Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Umasikini

Karibu mfuatiliaji wa Makala za kila siku zijulikanazo kwa jina la Wazo La Leo.
Tuanze kwa kutoa maana ya umasikini.
Umasikini umetafsiriwa kwa namna mbalimbali na watu tofauti. Kwa lengo la mada hii ya leo, ninaomba tubaki kwenye maana iliyotolewa na benki ya dunia:-
‘Umasikini ni pale mtu anapoishi kwa kipato kilicho chini ya $ 1.90 ambayo ni sawa na Tshs 4,370 (kwa kutumia dola moja sawa na Tshs 2,300) kwa siku. Ninachocharibu kukufikishia ni kwamba, tukichukulia familia ya kawaida kwa maana ya baba, mama na watoto wanne, hii familia inapotegemea kipato cha Tshs 4,300 kwa siku au pungufu ya kiwango hicho basi hapo kutokana tafsiri ya benki ya dunia familia hiyo ni masikini’
Mimi sijui ndugu msomaji upo katika kiwango gani cha kipato, lakini habari njema ni kwamba umasikini si jambo la kudumu labda upende. Upo msemo usemao ‘Kuzaliwa masikini si kosa lako bali kufa masikini ndio kosa lako’. Ukweli huu ni kwamba kila mtu anayo nafasi ya kubadilisha maisha.
Ili kupata uelewa zaidi juu ya maana halisi ya umasikini nakuomba ufanye mtihani ufuatao na kamwe usije rudia:-
‘Chagua eneo usilolilijua kwa maana ya kuwa hujawahi fika licha ya kujua ya kuwa ni eneo lililopo katika sura ya dunia. Eneo liwe la umbari wa kilometa 500. Pia usiwe unafahamiana na mtu awaye yeyote.
Kisha kata tiketi ya kwenda tu, huku ukiwa umeacha pesa zote nyumbani na wala usiondoke na chombo chochote cha mawasiliano.
Utaanza kidogokidogo kuelewa maana ya umasikini tangu ukiwa safarini achilia mbali utakapokuwa umefika na utakavyoanza kutaabika namna ya kurudi. ‘
Namwomba Mungu, wewe utakayefanya tendo hili, basi ikawe kichocheo cha kumbambana na umasikini kwa hali na mali.
Naamini mpaka hapo tuko pamoja katika uelewa wa umasikini.
Watu wamekuwa wakipambana kujinasua na umasikini kwa kujishughulisha na shughuli mbali mbali.
Inabidi ieleweke ya kuwa hakuna kitu humuumiza na kumnyanyasa mwanadamu kama umasikini.
Habari njema ni kwamba kila nafsi ndani yake ina mbegu iliyowekezwa yakuwezesha kuwa na maisha bora ajabu siku za usoni.
Unachotakiwa kukijua ni kwamba mbegu hiyo iliyo ndani yako kamwe haiwezi kumea na kufikia ukomavu wenye kukuletea matunda unayostahili (maisha bora) ni mpaka pale utakapoweza kuanza kutoa huduma yenye kunufaisha jamii inayokuzunguka. Hapo utakuwa umeiwekea mazingira murua kuanza kumea na kwa hakika utaona radha ya maisha ilivyo.
Ushauri wangu juu ya mapambano juu ya umasikini ni kama ifuatavyo:-
1. Inapotokea hujui cha kufanya au uchague njia ipi ya muelekeo, nakushauri baki ukitabasamu. Hii itasaidia kuipumzisha akili na kukupa mwangaza wa furaha ndani ya nafsi yako.
2. Haijawahi tokea mtu akawa kiongozi bora na makini au mtu aliyefanya makubwa duniani pasipo kujiamini yeye mwenyewe. INAWEZEKANA JIAMINI.
3. Jambo lingine muhimu kulijua ni suala la kuahirisha kufanya jambo/mambo. Hakikisha msamiati wa kuahirisha unakutoka na kamwe hauwi sehemu ya maisha yako. Ukipanga kitu lazima ukifanye lije jua au mvua.Tabia ya kusema nitafanya kesho au wiki ijayo au mwezi ujao au mwaka ujao ni tabia ambayo haijaacha mtu salama. Ni maombi yangu kirusi hichi kisiwe ndani yako.
4. ‘Tambua ya kuwa wewe ndiye mmiliki wa ramani ya maisha yako. Na kizuri Zaidi mchoraji wa hiyo ramani ni wewe mwenyewe. Wewe ni mwandishi wa maisha yako. Umeshika peni mkononi na matokeo ni uchaguzi wako wewe mwenyewe’ Lisa Nicholas
5. ‘Huduma nzuri itakusababishia uwe na mauzo ya kutosha. Iwapo utawakumbatia wateja wako, yaani ukawajali vya kutosha kushindwa kukukimbia, watakufanyia maajabu ya kukufungulia milango ambayo kamwe usingaliweza kuifungua wewe mwenyewe’ Jim Rohn
6. ;Mafanikio ni jumla ya juhudi ndogondogo ZA kila siku pasi kuachilia’ Robert Collier
7. ‘Jenga utamaduni wa kujifunza kitu kipya kila siku. Jaribu kufanya kitu tofauti. Jishawishi mpaka nafsi yako ikuelewe ya kuwa hakuna kikomo cha kufanikiwa’ Brian Tracy
8. ‘Wachache wanaojiingiza kwenye kufanya mambo yatokee wamekuwa wakionewa wivu na watazamaji ambao ndio wengi kwani kila siku ni kulalamika mara serikali hii, mara mitaji shida mara sijui nimelogwa na kadhallika huku wenzao wakiendelea wakitenda,’ Jim Rohn
9. ‘Kama watu watakusikiliza lakini pia wakakuamini, hakika watakuwa tayari kushikamana nawe kufanya biashara’ Zig Ziglar

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...