Maisha ni neno moja lakini lenye mana nyingi unapoamua kumyambulisha maana yake. Kufikia malengo utakayo kuyafikia nayo ni maisha na hili ni eneo nitakaloliongelea kwa kina siku ya leo.
Kutamani uwe vile na hivi ni rahisi sana lakini kuchukua hatua ya kutenda ndilo eneo ambalo wengi hushindwa na kuishia kuona maisha hayana maana yoyote. Wanadamu wanatakiwa kujua ya kwamba kutenda ni muujiza unaojiridhisha kwa watu wenye uthubutu na hili linatuthibitishia kusahau kabisa kutamani kuwa kama fulani bila kuchukua hatua ya utendaji.
Kwa kawaida huwa nawashauri watu ya kuwa chochote unachotamani kuwa nacho, tayari wengine wanacho. Kwa hiyo njia rahisi ni kukutana na hao ambao tayari wanavyo ili upate kujua yakupasa kunya nini ili nawe uweze kupata. Hii inamaanisha ya kuwa unakuwa tayari kupitia maumivu yatakayokufikisha unapotamani kufika, au ukaishia hatua ambayo hukuitamani kuifikia kwa kutofanya yale uliyoelekezwa kufanya. Yote kwa yote wewe ndiye mwamuzi.
Ni sawa na nadharia ihusishayo habu na rimu ya tairi ya gari – Je unapenda kuwa habu, au rimu? Ili uwe habu inamaanisha uwe mtu wa katikati Zaidi, na kuwa rimu ni kuwa mbali na utendaji au nguvu ya kuzuzungusha. Ninaposisitiza juu ya umuhimu wa nguvu iliyopo katika kuzamia kitu (kuweka macho, akili, nguvu kwenye kitu kimoja tu hata mtu akikuita inakuwa ngumu kumsikiliza kutokana na kuzama katika jambo moja), hii ni namna ya kulitazama suala zima la kuwa habu. Hivyo kung’ang’ana katikati kama habu ndicho kitu muhimu katka maisha yako, ndicho kitakachokutafautisha kati ya kuwa habu au rimu
Endelea kutafakari juu ya utendaji wa habu ili nawe katika maisha ujiweke kwenye nafasi ya habu na kitakachofuata ni maisha yako kuwa bora Zaidi.

Maoni
Chapisha Maoni