Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Pesa - Sehemu ya mwisho

Marafiki waweza kufanya maono yako yapanuke zaidi kwa upande mmoja lakini pia waweza kukuzimisha juu ya maono yako, je wewe uko na lipi kati ya hayo mawili…’ Tim Kyara.
Siku ya kwanza:Tulijifunza ni kwa jinsi gani unaweza kuidhalilisha pesa nayo ikakukimbia
Siku ya pili: Tulijifunza ni kwa njinsi gani twaweza tibu mahusiano yaliyovunjika

Siku ya Tatu: Leo tutajifunza ukaribu wetu na baadhi ya watu unavyoweza athiri mahusiano yetu na pesa.
‘…Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema…’
‘mwanadamu huzaliwa akiwa huru, lakini kila sehemu yuko na minyororo imemviringisha’ (man is born free, but everywhere he is in chain) Hii ni nukuu kutoka kwa Jacques Rousseau, Mfaranza mwenye philiosofia ya  siasa (1712 – 1778).
Ni kwa nini anasema hivi?
Kwa nini baadhi ya watu hupata pesa kirahisi sana kuliko wengine wenye kushishughulisha sana lakini huishia kupata kiduchu na kuweka kwenye mifuko yenye matundu, kwa kawaida mifuko hiyo huunganishwa na mabomba yanayozisafirisha pesa hizo kuwaelekea wale ambao kwao kuzipata pesa si shida maana huzipata kirahisi.
Watu wako wa karibu watakuamulia mapato yako yawe kiasi gani (Your network will decide your networth) hii inamaanisha ya kwamba utafanikiwa kifedha pia kimaisha kutegemeana na watu unaowaruhusu kushirikiana nao katika maisha yako
Kuna watu unatakiwa uvunje uhusiano mara moja lakini kuna aina ya watu huna budi kupalilia mahusiano nao kwa kuwa wanacho kile ambacho unakihangaikia ukipate katika maisha yako.
… ni rahisi, muulize MUUMBAJI. Mtengenezaji ndiye hutoa jina ya hichi kiitwe vile na kadhalika na hutoa majina kulingana na matumizi yake au lengo lake kutegeana na jinsi alivyokitengeneza. Kwa mfano, gari aina ya BMW haliwezi likajiamulia liwe FIAT au ukiweka mafuta aina ya diesel kwenye gari inayotumia petrol, gari halitatembea…kila wakati angalia kitabu cha maelezo ya matumizi (Refer to the manual always). Huwezi kujua wewe ni nani na uliumbwa kwa kusudio gani na utendeje, tembelea kitabu cha aliyekuzalisha (Refer your manufacturer’s manual).
Ni kwa jinsi gani utafanya maamuzi ya yupi uwe naye na yupi hapana; Nafikiri jibu ni rahisi lakini wengi hawalijui:
Nina amini mtu yeyote atakayehusiana nawe ni lazima aoneshe mambo makuu matatu:
Kuheshimu Uwepo Wako – Watu wanostahili kuwa pamoja nawe mara zote watathamini uwepo wako ( Pia na muda wako), watakuinua kinafsi, watakutia moyo na kila mtakapokua mnatawanyika mara tu baada ya kuwa mumeonana unajisikia umeinuliwa na kuwa u bora zaidi kuliko kabla ya kukutana. Ni watu wanaoongeza thamani kwenye nafsi yako; Ni rasilimali zako hata kama hawakupi senti yoyote kwani wamekuwa wakikupatia kitu ambacho pesa hakiwezi kununua..Nafsi iliyoinuliwa, iliyohamasika,na kuchochewa kuendelea kufanya unachokipenda hata kama hupati pesa na kuamua kujibidisha zaidi ni vitu adimu sana mtu kuwa navyo lakini marafiki sahihi hukupatia.
Kama utampatia mtu (au sehemu) muda wako Na utakayoyapata kwa huyo mtu au watu ni kukatishwa tamaa, kupewa msongo wa mawazo na mambo hasi kibao, huh…

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...