kuna kanuni rahisi sana unatakiwa kuijua upatacho kwa urahisi hupotea kirahisi. Mwenye ufahamu na anase huo usemi. Angalia watu wa bahati nasibu mara tu wakipata mamilioni wanaishia kuchanganyikiwa na mwisho kufilisika kwakuwa hakuna jasho walilochangia kupata hayo mamilioni.
4. Kutana na watu chanya achana na watu hasi. Badiliko ni lazima.
Orodha yaweza endelezwa kadri uwezavyo, lakini jambo la muhimu ni kuwa mafanikio huvutwa na mtu aliyebadilika kiasi cha kuwa sumaku kuvuta mafanikio (Success is something you attract by a person you become’ Jim Rohn.
Watu wanalamika ati uchumi umebadilika maisha yamekuwa magumu. Ukweli ni kwamba maisha hayajabadilika ila sisi ndio tumebadilika kwa kutokuwa na maarifa ya kutosha kupambana na mazingira ya kiuchumi tuliyo nayo. Acha kupigania kubadili uchumi, shughulikia badiliko lako na mengine lazima yafuate mstari.
Mtu mmoja nilikuwa nikiongea naye nikiwa nimetoka Kempiski Hotel. Akasema hata wewe huwa unaingia hotel hii? Ni kamuuliza kwani kuna watu wanazuiliwa? Jibu akaniambia du hapo ni balaa soda tu ni Shs. 5,000 chakula takribani sahani shs 50,000 unawezaje kulipa pesa nyingi kiasi hicho? Hapo ni ghari sana. Nikamuuliza wapi ni rahisi? Jibu mitaani soda ni shs 700. Jibu nililompa ni kwamba haitakuja tokea huduma au vitu kuwa na bei ghari hata siku moja, ila kuna watu wanashindwa kumudu na wengine wanamudu. Tatizo sio bei bali ni watu. Siku ukibadilika hata macho yanabadilika kwani utaanza kuona viwanja kariakoo, Upanga, Masaki, Ocean view vikiuzwa Tshs. 700,000,000 na ukavinunua lakini ni wewe yule siku za nyuma ulikuwa huoni hivyo viwanja na ukaishia kujenga Kimara Bonyokwa. Badilika ndio jibu sahihi.

Maoni
Chapisha Maoni