Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jifunze Kanuni/Sheria za Maisha Yalivyo

Tupo duniani tunaishi lakini sijui kama unajua ya kuwa tunaongozwa na kanuni au sheria ambazo kamwe huwezi zibadili. Hivyo ni vyema ukazijua kidogokidogo ili uweze jua jinsi ya kuendana nazo.
Utakapotenga muda wako kujifunza sheria za dunia hii utasaidika na mambo makubwa mawili:-
  1. Utajilinda na kuumizwa – Kikubwa hapa si kutozipenda sheria za dunia bali muhimu sana ni kupata taarifa za kutosha kuzijua hizo kanuni. Kwa kufanya hivyo utalijilinda na kuumizwa maana ikitokea hivi wajua hii ni kanuni lazima iwe hivi. Lakini ungalikuwa hujui ungeumizwa. Hakuna kitu kibaya kama mtu kuwa mjinga. Lakini upande mwingine ujinga huo ukikupelekea kuwa kapuku inakuwa mbaya Zaidi. Ila utapoteza kabisa maana ya wewe kuishi maisha haya pale itakapotokea ujinga wako umezalisha ukapuku na kupelekea kuwa kitandani ukiwa mgonjwa. Yaani u mjinga, tena kapuku na kama haitoshi u mgonjwa wa kushindwa kuamka kitandani. Unadhani unasubiri nini. Pambana kuondoa ujinga usikufikishe mahali pa kuwa mahututi.

  1. Utakapojifunza kanuni za dunia utapata kujua mazuri ya dunia na kuyafuata. Ninachomaanisha hapa ni kuweza kujua pande nzuri za dunia na ukaelemea huko ili uweze faidi Zaidi.

Sasa leo nitaongelea kanuni mbili za dunia ambazo ni:-

  1. Sheria ya kutumia – Sheria hii inasema chochote usichotumia utakipoteza. Mfano:-
  • Usipotumia ubongo wako utapoteza uwezo wake
  • Usipotumia matakwa yako utayapoteza
  • Usipoitumia hamasa yako ya kufanya kazi utaipoteza na kamwe usijidanganye kwamba utahifadhi hamasa uje utumie siku za baadaye.
  • Usipotumia Imani yako utaipoteza
  • Usipotumia nguvu zako utazipoteza
  • Usipotumia kipaji chako utakipoteza
  • Usipotumia uwezo wako utaupoteza
  • Hata mkono wako usipoutumia utaupoteza
Naamini kanuni hii umeielewa. Hivyo kila mmoja wetu anatakiwa sasa ajiulize ni kitu gani hakitumii ambacho kipo ndani yake au kinachomzunguka. Tulizana na orodhesha na mara moja anza kutumia kabla havijapotea.

Ili kumalizia kanuni hii nimependa tujikumbushe hadithi ya Bwana aliyegawa talanta kwa watumishi wake alipoazimia kusafiri kwa muda mrefu. Bwana huyu alikuwa na watumishi watatu na hivyo wa kwanza alimpa talanta 5 na wa pili alimpa mbili na wa tatu alimpa 1. Kikubwa cha kuelewa hapa ni kwamba talanta hizi hakugawa apendavyo yeye ila aligawa kutokana na uwezo wao. Zamani talanta zililinganishwa na thamani ya almasi. Nataka uanze kutengeneza picha ya thamani ya talanta walizopewa watumishi.

Bwana akasafiri kwa muda mrefu na aliporudi aliwaita. Wa kwanza akamuuliza ziko wapi talanta zangu? Jibu hizi hapa na sasa ni 10 maana nilizifanyia kazi zikazaa mara mbili. Vivyo hivyo aliyepewa mbili akaulizwa naye akajibu hizi nne maana nilizifanyia kazi zimezalisha zingine mbili na watatu alipoulizwa alisema nakujua wewe u makini na mali zako. Hivyo nilitafuta karatasi zuri nikaviringisha talanta yako na kuifukia chini na niliposikia umerudi nimeifukua na kwa bahati nzuri hakuna aliyeiba. Pokea talanta yako kama ulivyonipa.

Ndipo Bwana alipokasirika na kumpokonya ile moja na kumkabidhi mwenye kumi.
Tunajifunza nini? Dunia iko radhi kukuzawadia mara dufu utakaposhughulika na vipaji ulivyopewa na kinyume chake utapokonywa na vitaelekezwa kwa walio tayari kuvitumia vipaji vyao na wewe unabaki tu ukisema ama kweli kuna watu wana bahati duniani. Acha ujinga siku zote bahati huwafuata wanaojituma.

  1. Kanuni ya kupanda na kuvuna – Chochote upandacho utavuna tu na kama sio leo basi kesho. Kamwe usijifanye mjanja utavuna tu.
Mambo ya kuzingatia kwenye hii kanuni:-
  1. Hasi – Ukipanda ubaya lazima utavuna ubaya. Kondakta anapokuzidishia pesa mrudishie. Ukichukua tu subiria lazima nawe pesa zako zitatoweka. Hiyo ni kanuni. Usimfanyie jambo baya mtu awaye yeyote kwani litakurudia tu. Kile usichopenda kutendewa usikitende asilani. Ukitaka kutajirika kwa kuiba nakupa pole maana pesa zote zitapotea na kubaki ukiwa hoi bini taabani. Acha ubaya tenda wema utashangaa kanuni inavokuzawadia.

  1. Chanya – Panda vitu vyema utavuna wema.


  1. Kumbuka huvuni tu kile ulichopanda bali mavuno huwa ni mengi Zaidi ya ulichopanda iwe ni hasi au chanya. Ukimwibia mtu Tshs. 5,000,000 basi tegemea katika maisha kupotelewa na fedha maradufu mpaka utaenda kwa waganga kumtafuta mchawi. Kumbe mchawi ni wewe. Jifunze kwa punje ya mahindi. Unapanda punje moja, je unavuna punje ngapi. Hii ni kanuni ya kidunia na kamwe haimuachi mtu salama lazima ikushughulikie. Ndio maana ukiwa mtoaji na kusaidia wengine kamwe hutapungukiwa ni kwa sababu ya hii kanuni. Ogopa usiwe kama bahari mfu ambayo kazi yake ni kupokea tu na wala haitoi maji kugawa kwenye mito mingine. Hata ukiwa unakula tu huendi chooni unafikiri nini matokeo. Hivyo iwe umepanda hasi au chanya mafuvuno ni maradufu.

  1. Unaweza poteza – Haijalishi umefanya hasi au chanya uwezekano wa kupoteza upo. Ni kanuni. Kama unaishi vizuri na ikatokea umepoteza usilalamike ni kanuni songa mbele kupoteza ni sehemu ya maisha.


  1. Usipopanda hutavuna – Jipange. Naomba nitumie mfano wa mtu aliyenunua TV ya shs. 900,000. Ukweli ni kwamba kuimiliki TV si gharama bali kuangalia TV ni gharama mara dufu. Kwa uwiano wa muda autumiayo mtu kwa siku kuangalia TV, utafiti unaonesha kwa wastani watu wanaomiliki TV wanatumia masaa 6 kwa siku kuangalia TV. Sasa masaa 6 ni robo ya masaa 24. Mtu huyu akifika miaka 60 kwa wastani atakuwa ametumia miaka 15 maishani kukenua mimacho kuangalia TV. Hii kimahesabu TV aliyoinunua kwa Tshs. 900,000 itakuwa inamgharimu takribani Tshs 12,000,000 kila mwaka yaani pesa ambayo angezalisha kwa kuacha kuangalia TV au saa moja tu kwa siku kama una ugonjwa wa kupenda TV. Sasa niambie kipi gharama. Kuimiliki TV au Kuangalia TV. Wewe umekaa tu na unafikia miaka 60 unaanza kulalamika ati wa mbili havai moja. Hakuna kitu kama hicho duniani. Usipopanda usitegemee mavuno. Amka, kaza mkono ingia kazini.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...