Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wazo La Leo

Ninamshukuru sana Mungu kuiona siku ya leo. Leo napenda kuzungumzia juu ya nguvu ya hamasa.
Naliongelea hili ili kila mtu aone jinsi anavyoweza kujiwezesha kuwa katika hisia chanya.
Kimsingi napenda kila mmoja ajue ukweli kwamba katika kila hali kuna chaguzi tunafanya.
Kitendo hichi cha kufanya uchaguzi ni takribani cha kila siku au kwa lugha nyingine ndio maisha yetu ya kila siku lazima ufanye chaguzi.
Ili kuweza kupata uelewa vizuri wa kujiwezesha kuwa na hisia chanya naomba nikupitishe katika vipengele vifuatavyo:-
Hofu - wakati wowote tunapokuwa watu wa kushughulikia hali iliyotufanya tupoteze amani au furaha tuliyokuwa nayo matokeo yake tunajawa na hofu ya kupata maumivu zaidi. Maumivu haya kamwe sio halisia bali ni onyo ya kuwa kama mambo hayatobadilika, basi hali iliyo mbele yetu itakuwa mbaya zaidi.
Hili lawezea kukutokea katika maisha. Mfano unapofukuzwa kazi ghafla, huingiwa na hofu ya maisha kuwa chini ya kiwango ulichokuwa ukiishi kwa sababu ya uhakika wa mshahara na marupurupu. Hivyo iwapo aliyeguswa na hili hatoamini ya kuwa maisha yatakuwa mazuri baadae, basi ataanza kuandamwa na mambo yafuatayo:-
Maumivu: Kuanza kupoteza matumaini ya mambo ambayo amekuwa akiyategemea kuwa nayo kama umiliki wa nyumba, kusomesha watoto shule bora, mavazi mazuri, Lishe nzuri nk.
Matumaini ya kuwa na furaha hutoweka na Maumivu kuzaliwa. Hili ni dhahiri tunapoanza kuhisi kuondokewa na mapenzi, furaha au faraja iliyokuwepo kwa kuwa kazini basi uwepo na maumivu moyoni huzaliwa.
Hili huwapata wengi mfano watu wanapofikia hatua ya kuvunja uchumba, mtu anapoishiwa fedha au anapojikuta ananenepeana na kupoteza umbile zuri.
Hasira - Tunapokuwa tumeumizwa tunaanza kuwa na machungu na watu ambao wamekuwa wakichangia tujisikie kupendwa, kuwa na furaha na Faraja katika maisha.
Kuchanganyikiwa - kule kujua ya kuwa ungelikuwa na maisha mazuri kunakufikirisha ya kuwa hutoweza kurudia hali ya matumaini uliyokuwa nayo mwanzo na kuona sasa maisha yamepoteza radha au umaana. Matokeo yake tunaanza kuchukua hatua za kujinasua: kujisomea vitabu tunavyotegemea vitatusaidia, wengine huamua kurudi shule, kuhudhuria semina mbalimbali. Tunapokuwa tukiendelea kujifunza, tunaanza kujiamini, tunapata Tumaini, na hamasa tena na kuanza kupata matarajio ya kufanikiwa katika maisha yetu. Lakini tunapoanza tena kuingia kwenye misukosuko ya kimaisha kwa mambo yetu kutokwenda vizuri huishia kukata tamaa na kuanza kujikutaa katika hali ya...
Kupoteza mategemeo - unapokata tamaa kuendelea kufanyia kazi malengo yako, matokeo yake ni kupoteza kabisa mategemeo uliyokuwa umeyajenga. Hapa ndio mwanzo wa mtiririko wa Maumivu. Hatimaye kupoteza mategemeo kunazaa...
Kujisikia vibaya moyoni: Hii ni hatari ambayo husababisha mtu kuwaza kujizuru. Unatambua ya kuwa unahitaji kubadilika, lakini unajikuta huhitaji tena kujaribu. Kila Mara unaishiwa nguvu kujaribu tena, unabaki kujisikia vibaya moyoni. Ni mpaka pale utakapopata ujasiri tena wa kujaribu tena, vinginevyo utajisikia...
Kutojitosheleza - Umepoteza tumaini. Unaanza kujiona huna thamani tena. Hujiamini tena ya kuwa una uwezo wa kubadili maisha yako tena. Unajihisi kupungukiwa fedha, afya, kazi/fani, hali ya kiroho, mahusiano na maisha kwa ujumla na wanaokuzunguka unaona kana kwamba wamekutenga.
Hapa ndipo linakuja suala la kutafuta msaada kutoka kwa mtu anayeweza kukusaidia kuanza kujiamini tena, Vinginevyo usipopata mtu wa jinsi hiyo utaelekea hatua ya...
Mkandamizo wa mawazo: Katika hatua hii utakuwa umeelemewa na Maumivu moyoni. Hapa wengi huishia kuwa mateja wa dawa za kulevya na maisha kuwa ya hovyo kupindukia.
Msaada waweza patikana kwa majirani na pia kumgeukia Mungu.
Nimalizie kwa kusema kuwa iwapo wewe na mimi tunayapenda maisha ni LAZIMA TUAMINI HAJALISHI TUNA HALI MBAYA KIASI GANI MAISHA YATABADILIKA NA KUWA BORA ZAIDI YA AWALI. NI KWELI WAWEZA KOSA CHAKULA KWA MIEZI KADHAA. KUMBUKA JAMBO MOJA TU YA KUWA SHIDA ULIYONAYO NI YA KITAMBO KAMWE HAIWEZI DUMU MILELE.
Ni mimi mwalimu wako/coach Seth Simon Mwakitalu 0754 441325/0788493836/0714051174.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...