Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Umasikini Ni Dhana Iliyojengeka Kwenye Ubongo

Umasikini ni dhana iliyojengeka kwenye ubongo na kamwe usije ukatafsiri ati umasikini ni ukosefu wa vitu vionekanavyo kwa macho kama kutokuwa na gari, nyumba, chakula na kadahalika. Mtu hufikia hatua ya kuwa masikini ni pale yeye mwenyewe anapoamini ya kuwa yeye  ni masikini (Kifupi amepofuka macho na haoni chochote anachoweza kukifanya nikimaanisha japo anaishi tayari ni maiti anangojea kuzikwa tu).

Imani hujenga mtiririko wa mawazo na mtiririko wa mawazo husababisha matendo mfanano (paralysed no more actions) na hatimaye hayo matendo humfikisha mtu kituoni anapostahili (kujihalalishia ya kuwa yeye ni masikini) ambapo sasa Imani hukomaa kama zilivyo dini tuziitazo siasa kali yaani mtu haambiliki, aminicho ndicho hupenda kumsikia kila mtu akubaliane nacho vinginevyo wewe unakuwa adui.

Zingatia kanuni hii: Imani>Mawazo>Matendo>Kituo>Imani kali>Mawazo>Matendo>Kituo…huenda ikijirudia (Repeat circle).

Wewe hauko vile ujifikirivyo, uko hivyo ulivyo kutokana na mfumo wa kiimani yaani umejiaminisha wewe ni masikini kwa mfano. Mtu waweza jiwazia ya kuwa huna maana mbele ya watu huku ukijieleza kwa hakika ya kuwa huna maana; lakini ukweli wa mambo ni huu – Chanzo cha kufikia hapo alipo hadi kujiita hana maana kilianza na mawazo (Kujiona hana maana). Ukweli hakuna mwanadamu mwenzako awezaye kukufanya wewe huna maana bila kibali chako.

Haitakuja tokea ukamwamrisha mtu anayejiona hana maana kumshauri  aache kufanya hivyo, isipokuwa matumaini ya kubadilika ni mpaka pale yeye mwenyewe atakapoamua kubadili Imani aliyonayo ambayo sasa itasababisha kubadilika kwa utitiri wa mawazo yaliyojijenga kwenye ubongo, kisha ataanza na Imani ya kujiamini na kujiona yeye ni wa maana na hatimaye uzoefu aliokuwa nao mwanzoni kubadilika kabisa.

Utajiri na umasikini vyote havitofautiani kwani chanzo chake ni kimoja - Imani. Mtu hawi tajiri kwa sababu ya kuwa tajiri bali mtu huwa tajiri kwa sababu ya Imani aliyoijenga ambayo sasa imezaa yeye kuwa tajiri. Kimsingi mawazo ya utajiri yakijikita sana kwenye ubongo ni sawa na mimba iliyokomaa yaani mtoto ni lazima azaliwe iwe kwa njia ya kawaida au oparesheni lazima mtoto azaliwe. Siri ni hiyo tu. Ndio maana nawashauri achaneni na TVs na Magazeti yanawacheleweshea kukomaza mimba kwani ubongo unakuwa na mambo mchanganyiko labda kama unaangalia vipindi vinavyoelezea wewe kutajirika au unasoma magazeti yanayoelezea wewe kutajirika. Hapa kazi ni moja tu kujishibisha taarifa lukuki za masuala ya kutajirika. Kwa kufanya hivyo lazima utakuwa tajiri hakuna njia ya mkato.

Hebu zijue tabia za watu walio na Imani iliyojengeka ya kuwa wao ni masikini:-
  1. Hawajiamini. Hofu zimewajaa wakitaka kufanya kitu. Kamwe hawako tayari kutumia fedha zao kwa fursa zinazojitokeza kwani kila wakati huwaza kupoteza fedha. Sawa sawa na yule mtumwa aliyepewa talanta moja na kuamua asiifanyie kazi na busara yake kumtuma aifukie.

  1. Kamwe mtu mwenye Imani kali ya kuwa yeye ni masikini hawezi kabisa kufanya maamuzi ya kufikiri ya kwamba hapa piga ua lazima nile bingo. Hujitahidi kwa hali na mali kukwepa kupata hasara kwa gharama yoyote ile japo ni mabingwa wa kucheza bahati nasibu lakini kamwe hawawezi wekeza katika bishara ya kumzalishia.

  1. Huamini ya kuwa kama Mungu aliwapangia kutajirika watatajirika tu bila kujali maamuzi na matendo yao ya kila siku.

  1. Wanasubiria fursa ziwafuate na kuwashika mkono kwamba hapa piga ua utatajirika badala ya kuthubutu juu ya fursa mbalimbali zinazokuja na kutoweka. Mara nyingi fursa zinapojitokeza huwa hawazioni hata ungewaambia kwa kutoa machozi.

  1. Siku zote hutafuta njia za mkato. Ukimwambia njoo huku kuna dili, hapo atachangamka. Ukimwambia hapa ukiweka 50,000 utapata 1,000,000 lazima atoe hiyo hela. Na ndio maana masikini wengi walididimizwa na DECI. Pole kama na wewe ni mmojawapo, ila sasa lazima upone. Achana na pesa za haraka haraka (NO FREE LUNCH, NO SWEET WITHOUT SWEAT).

  1. Maisha yao hayaoneshi kujijali na kumjali Mungu na ndicho kichocheo cha wao kushindwa kabisa kujitahidi kuchunguza, kuwekeza, na kujishughulisha na fursa mbalimbali na kwa kufanya hivyo wanashindwa kuona mawazo mazuri Mungu awapayo ili kufanikiwa. Inasikitisha sana hata vipaji walivyozaliwa navyo hawavioni.

  1. Ni watu wa kujihurumia sana. Hawataki maumivu ya aina yoyote. Chochote kitakachowataabisha huachana nacho mara moja. Kumbuka ya kuwa madini yote ni lazima upambane na mwamba kuuvunja ndipo ufurahie maisha, lakini kwao hilo halina nafasi.

Naomba nimalizie  kwa kukuuliza swali na ulijibu hapa kwenye kundi .Mawazo gani yanaendelea kujengeka kwenye ubongo wako? Je una mawazo yaliyojengeka mithili ya dini yenye siasa kali ya kuwa wewe ni masikini? Au wewe ni unajijengea mawazo ya kuelekea kwenye kutajirika kama ambavyo Mungu amenuia kwa kila mwanadamu?
Kumbuka siku zote utajiri ni urith uliopewa na baba yako wa Mungu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...