Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Unaamini nini?

Mtu akisikia maongezi juu ya Imani haraka kinachokuja akilini ni masuala ya kiimani. Lakini mimi natataka kutabainisha mambo makubwa mawili yaani Imani juu ya Mungu na Imani juu yako wewe mwenyewe.
Imani hizi mbili zina umuhimu mkubwa sana katika maisha. Ukweli ni kwamba usipomtanguliza Mungu katika shughuli zako au kama huamini kwamba Mungu yupo basi nisikufiche uko mahali pabaya. Mungu ni nambari moja katika kila shughuli tufanyazo. Mimi naamini hivyo.
Nisingependa sana kujikita juu ya Imani juu ya Mungu kwani tu watu wa dini mbalimbali lakii yatosha kusema twawajibika kumtanguliza Mungu katika shughuli zetu.
Sasa kikubwa ambacho nitaongelea kwa kina ni Imani iliyojengeka ndani yako tangu kuzaliwa hadi kufikia hapo ulipo.
Imani huanza kwa kusikizishwa na kisha kuanza kujijengea mfumo ninaouita mfumo wa kiimani katika maeneo yafuatayo:-
1. Philosofia – mfumo ukuongozao kutenda mambo. Ni vyema ukajua mambo yanayokuongoza katika maisha.
2. Maono – Kimsingi mtu huona kwa kutumia macho ya aina mbili, aina ya kwanza ni haya macho ambayo kila mtu anauwezo kumwangalia mwenzake na kumwamia macho yako mekundu na kadhalika lakini pia kuna kuona kwa kutumia ubongo na huku ndiko tunaita maono kwani hukupa uwezo wa kuona mbali sana.
3. Utambulisho (Identity) – Wewe ni nani? Kama huwezi kujibu swali hili basi ni tatizo. Maana kila mtu ameletwa hapa duniani kwa kusudio maalum ambalo litakutofautisha na wengine. Lakini unajua kusudio lako la kuwepo hapa duniani? Kumbuka hukuletwa kupumuapumua tu na kisha kutoweka. La hasha bali liko kusudio maalum.
4. Malengo – Malengo yakoyla siku ni yapi? Wiki je? Mwezi Je? Robo Mwaka je? Mwaka je? Miaka mitano Je? Miaka kumi Je? Na kuendelea
Je katika maeneo hayo manne ni kitu gani kwa uhakika waweza kutuelezea ujuavyo na jinsi unavyotekeleza katika maisha yako ya kila siku. Ukiweza kutuelezea kwa uhakika eneo moja wapo unavyolitendea haki basi tutasema kwa uhakika mfumo wa Imani yako juu ya eneo hilo umejengeka vizuri.
Kama unajua wewe ni nani basi hakuna mtu wa kukuelezea kinyume na hata akikuelezea kinyume haitakusumbua kwa kuwa tayari wewe unajua ya kuwa wewe ni nani.
Hebu tujiulize swali moja ya kwamba kama tangu tulipozaliwa tungekuwa tunaambaiwa maneno kama ‘Mwanangu wewe una uwezo wa kufanya jambo lolota’. Ungeendelea kusemeshwa hivyo kila siku hadi kufikia umri huu unadhani maisha yako yangekua kama yalivyo sasa?
Kikubwa ni kwamba tumeaminishwa mambo ya hovyo na yametuathiri maana ndio yamejengeka ndani yetu na kuwa Imani. Kuna watu wameaminishwa pesa ni shetani. Kwa hiyo mtu wa jinsi hiyo ni rahisi kulefti kundi kama hili linalozungumzia pesa kwa kina maana kwake mtu huyo kuwa na pesa za kutosha hata kuanza kusaidia wengine ni ushetani wengine wanaita free mason.
Imani iliyojengeka ndani yako hatuna budi kuibomoa na kupandikiza Imani sahihi ambayo sasa itafanyika kuwa msukumo wa ndani wa kufanya vitu sahihi na kupokea matokeo sahihi.
Hivyo hali uliyonayo sasa, changamoto unazopitia na mengine mengi bado hayana uwezo wa kukuelezea mwisho wako ni upi. Wewe ni mtu wa ajabu sana kwani ndani yako kuna nguvu kuliko hata zile zinazofuliwa na transafomer za umeme. Una uwezo wa kubadili historia ya maisha yako.
Kuanza kwako na kumaliza kwako kwa jambo lolote kunategemea sana na kitu ninakiita ‘breaking point’ yaani mahali unapokutana na ugumu kiasi cha kuanza kusema shughuli hii ni ngumu na kuamua kuiacha.
Hapo sasa ni breaking point.
Watu wote waliofanikiwa wamekua wakikabiliana na ugumu lakini wakavumilia na hatimaye wakavuka ng’ambo ya pili. Kinyume chake wasiofanikiwa wakikutana na ugumu utawaona hao wana kimbia ati tutakata mtaji maana ndio Imani iliyojengeka.
Hali uliyo nayo kamwe haiwezi kubadilika mpaka pale utakapobadilisha eneo la wewe kusimama. Hivyo ukibadili eneo la kusimama hali ya maisha yako itakuwa bora mno. (You can not change the condition unless you change your position’.)
Wewe usijitambulishe kwa yale uliyoyafanya siku za nyuma. Yawezekana kabisa siku za nyuma uliboranga sana na leo kamwe huwezi kusema mimi ni wa hovyo siko tayari kufanya kitu kile. Amini bado unaishi chini ya uwezo wako na kilichopo ni kuutambua uwezo wako ambao pia ni mchakato ili uweze kujitambua. Moja ya michakato ni pamoja na kujitenga na watu hasi, Kujisomea vitabu, Kusikiliza video/Audio, kuhudhuria semina mbalimbali, kuwa na utaratibu wa kuongea na mtu mmoja mmoja aliyefanikiwa kila mwezi, na mengine mengi. Hayo yataanza kuonesha uwezo wako na polepole utaanza na kuweza kubadili maisha yako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...