Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jinsi Gani Mtu Afanikiwe Katika Maisha

Wengi wetu huyatazama mafanikio kana kwamba ni kitu kisichowezekana kukifikia. Tunajifananisha na watu ambao jamii inawatambua ya kuwa wamefanikiwa na kamwe tunashindwa kujipima kujua kipi tufanye kuwafikia. Tunaishia kudhamiria vitu vichache kuliko uwezo tulio nao ambao wengi hawajui kwamba wana huo uwezo ambao kimsingi ni mkubwa mno kiliko tujuavyo. Lakini ukweli ni kwamba mafanikio ni rahisi sana. Na si uchawi.
Ili kuweza kufanikiwa katika maisha, unahitaji vitu vikuu viwili: kufanya kitu unachokipenda bila kujali unapata hela au hupati bali furaha yako ni kuendelea kufanya na ajabu itakayo fuata ni pesa kuanza kukufuata na jambo la pili ni unyenyekevu (Kuwa tayari kumwona mtu yeyote ni bora kuliko wewe). Sasa hebu tuongelee maeneo haya mawili ya kihisia.
Jinsi gani ufanikiwe katika maisha: Fanya unachopenda
Yawezekana kabisa unajishughulisha na kitu ambacho hukipendi ila unajilazimisha kufanya. Sijui umeajiriwa, au una fanya biashara ambayo huipendi ila unajisemea moyoni nikiacha nitakula nini. Hilo ni tatizo kubwa. Kuna uhusiano mkubwa kati ya kupenda ufanyacho na mafanikio. Vitu hivi viwili ni vigumu kutenganisha. Na unapojishughulisha na kitu usichokipenda na kukifurahia ukweli ni kwamba hutofika popote.
Unapofanya jambo ulipendalo na kulifurahia, unakuwa na msukumo mkubwa uliojaa hamasa. Kifupi unajiendesha kutokana na kusudio lako la kuwepo hapa duniani. Lengo lako la wewe kuwepo duniani huwa ni kubwa kuliko wewe na ukilikosa hilo kusudio lako la kuwepo hapa duniani utashindwa kabisa kuwahudumia wengine.
Jinsi Gani Ufanikiwe Katika Maisha: Kuwa Mnyenyekevu
Kufanya jambo ulipendalo pasipokuwa mnyenyekevu ni hatari – Katika hali ya kufurahia ufanyacho, mtu aweza kabisa kuanzia akilini kujipa haki ya kufanya vitu ambavyo viko mbali sana na utu na hapo utakuwa hulitumikii kusudi lako halisi la kuwepo hapa duniani. Unyenyekevu maana yake ni kukubali uwe chombo chenye kukupa nguvu kiroho, na kubaki ukiweka akili, nguvu macho vyote vikielekea kwenye kusudio lako la maisha.
Unyenyekevu ni kujihudhurisha kikamilifu (Kwa kadri uwezavyo). Kwa lugha ya KIYAHUDI unyenyekevu ni kujipa nafasi ya ziro unapojilinganisha na wengine. Naomba nieleweke vizuri hapa, kuwa ziro haimaanishi ujichukie. Kinachoongelewa hapa ni ile hali ya umimi/kujisikia matawi ya juu (EGO) kutokana na mafanikio yako ndiyo inayoongelewa ya kwamba ikubali kuchukua siti ya nyuma na kuwa tayari sasa kupokea nguvu kutoka juu.
Kwa kumalizia kufanya upendacho siku zote utakuwa ukisukumwa kusonga mbele na wakati unyenyekevu utakufanya ulitumikie kusudio lako katika maisha. Hivyo umeweza kuona kwa nini funguo hizi mbili zilivyo muhimu kuelekea mafanio.
Natamani Dr. Kimambo, ambaye yumo katika hili kundi kama angeweza kuliongelea suala hili (Purpose Driven Life). Najua ametingwa na majukumu lakini ni maombi yangu siku moja aweze kuliongelea. Ni jambo la muhimu sana wana karakana ya ubongo kulielewa.
Nategemea maswali mengi ili tupate uelewa kamili na kuanza kuishi inavyotakiwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...