Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Pesa - mwendelezo wa somo la jana

Jana katika kuongelea mahusiano yetu na pesa, tulijifunza sababu zinazofanya pesa ziwakimbie baadhi ya watu kila wakati na wakati huo huo hukimbilia kwenye mifuko ya watu wengine.
Kama tulivyoona, pesa ni kitu chenye uhai chenye uwezo wa kuhusiana na ikitokea umeidhalilisha (umeitumia vibaya) basi mahusiano hayatadumu itabidi pesa ikukimbie.
Hivyo leo katika ‘Mahusiano na pesa’ tutaangalia tiba juu ya mahusiano yaliyoharibika- pesa- mwanadamu-mahusiano.

Tiba kwa mahusiano yaliyovunjika pesa-mahusiano na mtu
Kabla hutujaanza kuangalia tiba juu ya mahusiano yaliyoathirika juu ya pesa, nafikiri ni muhimu tukaongelea baadhi ya Imani walizo nazo watu juu ya pesa ambazo zimekuwa kikwazo kiasi cha kutengeneza ukuta na kukosa kuwa na mahusiano yenye afya na pesa. Iwapo una Imani mbaya juu ya pesa, haijalishi unafanya nini kamwe hautafanikiwa kwa kuwa kimsingi Imani ni compass inayoongoza/kuendesha maisha yetu. Tunavuta na tuko jinsi tulivyo kutokana na tunavyoamini, na si vinginevyo.

Kama huamini ya kuwa ni jambo jema kuwa na pesa na tena kuwa nazo nyingi (kuanzia 2,300,000,000,000 kiwango cha chini), basi Makala hii haikufai naomba ishia hapa hapa kusoma maana makala hii si kwa ajili yako na unapoteza muda wako kuendelea kusoma. Ukweli wa mambo ni huu – Mungu anatuhitaji kila mmoja wetu aweze kuwa nazo nyingi – twaweza kufanya Zaidi, kama Mungu atendavyo, kwa wingi.
Natamani kila mmoja wetu akitafute na kukisoma kitabu kiitwacho ACRES OF DIAMOND by Russell H. Conwell (na kwa wale wenye kufurahia sana somo hili la pesa, nashauri haraka sana pata aina mbili za vitabu na vitakusaidia sana kukubadili jinsi unavyofikiri na pia maisha yako yatabadilika. Vitabu hivyo ni ‘THINK AND GROW RICH’ by Napoleon Hill na ‘THE MILLIONARE MIND’ by Thomas J. Stanley.

  1. Kubadili Matumizi – Pesa inapoinuliwa kiasi cha kuchukua nafasi ya kuwa na uweza katika mahusiano, yaani pesa inapokuwa bwana mkubwa badala ya nafasi yake ya kuwa mtumishi, basi ni suala la muda tu kwani kitakachotokea utakimbiwa na hizo pesa lakini ni baada ya kuharibu maisha yako na kila mtu na chochote ukipendacho, kwa lugha nyingine mtakuwa hoi bin tabaani na kama ni ugonjwa basi utakuwa umeachwa ukiwa chumba cha watu mahuti.
Unahitajika kuhakikisha ya kwamba pesa inabaki na iendelee kuwa mtumishi wako mwaminifu na mzalendo. Kuna njia mbili za kuhakikisha hili linafanyika (Hapa ndipo mahala pangu pa Unyenyekevu), njia hizo ni
  1. MTIZAMO (A T T I T U D E.
There is nothing as powerful as #Attitude. Attitude dictates your response to the present and determines the quality of your future.
You are your Attitude and your attitude is you.
{ If you do not control your Attitude, It will control you. }

  1. UNYENYEKEVU (Gratitude brings progress and complaining is backwardness.)

MTIZAMO: Huna budi kujiangalia kila siku juu ya mtizamo wako – Angalia ya kwamba unakusudia kujiongelesha kila siku ya kwamba pesa ni mtumishi wako. Nitaitumia ili initumikie mimi, familia yangu na watu wengine. Badiliko hili la kimtazamo (kujisemesha wewe mwenyewe) inahitajika Zaidi kadri upatapo watumishi wengi – watumishi wanapokuwa wengi yakupasa kwa unyenyekevu kabisa kujua kama walivyokujia ndivyo wanavyoweza kukuondoka iwapo tu utawadhalilisha (mtumishi-pesa). Mtizamo wako yapasa uwe – nina watumishi wengi ili waweze kufanya mengi mazuri,kunitumikia mimi na wale wote ninaokutana nao katika maisha ya kila siku. Wapende watu na tumia pesa kuwatumikia na si vinginevyo.
Utakapoweza kujitawala juu ya pesa, unadhani nini kitatokea, watu watakuamini na pesa zao na utajiri wao. Mungu (wengine wanaita dunia) atakuamini na zingine nyingi Zaidi. Pesa zitashika adabu na kuanza gwaride la kuelekea kwako kwa kuwa utakuwa umeitendea haki kanuni ya dunia juu ya pesa katika mahusiano halisi kati ya mtu na pesa. Umefanya vyema mtumishi mwaminifu. Umekuwa mwaminifu kwa vichache, nita kupa vingi Zaidi (REF. MATT 25:23)
UNYENYEKEVU – Kukubali ya kuwa Mungu yupo (au dunia kwa wasioamini) ambaye amekupa neema ya kuwa mtunzaji juu ya watumishi (pesa) kaika uwezo wako; kumbuka, hatumiliki tulivyonavyo, tu watunzaji tu na siku moja tutatoa hesabu  jinsi tulivyofanya kwa kila senti iliyopita katika utunzaji wetu.
Sasa unasema, ‘Nimejituma sana kupata pesa zangu’ Ok ngoja nikuambie,
Ni nani aliyekupa uhai na afya uliyonayo, uwezo wa akili na hamasa ya kufanya? Waweza nunua dawa lakini si uhai/afya, waweza nunua elimu lakini si uelewa/busara, waweza wekeza utakavyo lakini huna udhibiti juu ya faida…mtizamo wenye kuambatana na unyenyekevu utakufikisha mbali pamoja na watu na Mungu. Kuwa mtu wa shukrani kwa kila senti inayopita mikononi mwako.
Kukusanya na kuhifazi
Bwana mmoja katika moja ya historia za biblia aliwapa talanta (pesa) kwa watumishi watatu na akasafiri nchi ya mbali. Na aliporudi alihitaji kila mtu aeleze alichokifanya na fedha (talanta) alizowaachia. Yule aliyepewa 5 alirudisha na ziada ya talanta 5 na aliyepewa 3 alirudisha zingine 3 zaidi na yule aliyepewa 1 alirudisha ile ile 1 aliyokuwa amepewa. BWANA alikasirika, alimwambia,kama ilikuwa ngumu kwako kuifanyia biashara si heri ungeipeleka bank ambako angalau ingepatikana faida kidogo kuliko hivi ulivyofanya. Ndipo alipoamua kumpokonya hiyo talanta 1 na kumpatia yule mwenye jumla ya talanta 10. Mtumishi mwenye talanta 1 aliadhibiwa kwa kuhifadhi badala ya kuwekeza (Ref. Matt25:14-30)
Pesa kama mtumishi analazimika kufanya kazi na siyo kufichwa. Inatakiwa kubadilishana kwa huduma na bidhaa.
Watumishi wako wapo ili wakutumikie na kukuzalishia hivyo unapokuwa na watumishi wengi kwenye uwekezaji, uzalishaji ni lazima. Watende mema hata ukiwa haupo – waweze kuleta bidhaa na huduma kwako na wengine na kukufanya mwenye furaha – kwa kujitengenezea mazingira mubashara kwa ajili yako na familia.
Huu ni ushauri unaotolewa ya kuwa pesa kila ikipita mkononi mwako ni lazima uigawe. Mfano mmojawapo ni
Ishi kwa kutegemea 60% - ishi kwa upatacho kisha ongeza vyanzo
Wekeza 10% weka kwenye uwekezaji
Akiba 10% kwa malengo mmaalum hasa hasa uzalishaji
Akiba ya watoto 10%
10% msaada
Kwa wale wenye vipato vikubwa (watumishi), mfano hujaoa au kuolewa na ukawa unajipatia Zaidi ya 3,000,000 kwa mwezi. Naamini kwa maisha ya kitanzania hiyo ni pesa murua sana kuweza kuifanyia mipango vizuri.
Huo ndio ushauri wangu – kamwe usiruhusu kuitumia pesa kabla ya kuigawa katika mafungu. Hebu kuwa na bahasha kila moja na jina lake kutokana na mgawo.
Mifano ni mingi ya kugawa pesa (Financial Planning). Chagua mfano mmoja wapo na utumie. Kazi kwako.
Wafujaji Pesa – Jana niliongelea kwa kina.
Falsafa ninayoshauri watu waifuate linapokuja suala la matumizi ya hela ni ‘Ishi ndani ya uwezo wako,  kisha ongeza vyanzo’. Pata hamasa ya kuongeza njia za kujipatia vipato ili uweze kuishi kwa kujinafasi kutokana na ongezeko la fedha. Mimi siko kinyume na kuishi maisha ya kifahari bali niko kinyume na watu waishio maisha ya kifahari kwa kutumia 100% ya vipato vyao na au kwa kukopa pesa kulinda hadhi isiyo wastahili.
Kama utakopa ili kununua, kama huna uwezo wa kununua achana nacho (isipokuwa kukopa kwa faida ni kule kunakohusisha uzalishaji na si vinginevyo). Ni ujinga wa hali ya juu kukopa pesa ili kulinda aina Fulani ya maisha kama vile kununua gari kwa mkopo ni ujinga, kupanga nyumba kubwa kwa kukopa ni ujinga,  kununua vitu vya thamani kubwa kwa njia ya kukopa ni ujinga, kununua mavazi ya thamani kwa kukopa ni ujinga au kwenda likizo kwa mkopo ni ujinga. Mungu atusaidie.
Ushauri wa bure kuhakikisha matumizi yako yako sawia:
  1. Panga nyumba ambayo kodi haizidi 10% ya kipato naamaanisha faida kama wewe ni mfanyabiashara na kwa mfanyakazi ni ile hela unayopewa baada ya makato ya kisheria (Kama ni mkopo wa nyumba basi makato yasizidi 30%)
  2. Zibiti matumizi ya kulifanya gari lako liwe barabarani yaani gharama sisizidi 10% ya faida kwa mwezi au ule mshahara baada ya makato ya kisheria.
  3. Ishi kwa 40% - 60% ya faida yako ya mwezi au mshahara unaopewa mkononi. Acha kipato chako kiamue aina ya maisha ya kuishi na si vinginevyo.
Jambo la mwisho ni nyeti sana, watu wengi huruhusu marafiki, ndugu na wafanyakazi wenzao kuwafanyia maamuzi (kushinikiza) kuingia kwenye aina ya maisha wasiyo na uwezo nayo yaani mahali waishipo, nyumba na aina ya gari wanalotumia ni majanga matupu maana si kwa kipato chao. Kwa namna yoyote ile pata hamasa kwa utajiri wa marafiki zako lakini usirukie na kuiga aina ya maisha yao kabla hujafikia huko kifedha.
ISHI KUTOKANA NA KIPATO CHAKO KISHA ONGEZA VYANZO VYA KIPATO

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...