Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Uzalishaji

Karibu mfuatiliaji wa Makala sijulikanazo kama wazo la leo. Leo nimeonelea vyema niongelee juu ya nafasi yako katika uzalishaji, iwe umeajiliwa au unajishughulisha na shughuli binafsi – huna budi kujiweka katika nafasi itakayokufanya uwe mtu wa thamani katika uzalishaji na kwa uhakika utashangaa uzalishaji wako ukipanda kwa kasi maana utasaidika iwapo utafuata ushauri ambao ninakwenda kuuachilia kwako.
Kimsingi hakuna mwanadamu anayehitaji kuishi maisha yasiyokuwa na maana. Wengi wetu tunaishi pasipo kuwa na mwalimu/mentor/coach katika maisha. Naomba nikutangazie kuishi kwa namna hiyo kutakucheleweshea mafanikio yako. Ushauri wangu kwako chukua hatua haraka za kumtafuta mtu atakaye kuwa anakuongoza katika maisha. Amini usiamini ukichukua hatua utajionea mwenyewe maisha yako yanavyoanza kuboreka. Sijui naongea na mtu wa jinsi gani, lakini kwangu umri ni namba tu, vinginevyo hauna maana yoyote kimaisha kwani waweza badilisha maisha yako katika kipindi chochote.
Jambo ninalotaka kusisitiza ni kuwa uwe na sifa za kufundishika, acha kiburi kinachokuangamiza.
Sasa wengi mtaniuliza:- Mwalimu ni nani? Jibu ni yule mtu unayemkubali katika ujumla wa maisha yake kiasi kwamba unatamani uwe kama yeye. Ninachosisitiza hapa ni kwamba mwalimu/coach/mentor ni hitaji la muhimu sana kwa kila mwanadamu. Sina lugha ya kukueleza ukanielewa lakini huo ndio ushauri wangu kwako. Hata mimi unionavyo kufikia hatua hii niliyonayo ya kuweza kuwa mwalimu/mentor/coach kiasi cha kukubalika na watu wapatao 24 kwa sasa ni kwa kuwa ninaye mwalimu/coach/mentor wangu anayejulikana kwa jina la DR. AMANI MAKIRITA. Mungu amzidishe kila la heri katika maisha yake na familia. Amenitoa mbali na sioni pesa ya kumlipa nikatimiliza alichonifanyia katika maisha yangu. Kama ansoma Makala haya naomba apokee shukrani zangu za dhati.
Ngoja nikupe ufahamu kidogo uweze kujua umuhimu wa mwalimu katika maisha. Hadi niandikapo ujumbe huu ana watu wapatao 254 na mimi ni miongoni mwa hiyo idadi. Najua umeanza kuwaza ya kwamba anatumudu vipi? Ashukuriwe Mungu aliyetuletea teknologia ya wattsAp, wakati wengine wanaambukizana virusi vya selfie wengine hiyohiyo watssAp inatubadilishia maisha. Mwalimu wangu mpendwa katika kila siku iendayo kwa Mungu anatugawia maarifa adimu ambayo hata darasani huwezi kupata na ndio elimu ya msingi ili kuweza kuishi ukifurahia maisha. Elimu hii inaitwa elimu isiyo rasmi, yaani hakuna shule au chuo kinafundisha. Hii ndiyo inakufanya uwe tofauti na Bill Gate, Dangote, Mengi, Bakhresa, Manji, nisaidie kuendeleza orodha. Watu hawa karibia 97% hawana degree wala udaktari. Lakini ndio madaktari wa maisha. Wakati wewe unajivunia elimu na mbwembwe kibao ati umesoma sana huwezi uza karanga au maandazi, wenzako wenye elimu isiyo rasmi wanakusanya pesa kama mchanga. Unabaki kusema nimelogwa mimi, sina bahati, kweli wa mbili havai moja na misemo kadha wa kadha ukijihalilishia hali uliyonayo.
Naomba unielewe vizuri. Siidharau elimu hata kidogo. Mimi mwenyewe nimesoma kwa kiwango change name najiita msomi. Lakini nikuambie kitu kimoja – Msomi akibahatika kupata elimu isiyo rasmi na kuondokana na kiburi cha kujiona bora kwa ajili ya vyeti vyake vya darasani na ufaulu uliotukuka na kuishia hapo hapo pasi kuisakanya elimu isiyo rasmi - basi iko shida. Kimsingi ELIMU YA DARASANI + ELIMU ISIYO RASMI = MAISHA YENYE MAANA. Mwenye ufahamu na atambue hayo mahesabu. Mwanafunzi wangu Mariamu Manjole sidhani kama atakumbukwa kufundishwa name hiyo hesabu darasani kwani hata mimi nimeifahamu baadae sana.
Sasa naomba rudisha mawazo yako juu ya elimu isiyo rasmi juu ya kuwa na mwalimu/coach/mentor na matumizi ya WatsApp – Utajiuliza mbona watu 254 ni wengi inakuwaje mwalimu Dr. AMANI MAKIRITA KUWAMUDU? Jibu - Kinachofanyika ni kwamba sote katuingiza katika kundi moja la wattsAp lijulikanalo kwa jina la KISIMA CHA MAARIFA. Huko anatulisha hadi kutuzalisha sie akina Mwakitalu yaani katuibua kusikojulikana. Ninajivunia kuwa na Dr. AMANI MAKIRITA katika maisha yangu. Sijutii kukutana naye kimaisha. Narudia tena Mungu amzidishie mwalimu wangu.
Najua una maswali mengi juu ya hili kwa kuwa utaratibu wa kuwa na mwalimu /coach/mentor kwetu tulio wengi ni utamaduni wa kigeni lakini kwa wenzetu wa ulimwengu wa kwanza ni jambo la kawaida na ndio maana hali ya uchumi wao kwa walio wengi imeboreka sana ukilinganisha na sisi tusio na huo utamaduni. Mungu atusaidie maana twafa. Mwenye sikio na asikie maneno haya niyanenayo.
Naomba niishie hapa na endelea kunifuatilia kila siku nikikuletea Makala iitwayo wazo la leo.
Ni mimi mwalimu/coach/mentor wako ninayependa kuona unabadilika huko huko uliko nami ukinilipa mshahara wangu ambao ni shukrani utakazo kuwa ukizitoa kwa Mwenyezi Mungu ukisema hujutii kukutana nami kwenye mitandao ya kijamii maana wengi naamini hatufahamini japo mu wanafunzi wangu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...