Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mambo Ya Kuzingatia Ili Kuwa Na Siku Yenye Tija.

Maisha tunayoishi yanahitaji nidhamu ili kuelekea kwenye mafanikio tunayotarajia.
Leo naomba nikushirikishe yafuatayo:-

  1. Kila siku unahitajika kupanga malengo unayotarajia kuyakamilisha siku inayofuata. Tendo hili ni vyema likafanyika usiku kabla ya kulala.
Nakushauri uwe na noti buku maalum kwa ajili ya kuandika malengo yako ya kila siku.

  1. Kuwa mtu wa matokeo na sio maneno – Utakumbuka nimewahi kukusisitiza kabla hujalala orodhesha mambo angalau sita unayotarajia kufanya siku inayofuata. Ninasisitiza tena kuhakikisha unafanya hivyo.
Ukisha orodhesha, jiulize swali moja kuu – Kama utalazimika kufanya jambo moja tu kati ya hayo sita, je ni lipi utalipa kipaumbele na mengine ukayaacha. Tafadhali zungushia hilo jambo mara moja.
Kitakachofuata ikiwezekana zima simu yako na mara moja anza kukifanya kwa kanuni ya kuwa ukianza hakuna mapumziko mpaka umemaliza ndipo waweza kujipa dk kumi au kumi na tano za kuanza kuandika mawazo (ideas) yatakayoanza kukujia kwenye kinotibuku chako cha kurekodi mawazo hayo (Brain dumping note book).
Hili litatokea tu iwapo utafanya shughuli hiyo pasipo muingilianao wa simu au tv au paka au mbwa. Fanya ukiwa umedhamiria kiakili, nguvu na muda wako katika hilo jambo tu. Hii pia njia mojawapo ya kutahajudi.

  1. Kuwa mtu wa watu – Kimsingi sijawahi na kamwe haitakuja kutokea mtu awaye yeyote kuweza kufikia mafanikio kwa maana ya mafanikio pasipo msaada au ushirikiano wa watu wengine.
Hivyo huna budi kuwa mtu wa mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka bila kujali huyu ni tajiri au muhitaji, kilema, watoto na mtu awaye yeyote, hakikisha huoneshi utafauti namna unavyowachukulia na kuwapa heshima. Kumbukeni habari ya unyenyekevu (Kujisikia kwetu au kujiona kwetu, namaanisha umimi lazima uwe zero).
Kama unajihusisha na mauzo ya bidhaa au huduma naomba nikukumbushe ya kuwa watu hawaji kununua ati una bei nzuri, la hasha. Nyakati za watu kukimbilia bei nzuri zimepitwa na wakati.
Kikubwa ni MAHUSIANO. Hakikisha unajikomba kwa wateja wako kwa kadri uwezavyo kwa kuwapa huduma na kauli njema kupindukia. Kuwa mbunifu kwa kuwafanyia vitu ambavyo kamwe kwingine hawavipati, mfano jua birthday ya kila mteja wako. Weka kumbukumbu vizuri na kila birthday ya mtu ikifika hakikisha unamtakia birth day njema na ikibidi nunua min cake na card mpe. Jenga huo utamaduni. Wakati mwinge akinunua sana mpe complimentary kama mfano daftari na peni ampelekee mtoto. Kumbuka faida uliyotengeneza kwa vitu alivyonunua ni kubwa kiasi cha kwamba daftari na peni haviwezi kukutia hasara.
Wakati mwingine jiwekee kautaratibu hata kumkodia bodaboda au bajaji iwapo mzigo ni mkubwa.
Ukiweza miliki bodaboda na bajaji kwa ajili ya kuhudumia wateja inapobidi.
Natamani ningewakusanya pamoja niwape maujanja lukuki ya huduma kwa mteja na uone kama biashara yako itabaki kama ilivyo sasa.
Naamini iko siku tutakusanyika mahali na kupeana dozi sahihi.
Nazidi kuwaza kwa sauti – Mwaka unapoanza ni vyema tukakaa pamoja na kuongea mambo nyeti ya kutukomboa kiuchumi. Kila mwaka nitakuwa na semina moja kwa wana karakana ya ubongo.

  1. Afya – Kama una ndoto kama zangu (Ifikapo Januari 1, 2025 nitakuwa na kituo cha kulelea watoto yatima 500, nitamiliki double coaster 17 kwa ajili ya outing ya week endi, na kuwatoa angalau mara moja kama sio mbili kuvuka mipaka ya nchi ili kujifunza, na nitalipia watoto wa wazazi wasiojiweza kifedha kusomesha chuo kikuu wapatao 10,000).
Sasa ndoto kama hizi lazima uwe katika afya iliyo njema wakati wote. Ushauri wangu:-
Kula vyakula kwa uangalifu. Maana uko jinsi ulivyo kiafaya ni kutokana na vyakula ulavyo. Afya uliyo nayo si kwa bahati mbaya bali ni uchaguzi wako.
Bado una nafasi waweza badilika kabisa katika swala la ulaji. Kula kwa kiasi na tena ukisikia njaa. Kama huna njaa usile. Usile kwa kufuata harufu (Rost, Bugger, pilau nk) Kula kwa umuhimu wa chakula mwilini mwako. Binafsi vyakula vyote vya kutumbukizwa kwenye mafuta na kuopolewa SILI KABISA. Sukari ya viwandani sishauri kutumia, tumia asali au acha kama mimi, Nyama nyekundu kula kwa uangalifu zina madhara mengi mno kiafya nakadhalika maana muda si rafiki. Siku ya semina utapata dozi sawia.
Fanya mazoezi angalau dk 30. Ila itapendeza kama unaweza kukimbia au ketembea haraka haraka angalau km 2 kwa siku na tena kabla hujaianza siku.
Maji – Ukiamka tu kabla ya kuswaki kunywa maji ya kawaida ukiweza ni vizuri Zaidi ya vuguvugu. Kiwango cha maji ni uzito wako kwa kgs gawanya kwa 24 jibu utakalo lipata ni lts za maji upasayo kunywa asubuhi kuuwezesha mwili wako na ubongo kufanya kazi vizuri.
Mara kadhaa usipende lifti, bali tumiaa ngazi.
Nisikuchoshe, kwa leo inatosha ila siku ya semina utapata dozi sawia.
Kumbuka mafanikio yanamuhitaji mtu asiye dhaifu.

  1. Tabia – Kuwa mwaminifu. Weka mkataba wa kuwa mkweli siku zote za maisha yako hata kama ukweli utakuumiza wewe ni bora mara mia. Uongo unakuua.

  1. Nidhamu binafsi – Uwezo wa kufanya ulichopanga tena wakati mwingine kwa kujilazimisha maana waweza kutojisikia kufanya lakini kwa kuwa unahitaji nidhamu binafsi hakikisha unafanya iwe jua au mvua. Toa matokeo acha visingizio.

  1. Utoaji – Kutoa ni mwanzo wa mfumo wa siri wa kukuzawadiamaradufu ya utoavyo. Kuwa mtu wa huruma. Saidia watu. Somesha mtoto au watoto wenye mazingira magumu na mengineyo mengi utakayoweza kuyafanya. Ishi maisha ya kuihudumia jamii (Life of contribution) kadri ya mafanikio yako. Mimi ni mkristo, jambo hili limenipeleka mbali Zaidi hata utoaji wangu wa sadaka nimeubadilisha kabisa. Sina lugha nyingine ya kukusisitiza juu ya utoaji. Ukitaka kujaribu ili uthitishe hakuna njia nyingine Zaidi ya kuanza na uone utakavyoishi kwa furaha na kutopungukiwa pesa. Hii ni kanuni ya ajabu ya dunia maana haichagui mtu. Yeyote aliye mtoaji lazima atarudishiwa Zaidi ya anavyotoa. Mwenye ufahamu na afahamu hili nisemalo.

  1. Acha kitu/vitu katika ubora Zaidi ya ulivyokuta – Kama ni mpangaji na ukitaka kuhama nyumba hakikisha unaikarabati kwa uzuri kuliko ulivyo kabidhiwa na usidai pesa uliyotumia. Kama unakunywa maji barabarani au kwenye basi tafadhali usitupe hovyo chupa mpaka utakapokuta dustbin. Na kama ni kwenye gari yako tafadhali weka chupa ndani ya gari acha kutupa barabarani. Kama umetoka kula chakula hotelini na ukapewa kijiti nakuomba usikitupe barabarani mpaka kwenye dustbin ikibidi beba kwenye mfuko mpaka utakapo pata eneo sahihi.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia, maana najisikia vizuri sana ninapoweza kuwa msaada kwa mtu. Mimi ni mtumishi wenu. Na kwa vile umeamua mwenyewe kuwemo humu basi huna budi kuhakikisha tunajadili kwa pamoja na kufikia suluhisho muafaka kwa maisha yetu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...