Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Siku Moja Utatoweka Katika Uso Wa Dunia

Leo nimeonelea vyema tukumbushane ya kuwa hatupo hapa duniani milele. Sote tu wapitaji na sijui kama umewahi kujiuliza hili swali ya kwamba siku moja utatoweka.
Ukilijua hili vizuri hutakuwa na muda wa kupoteza maana kifo hakina taarifa wala kanuni. Hivyo kila siku akupayo Mungu hakikisha unajipangia kufanya vitu kana kwamba kesho hutakuwepo.

Hili litakufanya uwaguse watu wengi Zaidi katika uwepo wako duniani. Utalazimika kuishi maisha yenye maana na kuwa mwangalifu kwa mengi ili uache alama utakapokuwa haupo.
Napenda msemo anaoutumia Joel Nanauka ya kwamba ulikuja duniani binafsi lakini yakupasa kuondoka ukiwa taasisi akimaanisha taasisi si ya mtu mmoja bali ya wengi. Hivyo kuondoka kwako kuache mazungumzo kwa wengi kwa jinsi ulivoyagusa maisha yao na hapo ndipo unakuwa taasisi na sio tena mtu binafsi.


Maisha ni mafupi. Ishi kila siku kwa utimilifu wake (Live full today). Kuwa bora kuliko katika kila jambo ulifanyalo.


Kujua utakufa itakujengea kukumbushwa utakapoondoka watakuongeleaje. Yakupasa kuacha kumbukumbu chanya duniani ya jinsi gani uliwafanya watu wajisikie kwa uwepo wako na jinsi gani binafsi ulijisikia.



Ndio tutaondoka lakini maisha yetu hayana budi kuendelea kuishi. Kuwa mwangalifu wa jinsi unavyoishi.

Hivyo ili kuokoa muda – unahitaji nini? Au unatamani nini? Hicho unachotamani tayari watu wanacho. Inaashiria ya kwamba si muujiza na wewe inawezekana kuwa nacho. Jifunze kupitia kwao na vitabu hata mafunzo mbalimbali yenye kukupelekea kupata kile unachohitaji. Maisha ni mafupi hebu harakisha uache alama.

Na siku zote ukijua unapita tu hapa duniani basi hakikisha hupotezi muda kwa kujishughulisha na kitu kisichokupa furaha moyoni. Ishi maisha yenye maana acha kupoteza muda.

Pia kuwa wewe. Acha kuiga. Jisikilize. Kikubwa uache taswira halisi ya kwako. Kamwe usishindane na mtu. Mashindano halisi ni wewe mwenyewe kwa kuhakikisha kila siku unakuwa bora kuliko jana. Na huo ndio ushindi. Maisha ni mafupi. Kaza mkono katika kazi.
Kuwa tayari kuumia na kujitoa kwa vitu vikufanyavyo kuwa na furaha ukivifanya na kama sivyo achana navyo. Maisha ni mafupi.


Namna pekee ya wewe kufanikiwa ni kuwa na furaha. Acha kuishi maisha ya kuigiza kwa kuwafariji watu kinafiki wakati ndani kabisa ya moyo wako sivyo ulivyo. Maisha ni mafupi.
Kumbuka chochote utakacho kipo ndani yako. Nakumbuka siku moja TD Jakes alisema ‘Walikwenda Kenya siku moja na kukuta watu katika kijiji fulani wanataabika juu ya upatikanaji wa maji. Wengi walipoteza maisha na wengine kuugua sana na kila mtu alilalamika sana. Kilichofanyika kwa haraka ilikuwa kuanza mara moja kupima wapi maji yatapatikana. Cha ajabu palepale walipokuwa wanaishi palikuwa na mwamba wenye maji mengi haijapata tokea. Hivyo utaratibu ukafanyika na watu walishangazwa ya kuwa walikalia maji huku wakifa pasi kujuaâ.
Nini mantiki ya habari hiyo na ujinga waweza kukuangamiza kabisa. Weka juhudi kujitafuta kujua nini kilichomo ndani yako. Hiyo ndio shughuli kuu na huna budi kuifanya kwa kasi. Usije juta na ku…

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...