1. Kitu gani kinakusukuma ufanye. Hivi umewahi hata siku moja kukaa peke yako na ukajisemesha ya kuwa kama pesa sio tatizo hata kidogo ungeweza kufanya nini hapa duniani. Je hiyo orodha unayo?
Orodha hii kimsingi inatakiwa kuwa ndefu angalau vitu au idadi ya mambo yasiyo pungua 100. Nakushauri kama zoezi hili hujawahi kufanya lifanye mara moja. Kuwa na fikra huru maana rasilimali pesa si tatizo tena, hebu orodhesha kila kitu ambacho unatamani kufanya iwapo pesa si tatizo.
Ukisha pata hii orodha, anza kuipitia kwa kuweka mbele tarakimu yaani 1 ukimaanisha uwe umekipata baada yam waka mmoja, 2 baada ya miaka 2 hivyo hivyo 10 hata 20 itategemea nini umeorodhesha. Ukihitaji msaada nipigie tusaidiane. Hii jambo muhimu sana maana huzalisha msukumo wa kufanya mambo yatokee.
2. Kujiamini – Kinachomfanya mtu kuwa na nidhamu ni pale anapokuwa mtekelezaji wa mambo madogomadogo ya kila siku (Daily routine). Mfano kufanya mazoezi, kujisomea, kupangilia ratiba ya angalau mambo sita ya kufanya siku inayofuata, kuamka kabla ya saa kumi na moja, kutahajudi, kuandika malengo yako ya wiki, mwezi na ya mwaka, kusali/kushukuru, kujijengea taswira ya maisha unayoyataka, kupata muda wa kukaa na familia, kumfanyia mtu jambo jema yule ambaye kamwe hutegemei siku moja kukulipa, kufanya kitu unachohofia kukifanya au hujawahi kufanya, kuwasiliana na watu wapya. Kuwaandikia angalau watu wawili kila wiki kuwashukuru kwa lolote ulilotendewa. Orodha yaweza kunyambulishwa. Mambo ya jinsi hii ukijipangia kufanya na ukafanya kujiamini huongezeka.
3. Kufurahi toka ndani na sio feki furaha kufurahisha watu/kuadaa watu – Unapokuwa na utayari wa kusaidia watu furaha hii ninayoiongelea huzaliwa na kukua kadri unavyoendelea kusaidia watu katika nyanja mbalimbali. Naamini umekwisha wahi kukutana na watu unatamani usiondoke kwa jinsi anavyokuhudumia yaani anaonesha urafiki wa hali ya juu na huku akikuhudumia kwa tabasamu mubashara.
4. Ujuzi – Hakikisha unajinoa vya kutosha katika uwanja wako wa kujidai na ufanyapo kitu kifanye kwa ubora wa hali ya juu. Hiyo ndio iwe moto yako. Fanya kwa kadri ya uwezo wako wa juu kabisa acha ubabaishaji.
5. Maandalizi – Hakuna kitu muhimu katika maisha kama maandalizi ya kila kitu unachotegemea kukifanya.
- Humgharimu mtu muda kujiandaa, lakini ni bora mara mia kuliko kufanya vitu hovyohovyo. Kuna ukweli usemao katika kila dakika moja ya kupangilia unaokoa dakika 10 za utendaji. Andaa siku yako siku moja kabla, Jiandae kwa ajili ya kufundisha usikurupuke. Kufundisha pasipo maandalizi ni udanganyifu, Jiandae kufanikiwa maana wengine wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa tu hawana maandalizi. Ndio maana unaona mtu akiokota milioni mia moja anakuwa kichaa kwa kuwa hakuwa na maandallizi ya kushika milioni mia moja na hajui afanyie nini. JIANDAE.
- Jiandae juu ya kile unachotarajia kukifanya.
- Kumbuka siku zote maisha hukupa kile unachostahili na sio unachotamani. Sasa huna maandalizi ya mafanikio kwa nini upewe. Wewe hustahili bali unatamani.
6. Kujitegemea – Jiangalie kwanza wewe mwenyewe. Acha kuwa mtegemezi. Jifunze juzi mbali mbali kukuza kujitegea kwako. Jaza mapungufu yako ili uzidi kujitegemea Zaidi. Wajibika acha ubabaishaji. Kamwe usimlalamikie mtu yeyote. Ukitaka kujua mtu wa kumlalamikia ambaye ameyafanya maisha yako kuwa ya hovyo basi nenda kwenye kioo na utakayemwona ndiye pekee wa kumlalamikia. Acha kabisa ngonjera mara magufuri mara uchumi mbaya. Hakuna kitu kama hicho wewe ndio tatizo.
7. Taswira yako kwa Jamii – Unaonekanaje? Je umekaa kitapeli? Je unanyoa nywele kiasi cha kuonekana muhuni? Je unaonekana kama kiongozi? Je unaonekana kana kwamba ni mtu unayeyadhibiti maisha yako? Unavaaje – kama mwenye mafanikio? Unaongeaje? Unafikirije? Je ni mtu mwenye kupenda kujifunza? Mwonekano wako ni muhimu sana kwa jamii. Moja ya mambo ambayo watu hujali ni pamoja na kuwa na kioo nyumbani kwako ili kabla ya kutoka lazima ujikague. Maisha haya yaweza kukufanya ukatoka pasipo kuchana nywele na ukaonekana umechanganyikiwa. Lakini pia viatu vyako viwe vinang’a bila kusahau mkanda mzuri kwa akina baba na mengine mengi. Mwanadada unavaaje? Je vimini? Vaa kwa staa acha kujikwatua kupindukia kwani utaonekana kituko. UNAONEKANAJE KATIKA UJUMLA WAKE? JITATHIMINI.
8. TABIA – Ni bora niajiri mtu mwenye tabia njema kuliko mwenye ufaulu wa hali ya juu lakini mwenye tabia mbaya. Tabia ni kila kitu kwenye jamii. Je u mwadilifu, mwaminifu na mwenye kujiongeza katika utendaji wako. Je unafanya vitu sahihi kila wakati. Je kama hakuna mtu uko peke yako waweza kuendelea kufanya vitu sahihi. Au wewe ni tapeli, mjanjamjanja tu. Badilika, mafanikio huwakimbilia wenye tabia njema.
9. Nidhamu binafsi – Jua nafasi yako. Fanya yakupasayo bila kuahirisha wala visingizio
10. Uwezo wa kufanya vitu kupindukia – Acha kuwa mtu wa kawaida kawaida. Ukipewa kazi ifanye mpaka watu washangae maana unapitiliza. Kumbuka unapofanya kitu bila kujali ujira, nakuhakikishia ujira utakufuata. Mfano umeajiriwa kama messanger. Kuna wakati unakuwa huna cha kufanya nakushauri usikae chini fanya gardening, fagia, okota karatasi zilizozagaa nk. Fanya kupitiliza. Ikitokea wanataka kufukuza watu kazini wewe utaachwa maana u rasilimali lakini wengine ni mizigo. Ukitaka fedha nyingi yaani kuanzia 2,300,000,000,000 najua wengine hata kusoma hawawezi. Ni lazima kufanya Zaidi.

Maoni
Chapisha Maoni