Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Aina 6 za mikakati ya kukijengea kujiamini

Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kutupa siku nyingine yaani tarehe 1 Disemba, 2017. Tarehe hii ni mwanzo wa mwisho wa mwezi katika mwaka. Ninampa sifa na utukufu Muumba kwa kutulinda hadi kufikia siku ya leo.
Ninazidi kumuomba Mungu azidi kunijalia pumzi nizidi kutenda kusudio la mimi kuwepo hapa duniani. Ni matamanio yangu ya kuwa nikifa niwe nimetoa kila kitu alichokiweka ndani yangu na hivyo kuacha alama kama kumbukumbu ya kuwepo kwangu. Sifa na utukufu namwachia Yeye aliye juu.
Leo tunakwenda kujifunza mikakati sita ya kujijengea kujiamini. Naokuomba fuatana nami katika safari hii nikianza kudadavua moja baada ya nyingine:-
1. Kila siku jijengee tabia ya kujikumbusha yote uliyoyafanya kwa uzuri
a. Mkazo ubaki katika kile ulichofanikisha kukikamilisha haijalishi ni kikubwa au kidogo kiasi gani - Kamwe usifanye kosa la kupuuzia kitendo hichi.
b. Tumia utaratibu ufuatao kukujengea tabia maridhawa kila siku
i. Kupangilia mambo ya kufanya siku inayofuata. Tendo hili ni vyema ukalifanya kabla ya kulala kwani itasaidia ubongo wa ndani (subconscious mind) kunasa na ukiwa umelala mipango yako ikawa inafanyiwa mchakato na ukiamka tu ni suala la kufuatilia vile ulivyopanga kutekeleza. Ushauri wangu mipango mkakati izingatie vipaumbele mfano ahadi ulizoweka za kukutana na watu, miradi unayotazamia kuifanya na kadhalika. Hivyo kila siku usiku au asubuhi ya siku inayofuata jijengee tabia ya kutathimini jana yako au kutwa yako kutokana na mipango mikakati yako.
ii. Kuchukua hatua ya kutenda – Fanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vyako ambavyo vitakusogeza kukamilisha malengo yako sema labda umejipangia malengo ya siku sitini basi kila kinachochangia kukusogeza kwenye hayo malengo kipe kipaumbele.
iii. Kujifunza –Jenga tabia kila siku kutanua uelewa wako kupitia kujisomea, kusikiliza cassete za mafundisho, videos, mwalimu wako wa maisha – mentor (kitu hichi ni kigeni sana kwetu watanzania, kwani unaona mtu anaishi pasi kuwa na mtu anayemwongoza katika maisha. Kimsingi huna budi kumchagua mtu ambaye unatamani kuwa kama yeye ili awe ndiye mwalimu wako. Hili ni muhimu sana, nakuomba usipuuzie na kuhudhuria mafunzo mbalimbali hata ikibidi kulipia fanya hivyo.
iv. Kupumzika (Relaxation) – Ondoa msongo wa mawazo wa kila siku. Tahajudi (Meditate), sikiliza muziki na pata muda na familia huku ukiwa umezima simu kabisa.
v. Fikiri – Pata muda wa kuitafakari siku yako ilivyokuwa. Pitia malengo yako na jaribu kuyatengenezea picha kwenye ubongo kana kwamba sasa unamiliki, pata mawazo mapya (develop new ideas), tumia noti buku yako kuyanukuu.
2. Jifundishe wewe mwenyewe, kama ambavyo ungelimsaidia mtu mwingine kuondokana na changamoto, basi jifanyie vivyo hivyo mwenyewe.
3. Jisomee kutoka kwa watu waliokutangulia wenye kukufanya ujisikie u bora kuliko ulivyokuwa ukijifikiria (Read Inspiring biographies and autobiographies).
a. Maisha yasiyo na changamoto ni udanganyifu na sijui utayapata wapi.
b. Tambua na kubali ya kuwa katika maisha utakutana na kupanda na kushukuka. Hayo ndio maisha halisia na si vinginevyo. Kila mtu hupitia hakuna asiyepitia kupanda na kushuka. Hiyo ndio tfsiri sahihi ya maisha.
c. Kujiamini kwako hukua pale tu unapokabiliana na changamoto za kimaisha na sio kuzipa mgongo. Haimanishi utaweza kuzishinda changamoto zote lakini kikubwa ni mtazamo wako sahihi utakufanya upate ushindi katika changamoto lukuki kuliko
d. Kuwa mtu wa shukrani
4. Jijengee wigo mzuri wa kusaidiana. Ishi vizuri na watu. Wafanyie watu yale yote ungependa wewe kufanyiwa. Jenga mahusiano mazuri na watu na mengine mengi. Kifupi kuwa mtu wa watu. Acha majivuno hata kama umefanikiwa kiasi gani. Jishushe. Kumbuka wahenga walisema aliye juu mngoje chini. Naomba hili lisiwe kwako.
5. Jisukume kuhakikisha malengo yako ya muda mfupi unakamilisha.
a. Hakuna njia rahisi na ya muhimu kujijengea kujiamini kama kuhakikisha unakamilisha yale uliyojisemea utafanya.
b. Unahitaji kupoteza kitu fulani kabla ya kupata ushindi. Huwezi kuwa mkimbiaji mzuri ukiwa na kitambi. Ni lazima upoteze kitambi ndipo ushinde mbio. Huwezi kuwa mtu chanya mpaka upoteze marafiki hasi na kadhalika.
6. Jifanyie kitu kwa ajili yako kila wiki
- Tafuta namna ya kusherehekea yale uliyoyafanikisha katika wiki husika. Unadhani hustahili? Kama ni ‘HAPANA’ anza tena na hatua ya kwanza hapo juu hadi ufikie hatua ya sita. Lakini kama unastahili, tafadhali jifanye kitu cha kujipongeza.
Kumbuka safari ya kujijengea kujiamini inaanzia na ushindi upatikanao katika kila wiki. Jifunze kujipongeza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...