Maisha ni neno moja lakini lenye mana nyingi unapoamua kumyambulisha maana yake. Kufikia malengo utakayo kuyafikia nayo ni maisha na hili ni eneo nitakaloliongelea kwa kina siku ya leo.
Kutamani uwe vile na hivi ni rahisi sana lakini kuchukua hatua ya kutenda ndilo eneo ambalo wengi hushindwa na kuishia kuona maisha hayana maana yoyote. Wanadamu wanatakiwa kujua ya kwamba kutenda ni muujiza unaojiridhisha kwa watu wenye uthubutu na hili linatuthibitishia kusahau kabisa kutamani kuwa kama fulani bila kuchukua hatua ya utendaji.
Kwa kawaida huwa nawashauri watu ya kuwa chochote unachotamani kuwa nacho, tayari wengine wanacho. Kwa hiyo njia rahisi ni kukutana na hao ambao tayari wanavyo ili upate kujua yakupasa kunya nini ili nawe uweze kupata. Hii inamaanisha ya kuwa unakuwa tayari kupitia maumivu yatakayokufikisha unapotamani kufika, au ukaishia hatua ambayo hukuitamani kuifikia kwa kutofanya yale uliyoelekezwa kufanya. Yote kwa yote wewe ndiye mwamuzi.
Ni sawa na nadharia ihusishayo habu na rimu ya tairi ya gari – Je unapenda kuwa habu, au rimu? Ili uwe habu inamaanisha uwe mtu wa katikati Zaidi, na kuwa rimu ni kuwa mbali na utendaji au nguvu ya kuzuzungusha. Ninaposisitiza juu ya umuhimu wa nguvu iliyopo katika kuzamia kitu (kuweka macho, akili, nguvu kwenye kitu kimoja tu hata mtu akikuita inakuwa ngumu kumsikiliza kutokana na kuzama katika jambo moja), hii ni namna ya kulitazama suala zima la kuwa habu. Hivyo kung’ang’ana katikati kama habu ndicho kitu muhimu katka maisha yako, ndicho kitakachokutafautisha kati ya kuwa habu au rimu
Endelea kutafakari juu ya utendaji wa habu ili nawe katika maisha ujiweke kwenye nafasi ya habu na kitakachofuata ni maisha yako kuwa bora Zaidi.
Ni mimi mwalimu wako Seth Simon Mwakitalu 0754 441325/0714 051 174/0788 493 836 au barua pepe ssmwakitalu2013@gmail.com
Kwa wale wote wenye kuhitaji kujifunza Zaidi waweza wasiliana nami ili kujumuika na wengine ambao hupata kujifunza kwa pamoja kupitia kundi la watsApp lijulikanalo kwa jina la KARAKANA YA UBONGO.
Kujiunga na kundi hili ni lazima ufanyiwe udahili/interview ili kuona kama unafaa au la. Hatuhitaji utuletee virusi katika kundi. Nakutakia siku njema yenye mafanikio tele. Kwa heri.

Maoni
Chapisha Maoni