Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Si Kasi Ya Saa Bali Kasi Ya Ubongo

Ukijisahau muda unasonga mbele na ukijitathimini unajutia ya kwamba umepoteza muda.

Ukweli unabaki pale pale ya kwamba kamwe hutoweza kurudisha muda uliopotea.

Upande wa pili wa shilingi ni ubongo wako. Napenda leo utambue ya kwamba si suala la saa tu kwenda kasi na wewe kutofanya kitu bali zaidi sana ubongo wako una kasi ya kuelekea wapi.

Kumbuka uwazacho ndicho kinakuelezea wewe. Ubongo wetu unafanya kazi zaidi ya komputa.

Ninachojaribu kukielezea hapa ni kwamba tunahitajika kuzitumia bongo zetu zaidi ya kuangalia saa inavyo zidi songa mbele.

Ubongo wetu una macho na uchaguzi unao wewe kuangalia kwa kutumia macho ya kawaida au kuangalia kwa kutumia ubongo.

Kuna faida nyingi sana utakapojiruhusu kutumia macho ya ubongo kwani utaanza kuchukulia vitu kwa utofauti na wanaokuzunguka.

Mfano – Yawezekana unapitia maisha ya kukatishwa tamaa, unajishughulisha sana wala huoni kusonga mbele, unaumizwa na watu wako wa karibu kiasi cha kuzalisha maumivu/uchungu moyoni. Inafika mahali unatoa machozi mpaka unadiriki kusema bora kuaga dunia maana maisha yamekugeka. Ukiri wote huu ni kwa sababu umezoea kutumia macho ya kawaida kuona mazingira yako na mambo yanayoendelea kwenye maisha yako.

Leo naomba anza kufanyia mazoezi macho ya ubongo kutafsiri mambo yanayokuzunguka/kukukabili.
Ukitulia na kuanza kujitathimini utaona ya kwamba maumivu yako yanazalisha kitu kizuri ndani yako na habari njema kwamba maumivu ni ya muda tu.

Ukweli wa mambo ni kwamba ukuaji wa mtu mara nyingi hutokea wakati wa vipindi vigumu. Mtu hubadilika na kumbanua maisha yake kwa uwazi zaidi anapopita katika ugumu wa maisha na ukiendelea kuruhusu macho ya ubongo kufanya kazi utaanza kuona namna za kuondokana na hali inayokukabili.

Kumbuka baadhi ya yale unayopitia yamesababishwa na maamuzi yako ya hovyo na sasa una zawadiwa matunda ya maamuzi yasiyo makini lakini pia kuna fundisho utakuwa umepata na baada ya hapo kamwe huwezi rudia maamuzi ya jinsi hiyo.

Ushauri wangu kwako – usiwe mtu wa kukurupuka kufanya maamuzi. Hakuna kitu kipya utaanzisha ambacho hakina mtu akifanyacho. Tumia njia rahisi ya mafanikio – Kuuliza. Waulize ambao tayari wanafanya unachotaka kukifanya. Utapata mambo mengi na kwa gharama nafuu.

Nyenzo yenye nguvu kuliko zote zikufaazo kukabiliana na changamoto ni ubongo wako.
Acha kulalamika. Shughulisha ubongo wako. Utashangazwa kwa jinsi maisha yako yanavyorahisishwa kwa yale yatakayokuwa yakizalishwa na ubongo kukusaidia kutoka kwenye changamoto ya aina yoyote.

Fursa nyingi zimechanganyika na changamoto. Kinachotokea kwa watu wanaofanikisha maisha ni kwamba wanajua kulamika ni kuua uwezo wa kuona fursa.
Kinachotokea wakati wengine wanalalamika na kubwa zaidi wanaelezea mpaka sababu za wao kushindwa kufanya mambo yakaonekana na hivyo kujikatatia tamaa.

Mfano mzuri ni hapa Tanzania kuna kelele nyingi zisizo na maana ati uchumi kipindi cha utawala wa Magufuli umekuwa mgumu. Hii sio kweli kabisa. Macho ya nje yanakudanganya. Ukitumia macho ya ubongo utashangaa fursa lukuki ambazo zinakwenda kutajirisha watu kuliko kipindi chochote cha maraisi waliopita.

Na wakati huo huo kuna watu wataharibikiwa na maisha kuliko kipindi chochote cha maraisi waliopita.

Shida hapa si uchumi umegeuka. La hasha uchumi huu si kwa ajili yako tu. Kila mtu unamgusa. Sasa jiulize iweje wengine wapete wakati wewe unalalama?

Acha kutegemea macho ya mwilini kwa kila jambo. Dunia hii ina uhaba mkubwa wa watu wenye uwezo wa kufikiri na kutatua changamoto mbalimbali. Mafanikio kwa lugha nyepesi ni uwezo wa kutatua changamoto.

Sasa fursa kubwa na yenye kulipa kwa kasi na ambayo haina watu wa kutosha ni hii ya kujiingiza kwenye kufikiri na kutoa suluhisho.
Takwimu zinaonesha dunia nzima ni 3% ndio wana tumia rasilimali hii adimu Ubongo tulionao.
Hapa hakuna aliyesoma wala asiyesoma. Macho ya ubongo yakitumiwa ipasavyo utaanza kuchukulia vitu kwa namna tofauti kabisa ila pia hakuna kazi ngumu na yenye kuogopwa na watu kama kufikiri au kuishughulisha akili.

Mtu akipata changamoto ya fedha anabaki kutapatapa mara marafiki, mara saccos, mara mabenki mpaka kila mtu anajua jamaa kafulia.
Tatizo si fedha. Tatizo anawezaje kusababisha wenye fedha wakampa? Maana kinachokosekana ni kiunganishi cha kumfanya mwenye pesa atoe na maisha yaendelee.
Kwenye changamoto za fedha kanuni nyepesi kutumia inaitwa kwa lugha ya kiingereza OPM – OTHER PEOPLE’S MONOEY (FEDHA ZA WENGINE).
Ukitulia ukahusisha ubongo waweza ibuka na mambo mengi ya jinsi ya kuzipata fedha kwa njia isiyo ya mkopo.
Mfano – Ninamkabili mtu tunayefahamiana na pesa kwake si tatizo. Naomba kukutana naye nikiwa na wazo zuri la kuzalisha pesa na sio kumkopa.
Watu wengi wenye pesa wanajua umuhimu wa kuzifanya pesa zisiwakimbie wakati 97% wanajua kuzifanya pesa ziwakimbie kwa kuwa wakipata tu pesa mawazo ya haraka ni kuzitumia wakati 3% ni watumwa wa kuwekeza pesa na wanaishi kwa sehemu ya faida na sehemu nyingine inarudishwa kuzalisha.
Mfano namwambia nina taarifa kampuni ya bia wanatafuta eneo la hekari tatu lililo karibu na barabara ili waweze jenga ghala na kwa bahati mzee Masudi analo hilo eneo na anahangaika kupata mteja.
Eneo la mzee Masudi analiuza kwa milioni 20 lakini Kiwanda wako tayari wakipata kukinunua kwa millioni 300 lakini hawajui pa kukipata. Ninaomba twende kwa mzee Masood ukinunue kiwanja kiwe chako na ukiwa na hati tayari tuwaone  wahitaji. Mzee Masudi anatumia network yake na anagundua taarifa ni za kweli na anachukua hatua mara moja.
Mwisho wa siku anamshukuru kijana kwa kumpa million 100. Niambie sasa shida iko wapi. Kinachotuumiza ni ubinafsi hutaki na mwingine apate.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...