Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Umuhimu Wa Saa Moja Baada Ya Kuamka Na Saa Moja Kabla Ya Kulala

Duniani tunajifunza kila siku. Na ukikata shauri kujifunza kila siku na kufanyia kazi yale yote unayojifunza maisha yako yatakuwa yakibadilika siku baada ya siku. Unahitaji maamuzi magumu ili kubadilika.

Kama kuna jambo mojawapo muhimu unatakiwa kulijua kwa kina basi ni ile saa yako ya kwanza unapokua umeachia kitanda namaanisha asubuhi uamkapo na pia saa yako moja kabla ya kulala.

Ukiamka unakimbilia kufanya nini? Utafiti umeonesha ya kwamba wengi tumeathirika na jambo moja kukimbilia simu na kuanza kuangalia watsapp, face book, twitter, Instagram. Tunahitaji kubadili kwani si tabia njema. Saa moja ya kwanza baada ya kuamka kitandani ni ya muhimu sana kujua unaanza na kitu gani cha kwanza ila isiwe simu. Hapa ningefurahi kama kila mmoja angeliniambia akiamka tu anakimbilia kufanya nini? Najua itanichukua muda kupata mawazo mbalimbali lakini naamini kila mmoja anajua anachokimbilia mara aamkapo.

Hakuna kanuni ya kipi uanze nacho lakini kutokana na umuhimu wa saa moja ya kwanza kuwa na umuhimu sana juu ya mstakabali wa siku yako nzima basi ni vyema kuanza na chochote kati ya hivi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuianza siku ila kamwe usianze na kushika simu. Mambo machache unayotakiwa kuhakikisha unayafanya katika saa yako ya kwanza ni pamoja na:-
  1. Anza kwa kumshukuru Mungu kwa kuiona siku nyingine nzuri na jisemeshe ya kuwa unakwenda kuiishi siku kana kwamba ndio siku yako ya mwisho kuishi hapa duniani na unataka kuacha historia ya kuwa siku ya mwisho ulifanya makubwa sana na kama ungepewa siku zingine ungeushangaza ulimwengu. Jiambie ya kuwa siku ya leo utajituma sana kuhakikisha hakuna ulichopanga kitakacho bakia paipo kukifanyia kazi. Endelea kujisemesha ya kuwa wewe u bora sana na utafanya kila jambo kwa ufanisi wa hali ya juu. Fanya hivyo kila siku. Futa kwenye ubongo wako msamiati wa kuahirisha.

  1. Anza na kutahajudi. Kama kuna moja ya jambo nyeti katika maisha ya mwanadamu basi ni kutahajudi maana hapa unampa nafasi Mungu aongee na wewe. Kama utaweza kutumia saa nzima kutahajudi utaharakisha sana safari yako ya mafanikio. Maana mara baada ya kutahajudi utapata mawazo mbali mbali na hakikisha unayanakili yote kwenye kijinoti buku chako (Brain Damping note Book).

  1. Anza kwa kujisomea kitabu chenye kukupa hamasa na kukufundisha mambo yatakayokusaidia kuboresha maisha yako. Sijui u mahiri katika eneo lipi – kikubwa hakikisha unaendelea kujiongezea maarifa katika hilo eneo lako kila siku. Kikubwa katika saa yako moja baada ya kuamka usiruhusu kuangalia TV na wala usichezecheze na watoto wala paka wala mbwa. Hakikisha umejitenga wewe peke yako katika utulivu wa hali ya juu. Ukiwa unajisomea hakikisha una mahali pa kuandika mambo ujifunzayo kwenye hicho kitabu.

  1. Anza kwa kusilikiliza audio au video kutoka kwa watu mashuhuri katika mafanikio kama Bill Gates, Jim Rohn, Les Brown, Max Well na wengine wengi.

  1. Hakikisha kila siku kabla ujaianza siku lazima utokwe na jasho. Hili ni tendo muhimu sana. Tokwa jasho kabla hujaanza siku. Vitu vitakavyo kusaidia kutokwa jasho ni pamoja na kurukaruka Kamba, kukimbia angalau km 2 hakikisha hazipungui. Hichi ni kiwango mahususi. Hivyo kimbia au tembea km 1 kwenda na kurudi km 1. Endesha baiskeli. Tendo hili hata upangeje siku yako ni lalazima kulifanya. Hii itakuhakikishia kuianza yako ukiwa na nguvu za kutosha kufanya maajabu.

  1. Kunywa maji ya kawaida ila ni vizuri sana kama utaweza ya vuguvugu – kiwango cha maji ya kunywa kitategemea na uzito wako. Kanuni ni kuchukua uzito wako kwa kgs na kisha gawa kwa 24 jibu ni kiwango cha lita za maji ambazo ni lazima uzinywe asubuhi kabla ya kuswaki. Kwa nini unasisitizwa kufanya hivyo:-

  1. Kwanza unatakiwa kujua 75% ya ubongo wako ni majimaji na hivyo maji ni lazima kwa mstakabali wa ubongo wako vivyo hivyo na mwili wako umetawaliwa na maji kwa sehemu kubwa. Na kumbuka kanuni ni kunywa maji kabla ya kuswaki.

  1. Maji huamsha viungo vya ndani tayari kwa utendaji wa siku.


  1. Maji ni dawa. Magonjwa mengi yaliyokuwa yakikusumbua siku za nyuma hutayasikia tena. Anza kubadili tabia kwa kuchagua kunywa maji badala ya soda au juice za mabox. Pendelea maji. Mimi nina miaka Zaidi ya kumi sasa sinywi kabisa soda. Maji ndio chaguo bora kuliko ila radha yake si ya kukuhamasisha ila faida yake mwilini ni lukuki.

  1. Ukinywa mfululizo baada ya siku 30 utashangaa hata ngozi yako itakavyoanza kuwa nyororo.


  1. Itakusaidia kusafisha figo. Ukikojoa angalia mkojo mwako – hakikisha kila siku ni mweupe. Usiruhusu kuwa wa rangi unajiumiza.
Tuna madaktari humu kwenye grupu wanaweza changia umuhimu wa maji mwilini. Haipendezi kunywa maji ati kwa kua una kiu. Hiyo ni ishara mbaya ya kuwa mwili umekaukiwa kiasi cha kukuamuru unywe maji. Ni sawa na mmiliki wa gari kuamua kuweka maji kwenye rejeta pale litakapoanza kuchemka utaishia kuathiri gari. Dereva mzuri pamoja na mambo mengine ni lazima ajihakikishie maji kwenye rejeta.

  1. Jizoeshe kufikiria na kujenga taswira ya maisha unayoyataka. Kwani mawazo yanayotawala kwenye ubongo hugeuka na kuwa sumaku ya kuvivuta uwazavyo. Tafuta video ya THE SECRET uiangalie.

  1. Saa yako moja ya kwenda kulala hakikisha unaitumia kupitia malengo yako kama unapicha za malengo yako tafadhali pitia hizo picha zote. Kumbuka akili hufanya kazi kwa haraka kupitia picha. Hebu kuwa na album ya malengo yako.

  1. Tumia saa yako moja kwa kufikiri. Jiachilie na anza ziara na ubongo wako ukiwa umetulizana au anza kufikiria suluhisho la tatizo linalokusumbua na utashangazwa na ubongo wako utakavyokupa namna mbalimbali za kutatua. Orodhesha hadi zifike ishirini na anza kuzitumia, ya kwanza isipofanya kazi nenda ya pili na ya tatu naamini hata kabla ya kufika ya 10 utakuwa umepata suluhu.

Nikuombe kitu kimoja. Idhibiti simu yako. Ikibidi wakati wa kufanya jambo linalokuhitaji utulivu na kuzingatia zima kabisa mpaka utakapomaliza ndio uwashe. Acha visingizio ati nikizima nitakosa taarifa mbalimbali. Hivi hizo taarifa zimekufikisha wapi?

Nisikuchoshe najua ili kufanikisha haya nikuelezayo huna budi kuwahi kulala na kuamka mapema yaani kabla ya saa 11 asubuhi uwe nje ya kitanda. Mwanzoni anza na alamu na baada ya siku 21 hutahitaji alamu tena kwani ubongo wa ndani utakuwa umekuelewa ya nini unahitaji na utaendelea kukutimizia. Huchukua siku 21 kuiandikisha tabia mpya.
Si kazi rahisi kwa kuwa ubongo umetengezwa katika mazingira ya kutuhurumia, hivyo kubadilika ni mpaka wewe mwenyewe uwe umejua umuhimu. Utaanza kwa kujilazimisha mpaka ubongo utakubali kukubadilishia tabia. Wengi huanza kwa hamasa siku tatu za mwanzo na kisha huacha.
Hakuna mwaka mpya kwa kuwa wewe ni yule yule na utabaki kufanya maigizo tu ati mwaka huu nitafanya hichi na hichi ila ni mihemko tu. Si jambo dogo la mwaka mpya na mambo mampya. Mwaka mpya utaleta umaana iwapo tu wewe utakuwa mpya kuliko mwaka jana. LAZIMA UBADILI UNAVYOCHUKULIA NA KUFANYA MAMBO. MADILIKO NI MUHIMU MAANA NDIO YATAKAYOLETA MATOKEO MAPYA NA SI MWAKA MPYA. MWAKA UKUKUTE UMEBADILIKA SANA. HAPO LAZIMA KITAELEWEKA.

Maoni

  1. Nimeipenda hii makala coz inaelimisha thank u

    JibuFuta
  2. Yaliyosemwa yote ni hakika na ni muhimu kubadilika, kwa kweli nimehamasika sana hivyo naifuta Kiangazi yangu na kuandika masika.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...