Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Ushauri wa bure

Naamini kwa rehema za Bwana sote tu wazima. Leo ninakuja na ujumbe juu ya ushauri wa bure:
1. Katika maisha hakikisha unajiwekea msimamo ya kuwa unapofanya shughuli yoyote Ile hulegezi mikono lakini pia unaifanya kwa kiwango cha juu/ubora (make commitment to your excellence).
2. Ishi maisha yenye ujasiri kwani tunakabiliwa na maadui wakuu wawili ambao wamekuwa wakitushika na kutuvuta. Maadui Hawa ni hofu ya kushindwa na hofu ya kukataliwa. Jenga tabia ya kujisemesha ya kuwa unaweza kufanya.... Kamwe usiruhusu hofu kukushida.
3.Kujitoa (commitment) - Naona vyema nikatoa mfano ili kuweza mjua mtu mwenye tabia ya kujitoa. Tumchukulie mtu anayefanya kazi ya kuuza vyombo vya nyumbani ain't mauzo ya chochote like. Mtu WA Hindi hii ana kazi kubwa ya kufanya kazi yake akiwa na hamasa na tabasam mubashara. Hapo ni lazima auze kwani ameonyesha kujitoa kweli kweli na cha ajabu ni kwamba kwa kila mtu afanye biashara ya kuuza kuna siri nzito imejificha kwenye hamasa na tabasam mubashara kwani wateja huambukizwa na kuishia kukuunga mkono kwa kununua. Kama ulikuwa hulijui hilo hebu jaribu.
4. Ishi maisha ya kupenda kusaidia watu wasio na uwezo wa kukulipa. Hapa utaishi uhalisia wako. Acha maigizo ya kusaidia watu ati mmekuwa mkipigana tafu. Naomba nisieleweke vibaya - Ninachomaanisha kusaidiana ni vizuri lakini kusaidia mtu ambaye kutokana na hali yake uwezekano wa kukulipa haupo kabisa. Ukifanya hivyo ni vizuri zaidi.
5. Maandalizi - Hichi ni kielelezo kinachotofautisha weledi wa mtu mmoja na mwingine. Kimsingi chochote kitakachokuhitaji kukifanya, maandalizi ni muhimu sana. Kama kuna mwalimu anasoma ujumbe huu atakubaliana nami juu ya usemi usemao "PASIPO MAANDALIZI NI UDANGANYIFU". (NO PREPATATION THEN IT MEANS YOU INTEND TO CHEAT). Yaani usipojiandaa unachokwenda kufundisha watoto basi umejiandaa kuwadanganya haijalishi una ufahamu kiasi gani. waalimu wawili, mmoja hafundishi pasi kujiandaa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...