Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Unakwenda wapi?

Mara nyingi unapokuwa umepewa maelezo ya eneo ambalo toka uzaliwe hujawahi kufika hakika utahitaji kupata namna itakayokuwezesha kufika huko utakako kwenda.
Ashukuriwe Mungu kwa ubunifu aliompa mwanadamu katika suala la kusaidiana kufika maeneo ya ugenini kwani kuna vitu mbali mbali vimsaidiavyo mwanadamu kuweza kufika aendako.

Nakumbuka mimi binafsi kwa mara yangu ya kwanza kwenda Marekani. Haikuwa jambo rahisi.

Ninaye rafiki aishie Marekani na familia yake kwa muda sasa. Hivyo tuliandikiana na kunipatia namba zake za simu akiwa marekani na za mke wake na simu za nyumbani ili tu kutengeneza mazingira ya kupokelewa kirahisi na nisipate usumbufu nchi za watu na tena nchi yenyewe marekani.

Nilimpatia details za ticket ambazo zilionesha hadi muda wa kuwasili Dallas. Simaanishi daladala maana vijana hamishi kusema mzee kateleza, hayo ni majina ya nchi za wenzetu. Eneo hilo liko TEXAS nchini Marekani.

Nakumbuka aliniuliza swali moja unapokuja uwe unaniambia ndege unayokuja nayo maana kuna eneo najua utabadilisha ndege maana ticketi yako siyo ya moja kwa moja. Nikamwambia nimekuelewa.

Safari ilianza uwanja wa Mwalimu Nyerere kwa kupanda Emirate hadi Dubai na kubadilishiwa ndege. Hapo tulipanda ndege ijulikanayo kwa jina la Air Bus, Si wakati wake kuelezea mambo ya ndege lakini nilijifunza mengi.

Ndege hiyo ilitufikisha New York ambapo napo tulibadilisha ndege na kupanda AA (American Airways) ingekuwa bongo basi ni Air Tanzania, hizi ni kama daladala hapa kwetu maana kila baada ya muda mfupi zinaruka yaani ziko nyingi mno.

Amerikan Airways ni ndege ya ndani na mimi nilimtaarifu mwenyeji wangu ya kuwa ndio tumebadili ndege hapa Dubai naja moja kwa moja tafadhali nipokee.

Naye hakufanya ajizi aliwasili airpot pale Dallas lakini upande wa international airpot sio local airpot.

Hapo ndipo ngoma ya kinyakyusa ilipoanza. Marekani kubadili ndege kwenda upande wa local flight inabidi upande treni kwani kuna utofauti wa umbali kati ya local na international flights.

Rafiki yangu alichanganyikiwa maana hakuniona name sikuwa na simu kwani hata Dubai nilitumia call box. Akili ilichoka hata kujiongeza nikawa nimeshindwa. Nikabaki najisemea Kyala Ndula (Mungu nisaidie).

Rafiki alirudi nyumbani kwake baada ya kukaa sana airpot na kutomuona mgeni wake.

Usiombe kupotea ugenini tena Marekani utajuta kuzaliwa.

Baadaye sana kama baada ya masaa 8 kupita ndipo nikapata wazo la kuuliza huduma ya simu na kuoneshwa.

Nilipompigia alikuja mara moja na tulilia kilio cha furaha maana du. Acha niishie hapa.

UNAKWENDA WAPI?

Compas, Vibao barabarani, Simu, Ramani ya jinsi ya kufika maeneo mbalimbali, Kuuliza watu, Kwenda kituo cha polisi na mengine mengi husaidia mtu kufika aendako.

Sasa mimi leo nitaongelea ubao wenye alama ya kukuelekeza kwenye maisha ya ndoto zako.
Ubao wenye alama ioneshayo eneo fulani liliko kwa kamshale kaoneshako uelekeo husaidia kwa wageni kuelekea waendako.
Mara nyingi mbao za jinsi hii uwekwa njia ya panda. Lakini pia maeneo hayo huwepo pia na vibao vyenye kukuonya labda juu ya spidi au kuwataadharisha waendesha baiskeli na au wanyama baada ya umbali kidogo hivyo unataadharishwa kupunguza mwendo zaidi.

Sasa chukulia unaendesha gari katika mji  usio na sheria za barabarani, na ni ruksa kuendesha upande wowote na mbaya zaidi hakuna vibao vya kukupa maelezo wala alama za barabarani  isitoshe mji wenyewe una pilikapilika za magari mara upigiwe honi tena ile kali mara utukanwe ati mzembe yaani kila aina ya adha na wakati mwingine mtu huja mpaka kwenye gari yako na kukutolea maneno makali. Madereva wenzangu mnajua ninachoongelea Na kila ukiangalia unaona barabara zina magari mengi kupindukia, mara nao waendesha baiskeli wamo utafikiri msafara wa mamba maana kenge hawaishi kujihudhurisha, bodaboda bila kumsahau mjomba ake bajaji – Je utajisikia salama katika hali ya mazingira hayo?

Je, Una nafasi gani uliyonayo katika hali kama hii kufika eneo uendalo ukiwa na uhakika wa usalama wako?
Hebu fikiria tena ya kuwa unaendesha gari katika mji wa ugenini na ghafla unajikuta umefika kwenye makutano ya barabara nne lakini hakuna vibao vya maelekezo ya wapi sasa uende na kibaya Zaidi huna GPS (Navigation Equipment in your car)… kuchanganyikiwa ndio kitu pekee kitakachokuwa kikiendelea kwenye ubongo wako.
Haitoshi kuendesha kwa usalama/uangalifu, yakupasa pia uendeshe kwa kuelekea muelekeo sahihi. Hii ndiyo sababu haswa ya kwa nini tuna vibao barabarani na pia alama za barabarani.

Sheria za barabarani, alama za barabarani na vipao vyenye maelekezo ya kukuelekeza uendako viko ili kukupa amri (Instruct), kukuongoza, na pia kukuonya kwa watumiaji wote wa barabara - vyote vikiwa na lengo kuu moja ambalo ni ulinzi na usalama. Yote hayo ni kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji wote wa barabara kuweza kufikia maeneo waliyokusudia wakiwa salama

Tunapokuwa safarini katika maisha yetu kuelekea kwenye vituo vyetu yaani maisha ya ndoto zetu, kuishi maisha kama ambavyo tungependa kuishi – na haya maisha ambayo tungependa kuyaishi, kwa kupitia njia ambayo muumba (kwa wengine dunia) ina alama zake na kibao murua chenye kuonesha uelekeako kwa kila mwanadamu yaani hata wewe usomaye ujumbe huu ili tuweze jishughulisha kama ulivyo mwongozo na kutuhakikishia usalama wa kuhakikisha tunafika tulikokusudiwa.

Ukishindwa kusoma, pia kuelewa na kujishikamanisha kwa kuwa na maisha ya kufuata alama na mshale ukuongozao kitakachozaliwa ni utachelewa kufika kwenye kituo chako au utaishia kwenye kituo ambacho hukukusudia.
Ninachokijua ya kuwa ndio alama ya barabara ya kutupeleka kila mmoja kwenye kituao chake yaani maisha ya ndoto yako kwa bahati nzuri mwenyezi Mungu mwenye kutupa ndoto na pia ametuwekea vibao vitatu na kila kimoja kina alama yake navyo ni AMANI, FURAHA, NA TATU NI UWEZO WA KUZALISHA/KUGAWA ULIVYOVIPATA KWA KUWA MTII KUFUATA ALAMA. (GIVING BACK TO COMMUNITY WHICH IS  AN ULTIMATE GOAL FOR EVERY HUMAN BEING)  kwa kifupi nikitumia lugha ya wenzetu ni sawa na kusema vibao hivyo ni PHD – Peace, Happiness, Delivery.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...