Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mwaka unafikia ukingoni, Nini Cha Kufanya?

Tunapokaribia mwisho wa mwaka kuna mambo ya muhimu ya kufanya.
Hebu tenga muda ili kutathmini mwaka unaoishia katika maeneo makuu yafuatayo:-
  1. Mafanikio yako binafsi na ya kifani yameboreka?
  1. Umetoka wapi? Uko wapi? Na unakwenda wapi?
  1. Una akiba kiasi gani? Una madeni kiasi gani? Una miradi yenye thamani gani? Je uwekezaji wako umefikia hatua gani?
  1. Afya yako ikoje?
  1. Mahusiano yako na mwenzi wako yakoje?
  1. Je ni nini mafanikio yako 2017? Je waweza orodhesha?
  1. Nguo zipi hujawahi kuzivaa kwa mwaka mzima? Hebu zitenge pembeni
  1. Group lipi la watsApp hujawahi ingia na kusoma?
  1. Wesites zipi umedowload lakini huwajawahi soma
  1. Ingia store yako ya jiko - je kuna makolokolo kiasi gani?
  1. Je wajua jinsi ya kupunguza kiwango cha kulipa kodi ya mapato?
  1. Je una mlundikano wa magazeti yasiyokufaa kwa sasa?
Msimamo unabaki pale pale ya kwamba hakuna mwaka mpya pasipo wewe kuwa mpya kwani mambo yatabaki kuwa yaleyale.
Hata upate muda wa kupanga malengo ya mwaka bado mwaka utaisha na hakuna kitu utafanya maana shida ni wewe hujabadilika.
Ninapoongelea juu ya kuuanza mwaka mpya ni pale wewe unapokuwa tayari una badiliko na una hamasa ya kufanya mambo makubwa. Sasa ukiwa na badiliko unakuwa na sifa za kusoma Makala hii.
Lakini kama hata kurasa kumi kwa siku huwezi kusoma na kuweza kushirikisha wana karakana ya ubongo, basi wewe ni mgonjwa na kama ni maradhi basi uko wodi ya watu mahututi. Kwangu kuweza kujisomea kurasa kumi na kushirikisha wenzako ni kigezo tosha ya kuwa umeanza kujielewa.
Nasikitika, kuna watu tangu wajiunge karakana ya ubongo wamekuwa wapo wapo tu. Mungu tuhurumie maana safari ni ndefu kwa tabia hii.
Sasa acha niongee na wewe ambaye hata hulalamiki kuwepo kwa Makala ndefu kama hii ya leo lakini unafurahia kusoma mpaka mwisho wa sentensi ili kuweza kujifunza.
Mosi – Nenda hospitali. Fanya check up ya mwili mzima. Usisahau meno, macho, kisukari, moyo, HIV. Kifupi jicheki kila kitu katika mwili pamoja na uzito wako.
Ukisha pima afya, tafadhali pokea ushauri wa daktari na ufanyie kazi kikamilifu. Maana ukiwa dhaifu hata maongezi tunayo yafanya hayatakuwa na maana yoyote. AFYA KWANZA MENGINE YAFUATE.
Pili cheki mahusiano yako na mwenzi wako, watoto, majirani, ushiriki wako kwenye mambo ya kijamii na kadhalika - je yako kwenye hali gani. Na nini ufanye ili kuyaboresha. Mahusiano yakiwa mabovu utapoteza hamasa ya kufanya kazi ili mambo yatokee. Hakikisha una mahusianao mazuri kila kona. Kuwa mtu wa watu. Kama utahitaji msaada katika eneo hili naomba tuwasiliane kuweza kusaidiana.
Tatu hali yako kifedha ukoje?
  1. Orodhesha rasilimali zako zote (Vitu vyote vinavyokuingizia pesa) mfano miradi, uwekezaji kupitia hisa, majumba na fremu unazopangisha na kadhalika
  2. Orodhesha vitu vyote vinavyokutoa pesa. Mfano gari – Linahitaji bajeti maalumu ya mafuta, matengenezo, vipuri vya mara kwa mara, vibali kama stika ya insuarance, wiki ya nenda kwa usalama na vinginevyo. Na kisha jiulize swali ni kweli umefikia kiwango cha kumiliki gari? Au ndio ule ulimbukeni wa kujionesha na wewe umo. Kuwa mwangalifu isiwe ni kigezo cha kupunguza speedi ya mafanikio. Mambo huenda kwa hatua kama makuzi nya mtoto. Mtoto hawezi kuzaliwa na ghafla akanza kutembea. Ikitokea hivyo kila mtu atasema ni uchuro.
Mimi ni mmojawapo wa watu niliyependa kuishi maisha ya kujionesha na yamenigharimu sana. Katika maisha yangu nimemiliki magari kuanzia Nissan Patrol, Pegeout, Suzuki, Pikipiki lakini baada ya kujitambua, sasa hivi vyote nimeuza na napanda daladala na mwendokasi maana ndio saizi yangu kwa sasa.
Ushauri wangu – ukiweza kuwa na pesa ya dharura yenye kutosheleza mwaka mzima na imekuwa hivyo mfululizo kwa miaka mitatu sasa, wewe hakika gari linakuhusu na utalimudu bila shida. Ninaposema pesa ya dharura ya mwaka mzima maana yangu ni kwamba ukiacha kuzalisha una uwezo wa kuishi maisha unayoishi sasa bila kumsumbua mtu yeyote kwa mwaka mzima.
Naomba nieleweke vizuri, sisemi gari baya, la hasha. Kuna baadhi ya shughuli unalazimika kuwa na gari ili kuendesha biashara yako vizuri maana ukiwa unakodi mara kwa mara gharama zinakuwa kubwa na faida hupotea. Gari la jinsi hii nunua haraka sana.
Gari ninalolisema mimi ni lile unalolitumia kama taxi maana kila mahali unalo. Ukienda uwanja wa taifa unalo. Ukienda beach unalo. Ukienda msalimia girl friend wako unalo. Hata nidhamu ya jinsi ya kutumia gari hujui.
Naomba nitoe kanuni ya kutumia gari binafsi – TUMIA GARI LAKO MITHILI YA GARI LA WAGONJWA (AMBULENCE). GARI LAKO LITUMIKE IWAPO NI LAZIMA. HAPO TUMIA LAKINI KAMWE USILITUMIE KAMA TAXI AU VAZI. KILA MTU AKIONA GARI ANASEMA JAMAA HUYO ANAKUJA MAANA MPAKA NAMBA YA GARI KILA MTU ANAIJUA.
Unapotaka kuchukua gari wewe jiulize kwani siwezi kwenda kwa daladala au kwa mguu? Kama jibu yawezekana acha gari. Najua hutaeleweka na walio wengi. Mimi sijui wewe, lakini mimi siishi kufurahisha watu. Nina maisha yangu binafsi na najua nakoelekea. Useme usiseme si shughuli yangu na huninyimi usingizi.
  1. Orodhesha nyumba zote ambazo ni za kuishi. Hizi zinakutoa hela kwanza kodi ya serikali ya kumiliki ardhi, pili fedha za ukarabati wa mara kwa mara na kadhalika
Kisha thaminisha vitu vyote vinavyokuingizia pesa na vile vinavyo kuhitaji utoe pesa. Tofauti yake ndio thamani yako ya utajiri kwa wakati huo.
Ukitaka kwenda kwa haraka kwenye mafanikio, jaribu kupunguza vitu vinavyokuhitaji kutoa pesa mfukoni na ongeza vinavyokuingizia pesa.
Mwakani tutajadili sana juu ya maswala haya ya pesa ili tuwekane sawa.
Nne – Nguo zote ambazo kwa mwaka mzima hujathubutu kuzivaa nakuomba zichambue na kuzitenga kwa ajili ya kusaidia wahitaji ila zilizochanika choma moto.
Ninapanga tuweze kwenda hospitali ya muhimbili msikitini na kanisani tukatoe nguo hizo kama wana karakana ya ubongo. Maana kuna watu wengi wenye uhitaji hukimbilia msikitini na kanisani ili wasaidiwe chakula na mavazi.
Kuna siku nilifiwa na ibada ilifanyika pale muhimbili na mchungaji pamoja na mambo mengine alituomba kama tuna mafazi na viatu tusivyotumia basi tupeleke pale wana uhitaji mkubwa.
Ninafanya maandalizi, nikiyakamilisha nitahitaji kujua walio tayari siku ya Jumapili ya tarehe 28.01.2018 saa 8 mchana tuweze kukutana Muhimbili geti la kuingilia tukiwa tumevaa t-shirt zetu za karakana ya ubongo na kofia zake. Tutaendelea kujuzana. Wale wa mikoani na nje ya nchi angalieni uwezekano wa kutuma au kuja. Fanya vile utakavyoona vyema toka moyoni. PAMOJA TUNAWEZA.
Tano: Una akiba kiasi gani? Ninakuomba pesa yoyote inayopita mkononi mwako lazima ifuate kanuni ya 70/30 na si vinginevyo. Hapa ndipo penye siri ya utajiri. Kama hujaelewa njoo inbox tuelezane. Ni muhimu sana hata ukipewa zawadi au kwa wanafunzi boom. Ni lazima pesa ifuate kanuni ya 70/30.
Kama ulikuwa ufuati na mimi ndiyo rafiki na kocha wako; ninakusihi acha tabia mbaya juu ya fedha – fuata kanuni ya 70/30 kuanzia sasa na kuendelea mwaka 2018. Kila mtu aliyetumia hii kanuni tukifikia mwisho wa mwaka 2018 atatoa ushuhuda wa jinsi maisha yake yalivyobadilika.
Kama huna akiba ni kwa sababu hufuati kanuni ya fedha 70/30. Amka na badili muelekeo. INAWEZEKANA KUFIKIA UHURU WA KIFEDHA LAKINI NIDHAMU NI LAZIMA.
Sita – Futa magroup yote ya watsApp yasiyo na tija. Choma magazeti usiyo yatumia. Ingia stoo ya jikoni chambua makolokolo yote yatupe shimo la takataka. Baki na vitu ambavyo ni vya maana. Ingia mwaka 2018 ukiwa na hewa safi kuanzia jikoni hadi chumbani.
Saba  Ushauri kwa wafanya biashara wote  Usiogope kutumia pesa kukaguliwa mahesabu yako ya fedha na makapuni yenye kibali cha kufanya hivyo kwani pesa utakazolipa kwa ajili ya kukaguliwa a zitapunguzwa kwenye kodi ambayo ungeilipa kwa kuwa malipo ya mkaguzi wa mahesabu ni moja ya gharama za uendeshaji biashara.
Wengi wasema ni gharama kutengenezewa mahesabu na makupuni yaliyosajiliwa. Huo ni uwoga usio na maana.
Kimsingi utashangaa faida yako itakavyoanza kupanda kama unaweka kumbukumbu vizuri faida itapanda mara tu utakapoanza kutumia makampuni yaliyothitishwa kufanya ukaguzi kisheria.
Kama una mashaka tafadhali tuwasiliane maana mimi niko na kampuni iliyosajiliwa kufanya ukaguzi kisheria tuweze kuelimishana. Tuna ofisi Dar, Mbeya na sasa Iringa kwa ajili hiyo hiyo ya kuelimisha wajasiriamali.
Kisheria wapo ambao ni lazima wawasilishe mahesabu yaliyokaguliwa na wapo ambao sheria haiwalazimishi ila kwa ushauri wangu njoo nikushauri na utashangaa kiwango cha kodi kitapungua na faida itaongezeka. Hili nina uhakika nalo. NJOO TUSAIDIANE. MAISHA NI KUSHIKAMANA.
Nane na mwisho  Nakuomba orodhesha mafanikio yako yote ya 2017. endo hili litakupa utulivu wa akili na kuanza mwaka kwa hamasa kubwa.
Kumbuka ukitaka mafanikio, hakuna njia ya mkato. Wewe kuwa mtendaji kusababisha vitu vitokee. Tenda ndio lugha ya mafanikio.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...