Maisha yanahitaji kujipanga. Acha kuishi kihasara.
Wengi wetu hujishughulisha sana na vitu vingi visivyo na tija na kutusababishia uchovu na kwa kuwa havina matokeo makubwa shida nyingine huzaliwa uhitaji wa pesa, msongo wa mawazo, mahusiano kuharibika, hujihisi hufai na kwa wenye Imani ndogo huishia kusema ukoo wetu una nuksi au nyota yangu imeibiwa.
Leo napenda kwanza ujue ukweli huu Kanuni ya Pareto inasema asilimia 20 ya vitu tufanyavyo vina uwezo wa kutupa matokeo ya asilimia 80 na kwa upande mwingine asilimia 80 ya mambo tufanyayo hutuletea matokeo ya asilimia 20.
Wengi wetu huishia kujishughulisha na vitu ambavyo ni asilimia 80 na tunapata matokeo asilimia 20. Mungu atusaidie tupange kufanya vitu vichache vyenye matokeo makubwa na tufurahie maisha.
Tabia hii ya kufanya mambo mengi yasiyo na tija na kutufanya kila siku tuko hoi imesababisha ndoa nyingi ziyumbe maana wengi wameishia kulala mzungu wa nne na wengine wamegawana vyumba. Hii ni hatari. TUBADILIKE>
Hapa ndipo huja suala la umuhimu wa kuimaliza siku kabla hujaianza.
Hakikisha huendi kitandani mpaka umepanga mambo ya kufanya siku inayofuata. Kitendo hichi kina faida kubwa sana ambayo wengi hawaifahamu.
Kimsingi unapopanga mambo ya kufanya siku inayofuata kwa lugha nyingine unahusisha ubongo wa ndani (subconscious mind).
Hivyo unapoenda kulala ubongo wako wa ndani (Subconsious Mind) huanza kufanyia kazi yale yote uliyoyapanga usiku maana yenyewe ipo kazini masaa 24. Utashangazwa jinsi mambo yako mengi yatakavyokuwa yamerahisishwa na kuifanya siku yako iwe na matokeo makubwa.
Jambo lingine la kuzingatia wakati wa kupanga รข€“ tengeneza utaratibu pia wa kujizawadia. Mfano wewe unafanya kazi ya mauzo na umepanga kuwapigia simu wateja watano kuwataarifu juu ya mali mpya zilizowasili.
Ukianza tu kupiga simu ya kwanza na mara umalizapo jizawadie sema kwa kunywa kahawa au chai mara moja tu yaani mnyonyo mmoja na sio kumaliza kikombe (One sip only). Na ukipiga tena simu ya pili unakunywa tena mara moja tu, vivyo hivyo mpaka unamaliza.
Hamasa itakuwa ikiongezeka ya kupiga simu nyingine ili upate kunywa tena. Maisha yanakuwa na radha nzuri na wakati huo huo unaendelea kuzalisha.
Mifano ipo mingi tuseme unasema nikimaliza repoti hii kabla ya saa tatu nitatoka nje kupunga upepo dakika tano. Hivyo ubongo wako utahakikisha unashughulika ndani ya muda uliopanga ili upate tano bora.
Kupanga kwa kujiwekea ukomo wa kumaliza shughuli Fulani una maana kubwa sana na siku zote usipende kuweka ukomo mrefu. Jitahidi kujibana ili kukamilisha unamaliza ndani ya wakati na hivyo utakuwa ukifanya mambo mengi kwa siku kuliko ulivyokuwa ukiishi pasi utaratibu wa kujipangia.

Maoni
Chapisha Maoni