Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Njia Rahisi ya Kuvunja/Kuacha Tabia mbaya Kuvunja au kuacha tabia mbaya si jambo rahisi.

Wanasaikologia na mtaalamu wa kushugurikia watu walioathirika kiasi cha kuwa mateja wa mambo Fulani ndugu Judson Brewer anasema tabia ni matokeo ya mafuzo yenye kuendana na kuzawadiwa. Tukio kimsingi huleta mafunzo kwenye ubongo kiasi cha kusababisha kuwa na wakati wa ‘kujisikia vizuri’, kama vile ulaji wa vipisi vya keki ya chokoleti. Kuachana na tabia kama hii ya ulaji wa vipande vya keki vya chokoleti huchukua muda – sanasana hii hutokana na sababu ambazo kwa kila tabia ambayo hujitokeza kwa mtu huwa kimsingi imepitia mchakato wa hatua tatu kuanzisha, tabia na zawadi.
Inatakiwa kuijua tabia kwa kina, uelewa wa kujua nini kinachoendelea kwenye ubongo, ili kuweza kubailika kuwa bora Zaidi. Lakini leo nitaelezea njia rahisi ya namna ya kushughulika na tabia mbaya.
Kihistoria, mfumo wa kuzawadiwa kuhusiana na ulaji chakula ni suala la kuweza kuishi yaani kula uendelee kuishi.Brewer yeye anasema kawaida taarifa hupelekwa kwenye ubongo ili kukumbuka sehemu chakula kilipotikana, na mara nyingi iwapo kilikuwa kitamu wakati wa kula. Lakini baada ya muda, ubongo hujitafutia njia ya ubunifu ya kuharakisha mfumo wa kuzawadiwa. Tabia huwa zaidi ya kujitafutia chakula – hugandamana na hisia kiasi cha kutaabiaka kuweza kuachanisha na kuwa kichocheo cha kujisikia vizuri zaidi.
‘Sasa, kutokana na mchakato uleule wa mfumo wa ubungo, tumepitia kutoka kujifunza kwa ajili ya kuishi hadi kufikia hatua ya kujimaliza/kujiua sisi wenyewe kutokana na tabia zifuatazo, ‘Unene kupindukia/hatarishi na uvutaji sigara ni moja ya tabia zinazoongoza kusababisha maradhi na vifo ambavyo kimsingi vingaepukika lakini watu wanaendele kuugua na kufa si tu Tanzania bali dunia nzima.
Njia mojawapo ya kujidanganya iliyo rahisi kukabiliana na hili tatizo ni kwa kuamua kuwa mdadisi, Brewer anasema, katika maabara yake, aliweza kujaribisha athari, ya ubongo juu ya uvutaji, zoezi ambalo lilihusisha kuhamasisha watu wavute sigara lakini wakati huo huo akiwa anapenda kujua kwa kudadisi ya kuwa nini kitatokea katika nyakati hizo za uvutaji sigara. Alichokuja kugundua ni kwamba mwanamama mmoja akatokea kufurahia sana uvutaji sigara kuliko wenzake wote: Uvutaji sigara kwa kuhusisha ubongo: harufu huwa kama chizi (cheese) mbaya na kuwa na radha kama kemikali.
‘ Kujionea kile tupatacho kutokana na tabia zetu hutusaidia kuelewa kwa kiwango cha undani Zaidi – kuijua tabia tokea ndani ya mifupa yetu ili tusijilazimishe kushikamana au kujizuia kujinasua na tabia mbaya’
Brewer anasema, ‘Mwanzo hakuna mwenye kupendelea kujiingiza kwenye tabia mbaya’.
Brewer anasema - hii ndiyo haswa ubongo ulivyo. Huwapa watua kupata picha halisi ya tabia zao, nana kile wakionacho ndicho huleta utofauti. Haitokei mara moja kana kwamba usiku umelala na kesho asubuhi badiliko, lakini watu wanaweza kupata hamasa ya kuanzisha tabia mpya pale wanapopata wasaa kwa kujionea madhara ya tabia/matendo yao mabaya
‘Jambo ambalo laweza onekana kutokuwa na mantiki ni kwamba ubongo ni suala la kupendelea kuwa karibu na kwa mtu mmoja mmoja kujua haswa nini kinatokea kwenye miili yetu na fahamu zetu kila wasaa’
Brewer anasema ‘Utayari wa kuachana na tuliyoyazoea huambatana na udadisi, ambao kimsingi huishia kukuzawadia’

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...