Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Pesa

Naomba kabla sijaanza kuandika chochote nimshukuru sana Mchungaji Timoth Kyara ambaye ni rafiki na kocha wangu kwa jinsi alivyonifundisha na anaendelea kunifundisha juu ya pesa. Na mengi nitakayokushirikisha hapa ni yale nilijifunza kwake na baada ya kuona ni elimu murua ya kuweza kushirikisha wana karakana ya ubongo nikaamua kufanya hivyo. Karibu tuendelee.
Kuna msemo wa kiingereza usemao ‘A fool and his money are soon parted’ pia ‘man is born free, but everywhere he is in chain’ by Jean Jacques Rousseau, French Political Philosopher (1972 – 1978).
Kwa nini iko hivyo? Hivi umewahi kujiuliza inakuwaje baadhi ya watu kwao kupata pesa ni kitu raisi sana lakini kwa wengine ni kinyume kwani hujituma sana na kuishia kupata kiduchu ambapo huingiza kwenye mifuko iliyotoboka, kwa kawaida pesa za watu wa jinsi hii zimeungamanishwa na mabomba ambayo kimsingi pesa ikiingia tu mfukoni husafirishwa mara moja kwenda kusikojulikana na kumuacha mtu akiwa kapuku.
Kama kuna kitu nataka ujifunze leo basi ni ukweli kwamba ‘Hakuna kitu hutokea kwa sababu ya kutokea’. Kuna sababu kwa kila jambo. Kama ilivyo kanuni ya mvutano (Gravitational Force) – Ukirusha chochote juu ni lazima kishuke chini tena kwa spidi ya 9.81m/s2 au kama lilivyo jua huchomoza kutokea mashariki na huzamia magharibi ndivyo hivyo ilivyo kwa pesa kwa kila maisha mwanadamu hutawaliwa na kanuni za dunia. Jifunze juu ya pesa/Sheria za pesa na zitumie zikufaidishe.
Kwanini mahusiano yako na pesa yamefarakana?
Jaribu kurudi nyuma miaka 10, 5, au hata 2; Hebu chunguza marafiki zako wote wa karibu nawe ambao kwa sasa wameachana nawe na wengine wewe uliamua kuachana nao. Kuna kitu kilitokea katika mahusiano yenu kilichosababisha kutokuwa tena marafiki. Kitu cha kusikitisha, mahusiano mengi ambayo yamevunjika na mengine yako njiani kuvunjika ni kutokana na mapungufu ya kutopalilia mahusiano (waulize wenye mahusiano yaliyovunjika ya boy fiend na girl friend vilevile wana ndoa utaelewa kwa undani umuhimu wa kupalilia au kuweka mazingira yenye rutuba kimahusiano).
Sababu zingine ni pamoja na kutengwa, kupishana mitizamo/misimamo, kudharauliana na mengine mengi.
Pesa twaweza ifananisha na kiumbe hai chenye uwezo wa kuhusiana na kiumbe kingine hai. Kuna mahusiano makubwa kati yako na pesa ambazo kimsingi unabaki kuwa mwenye kuzihozi, kwa hiyo pesa iwapo mikononi mwako una mamlaka nayo ya kufanya chochote upendacho.  Kuna mithali ya kiingereza inasema ‘a fool and his money are soon parted’ says it all. Wakati pesa yako inapo kazana kukukimbia, ni wakati mzuri wa kufikiri; Labda umemkatisha tamaa  na hivyo kumfanya ajongee.
Moja ya njia ya kuvunja uhusiano ni kumdhalilisha mwenzako kila wakati ambapo chaguo pekee linabaki kujongea kutengana kabisa kimahusiano. Hivyo, unapowaza juu ya pesa kila mara inakukimbia yawezekana umekuwa ukiidhalilisha na ndio maana imeona njia pekee ni kukukimbia.
Sasa kama utapenda, ngoja nichambue namna tunavyodhalilisha pesa hata zishindwe kutulia na kuamua kutukimbia.
Udhalalishwaji wa mahusiano na pesa
Neno kudhalilisha kifupi linamaanisha matumizi yasiyo ya kawaida, yaani ‘matumizi ambayo siyo yaliyokusudiwa’. Kwa maneno mengine ili kuelezea vizuri ni sawia na kusema kutumika vibaya, kushindwa kushikilia, matumizi mabovu na kadhalika. Ni rahisi sana kudhalilisha mahusiano na pesa na yaweza kuwa na madhala yenye sura tofauti.
Wakati nikitambua kwa hakika ya kuwa kuna namna mbalimbali ambazo zinaashilia namna tunavyodhalilisha pesa tunapojaribu kuhusiana, hivyo kwa lengo la somo hili la leo, nimechagua mambo matatu ambayo yanabeba mizania ya juu kabisa:
  1. Kubadili Matumizi – ‘Pesa kwa namna mbalimbali yafananishwa na moto, ni mtumishi mzuri kwa upande mmoja lakini ni bwana mwenye kutisha kwa upande mwingine’. P.T.Barnum mwanafalsafa mashuhuri anasema ‘penda watu, tumia pesa kuwaokoa na kuwahudumia’. Katika mahusiano ya kudhalilisha, mtu anapenda pesa na huwatumia watu kuzipata (kuokoa na kutumikia) pesa. Katika mazingira ya jinsi hii, pesa hukoma kuwa mtumishi, na hugeuka kuwa bwana, bwana mwenye kutisha.
Unapoipaisha pesa hadi ikachukua nafasi ya kuwa bwana mkubwa, ni suala la muda tu itakushughulikia kwa kukuangamiza na hatimaye kuweza kukutoweka kabisa.
Pesa huwa bwana mkubwa kwako pale inapotokea ‘Waweza fanya chochote’ ilikuhakikisha unazishika (kutumika/kuokoa) kwa kufikia hatua hii tamaa inakuwa imechua nafasi. Tamaa kimsingi ni hali ya kutaka Zaidi yaani kutotosheka…kwa kawaida hali hii ugubikwa na hofu ya kujiona una upungufu.
  1. Kukusanya na Kuhifadhi – Pesa ni sarafu/noti lakini pia ni mtumishi; sarafu/noti, inatakiwa izunguke (ikibadilisha mikono kwa kupitia huduma na bidhaa) na pia kama mtumishi, pesa yatakiwa itumikishwe. Nani miongoni mwetu angefurahia mfanyakazi wake wa ndani awe anakaa tu siku nzima huku ukiwa umemwajiri achape kazi? Vivyo hivyo bwawa lisilo na maji au mkondo wa maji litaishia kunuka na kuua viumbe vyote hai vilivyokuwa vimewekwa humo.
Watu wenye fikra za kimasikini hupata tabu kuiachia pesa ikatumike. Kinachotokea huing’ang’ania na kuiweka kifungoni gerezani yaani ‘bank’. Ndugu yangu huu ndio udhalilishaji tunaoongelea hapa uhusuyo mahusiano ya mwanadamu na pesa katika ubora wake.
Hebu jipendelee na chunguza, kisha chagua bank ya chaguo lako na kisha endelea na uchunguzi uone faida watakayokupa kwa kuwekeza pesa kwao bila kufanya kazi huku ikiendelea kupungua thamani. Kama ikitokea umeweka pesa kwenye account isiyo ya akiba kiasi cha Tshs. 10,000 katika benki uliyoichagua wewe mwenyewe, pasi shaka kila mwezi watakukata gharama za kukutunzia pesa. Sasa chambua kupungua kwa thamani na gharama za bank wakatazo kukata kwenye pesa yako; utagundua ya kwamba mwisho wa mwaka utachukua kiwango pungufu kwa thamani na pia kwa kiwango.
Pesa katika sura yake ya sarafu au noti au fedha kwa sura ya kuwa mtumishi kamwe haitakiwi kukusanywa na kuhifadhiwa, Na kama utafanya hivyo, basi hapo utakuwa unadhalilisha mahusiano yako na pesa na muda si mrefu utajikuta umekaa kwenye kundi la kupoteza pesa.
  1. Ufujaji Pesa
Wakati kukusanya na kuzihifadhi fedha ni moja ya mahusiano mabaya ya kudhalalishana kuliko jambo lingine lolote linapokuja suala la mahusiano ya pesa na mwanadamu, ufujaji pesa ni udhalalishaji mwingine. Huu ni upotevu, matumizi ya hovyo pasi kaba na kutojali matumizi ya pesa; kutokuwa na mipango na pesa, pasipo kufikiri bali kuendeshwa kwa hisia na sifa sisizo na tija yoyote ile inapokuja suala la matumizi.
‘Kununua vitu usivyovihitaji (vitu vya anasa) pasipo pesa bali kupita kukopa ili tu kuwaridhisha watu ambao yu mkini hata hawavitaki (marafiki, ndugu, majirani)’ Ufanyapo hili, kumuka litakuchelewesha kufikia uhuru wa kifedha siku za usoni.
Pesa ni nyenzo, mtumwa na silaha yenye nguvu; jifunze kuitumia vyema – si kwa ufujaji au kutokuwa makini – iachilie (spend wisely). Busara ni pale unapojua wapi na kwa jinsi gani ya kutumia pesa iweze kukutumikia kwa ubora wa hali ya juu.
Kesho tutaendea na somo hili la pesa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...