Ruka hadi kwenye maudhui makuu

uwezo/nguvu ya mawazo (Ideas)

Leo ningependa kuongelea uwezo/nguvu ya mawazo (Ideas) ambayo kamwe huwezi kuyaweka kwenye mizania na ukasema hakika wazo au mawazo ya leo yana thamani sana au hata kumshukuru Mungu kwa namna uwazavyo na kupata mawazo/wazo murua kwa kuchukua hatua na kwa walio wengi maisha yamebadilika kwa kufanyia kazi mawazo (Ideas) ambazo kimsingi zimetoka ndani yao.
Kitu ambacho ninaweza kukiwekea mkazo ni uwezo wa kutambua uwepo wa mawazo (Ideas) na ukawa katika nafasi ya kuelezea wazo/mawazo yako na ukaeleweka na anayekusikiliza. Yawezekana naongea na mtu ambaye hata namna ya kupakua hayo mawazo hajui.
Naomba niongelee kidogo eneo hili. Kimsingi kila mtu anatakiwa awe na note book (Brain damping note book) angalau ya kutosha kuingia mfuko wa shati kwa ajili ya urahisi wa kubeba.
Najua unamaswali ya kuniuliza: Je hichi kijinotibook kinatumikaje?
Kimsingi upatapo wazo mara moja liandike kwenye hicho kijitabu kwani usipofanya hivyo mawazo hupotea na huwa ngumu kukumbuka. Yaani mwacheni Mungu aitwe Mungu.
Watu wote wanaojua umuhimu wa wazo/mawazo hutengeneza mazingira mazuri ya kupakuwa mawazo.
Sehemu tulivu ni murua kupakua mawazo (Ideas). Unaweza kukaa kwenye eneo tulivu simu ikiwa imezimwa, wala hakuna TV au paka au mbwa. Hakikisha ni eneo halina mwingiliano wa makelele. Tulia angalau nusu saa bila kufanya chochote. Akili ikianza kukuzungusha kwa kukuletea wazo hili na lile jitahidi kuirudisha. Kimsingi uwe kana kwamba umeisimamisha akili ipumzike. Kitendo hichi huitwa kutahajudi (meditation). Mara nyingi katikati ya utulivu au mara baada ya utulivu utaanza kupata mawazo yakikujia na hapo usifanye kosa anza kuandika kila wazo likujialo kwenye kinote book chako.
Kutokana na umuhimu wa mawazo (Ideas) watu wengi hutenga siku moja katika wiki au kila baada ya wiki mbili au kila baada ya mwezi mmoja kutegemeana na ratiba za utafutaji. Siku hiyo unakuwa hupatikani kwenye simu na wala huwi karibu na tv wala paka au mbwa. Kama hunielewi naomba nitafute kwa simu au tuonane nikuelezee kinaga ubaga.
Ushauri wangu pata muda asubuhi sana yaani kabla ya saa kumi na moja na jioni unapojiandaa kulala pata tena muda wa kutahajudi na kupakua mawazo ipasavyo. Jenga hii tabia. Ziko njia mbalimbali za kutahajudi. Muda haunitoshi kudadavua hapa. Ila kuwa huru kuwasiliana nami maana nitachukulia ni hitaji binafsi na nitakuhudumia pasi malipo yoyote.
Ninacho kijua kwa uhakika ni kwamba utajiri aupatao mtu na kuweza kuwa na fedha lukuki nikimaanisha kuanzia Tshs. 2,300,000,000,000 na kuendelea zinakuwa zimetokana na mawazo/Ideas ambazo pasi kujiuliza uliza wakazifanyia kazi.
Kumbuka liko wazo ndani yako ambalo siku ukilifanyia kazi maisha yako yatabaki simulizi. Ila kuna mambo machache unatakiwa kujifunza ili uwe bora Zaidi.
Mimi siku mhizi nimeongeza umakini wa kupakuwa mawazo yangu na nimejitenga na vitu vingi ili kurahisisha upakuaji wa mawazo. Siiangalii TV labda kwa bahati mbaya, Sisomi magazeti kwa maana haya ya kila siku yenye matukio mbalimbali. Nilikuwa shabiki sana wa mpira na sikuwa nikipenda kupitwa na mechi lakini sasa sitaki kabisa mpira. Ushabiki wa mambo ya siasa nimeacha. Si jambo rahisi lakini inabidi kufanya maamuzi magumu ili kufupisha safari ya mafanikio.
Ninachokijua mimi ni kwamba kila mwanadamu unayemuona ana mambo makuu mawili
a. Uwezo wa ajabu wa kufanikisha maisha yake hata kumzidi Billgate, Dangote, Donald Trump, Bakhresa na endelea kuorodhesha. Hilo nina uhakika 100%. Acha kulalama mwachilie jemedari wako aliyelala ndani yako. Akiamka hapatoshi.
b. Hakuna hata mwanadamu mmoja duniani aliyeweza kuutumia uwezo wake wote alionao hata huyo Bill Gate au Dangote na wengine wengi bado. Mwanadamu kwa asili ana uwezo wa ajabu mno. Masikitiko yangu wengi wamekufa pasi kuenjoi hata robo ya mafanikio waliyo nayo. Mungu atusaidie.
Sasa hivi mimi sitaki virusi kuambukizwa. Ninachagua watu chanya tu. Nikikugundua wewe maongezi yako ni kulalamika kila wakati na kuniambia vimisemo vyako mfano wa mbili havai moja, mara ng’ombe wa masikini hazai mara aliyekupa wewe ndiye aliyeninyima mimi basi hapo sina budi kufuta namba yako na kukutenga kabisa nami na urafiki unaisha.
Mara nyingi watu masikini wana tabia kama nilizoeleza hapo juu. Mimi niko radhi kuutumia muda wangu na mataji wa kimawazo wanaojitambua na safari wameanza. Hao twaweza kutana mahali kwa kahawa tukabadilishana mawazo.
Niko mbioni kuwa na kijiwe cha jinsi hiyo cha kuweza kukutana na matajiri kwa ratiba maalumu na wenzangu tulio kwenye foleni ya kuelekea kileleni ili kuambukizana mawazo mbalimbali maana huo ndio utajiri (Mawazo (Ideas)).
Naomba ifike mahali tusiendelee kufanya kazi ili kupata pesa bali pesa zitufanyie kazi sisi na kama utafanya kazi ni kwa vile unapenda lakini si ili upate fedha maana fedha zitakuwa zikitiririka bila kujali unafanya kazi au hufanyi. Maana utakuwa na hisa kwenye makampuni mbali mbali, majengo ya kukodisha, na uwekezaji mbalimbali.
Pesa ni moja kati ya nguvu alizo nazo mwenye kuzimiliki. Ndio maana tajiri akiongea upuuzi basi unachukuliwa ni hekima na masikini akiongea hekima huchuliwa ni upuuzi. Mwenye kuelewa na aelewe hili kwa uzuri.
Hivyo ukitaka kufa masikini endelea kufanyia kazi pesa utachakaa na tutakuzika karibuni, ila kama unataka kuwa tajiri inabidi pesa zianze kukufanyia kazi na sio wewe kufanya kazi ili kupata pesa. Nakubaliana kufanya kazi ili kupata pesa kwa kitambo lakini lengo liwe kufikia pesa kukufanyia kazi na ukifanya kazi iwe ni kwa kupenda (Hobby).
Hivyo kwa kumalizia nasema kilicho na nguvu sana ni Elimu juu ya fedha ambayo wengi ni watupu. Ni kweli pesa humpa mtu nguvu, lakini elimu juu ya pesa ni Zaidi ya pesa kwani pesa huja na kutoweka. Lakini ukiwa na elimu sahihi ya pesa hata zikiondoka zitarudi maana uko vizuri kichwani kielimu juu ya fedha.
Kumbuka elimu juu ya fedha hukupa uwezo juu ya fedha na unaweza kuanzia popote kuzitengeneza siyo kwa kuchapisha bali kuitumia elimu uliyonayo ikuwezeshayo kufikia hatua ya fedha kukufanyia kazi na sio wewe kufanya kazi kwa ajili ya pesa.
Nimalizie tu kwa kusema kuwa chanya pekee hakumaanishi kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha bali kuwa chanya na elimu juu ya fedha ndio jibu sawia. Hii inajibu swali kwanini wasomi wengi hawafanikiwi? Jibu ni kwamba ufahamu wao umelishwa elimu ya kufanyia kazi fedha na hivyo kushinda kubadilisha kazi kila kukicha ati anatafuta penye majani mabichi (Green Pastures). TUNAHITAJI ELIMU JUU YA FEDHA.
Nisikuchoshe. Kama unafaidika na mfululizo wa Makala hizi zijulikanazo kama Wazo La Leo, basi usisite kuwasiliana nami ili ujiunge na wenzako waliostuka na kuanza kujifunza vitu nyeti kwa pamoja kupitia group la WatsApp lijulikanalo kama KARAKANA YA UBONGO.
Kumbuka ni lazima ufanyiwe udahili ili kuona kama unakidhi viwango vya kujiunga kwani tunajitahidi kujitenga na wenye virusi wasije ambukiza wengine kwenye kundi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...