Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Acha Kuchota Maji Baharini Kwa Kutumia Kijiko.

HERI YA MWAKA MPYA.
Jambo moja unalotakiwa kulijua ni kwamba hakuna uhaba wa mafanikio.
Hivyo unapopanga kufanikiwa usiwe na mawazo ya uchache. Kanuni nzuri ya kupangilia malengo yako ni kuorodhesha uvitakavyo pasipo kuwazia kwamba pesa ni kikwazo.
Jiulize kama pesa isingalikuwa tatizo, je nini unatamani uwe navyo. Hakikisha unaorodhesha matamanio yako yote bila kujali vipaumbele. Kazi yako ni kutiririka tu.
Nitafurahi orodha ikifikia angalau 100 au kuzidi lakini isiwe chini ya 100. Ukiona unapata orodha chini ya 100 tafsiri yake wewe ni mvivu wa kufikiri. Yaani ainisha maisha yako uyatakavyo na acha kabisa kuwaza kwamba pesa ni kikwazo. Hii ni hatua muhimu sana na ningefurahi kama kila mmoja wetu angalifanya.
Hatua ya pili, anza kupitia kimoja baada ya kingine kwa kuandika tarakimu mbele yake. Yaani mfano umeandika nyumba (3) maana yake unataka uwe na nyumba baada ya miaka mitatu, labda Gari (1) ndani ya mwaka mmoja ( Hapa ni chochote kuanzia mwezi mmoja hadi 12 unaandika 1) na fanya hivyo kwa kupitia orodha yote.
Hatua ya tatu inayo fuata ni kuweka pamoja vitu vya kuwa navyo ndani ya mwaka mmoja (Orodha hii ni muhimu sana maana ndiyo inayokujengea kujiamini), miwili ….20 na kuendelea.
Hatua ya nne anza kuelezea kwa ufasaha ulichoorodhesha kwa kila ulichoorodhesha. Mfano nyumba (nyumba ya ukubwa wa mita ishirini kwa ishirini, iwe na ghorofa moja, chini iwe na parking ya magari matatu aina ya V8, garage, choo na bafu kwa wote, sitting room ya kuenea watu ishirini kwa wakati mmoja, chumba cha ibada kutosheleza watu 50 kwa wakati mmoja, sitting room maalum kuongelea masuala yenye unyeti wa kutokutaka wengine wasikie na kadhalika)
Kikubwa unaweka katika maandishi kitu katika uhalisia kinavyotakiwa kuwa. Kwa habari ya nyumba hakikisha unaongea na msanifu majengo utakacho na akiweke kwenye mchoro na baadaye picha ya muonekano kwa kila upande. Kikubwa unaendelea kuanisha kwa kutumia njia ya kujiuliza swali kila wakati nini nimesahau kuanisha, kila wakati na utaona ufahamu unazidi kutiririrka na usijisikie kuchoka mpaka ufike maahali umeishiwa kabisa kuainisha.
Ukifikia hatua hiyo basi unatakiwa utaje na tarehe, siku na mwaka wa kumiliki hiyo nyumba. Nakushauri pitia somo la nyuma linaloelezea SMART GOALS. Utapata ufahamu wa kutosha.
Kitendo hichi ni muhimu sana.
Kimsingi tuna makundi matatu ya malengo:
1. Uchumi (Pesa, biashara, uzalishaji)
2. Vitu – Hapa ni kila kitu unachotamani kuwa nacho iwe ni vidogo au vikubwa
3. Kujiendeleza (Personal Development) – Ili uweze kuwa imara (Mental toughness), kuwa na maamuzi sahihi, kuwa kiongozi, na mengine mengi)
Kanuni ya kuyafikia malengo yako:
1. Hakikisha malengo yote yameandikwa na kupangiliwa.
a. Pata muda kila siku kuyapitia pitia na itapendeza kama utayafanyia tafsiri ya picha. Mfano kama una ubao wako chumbani wa kubandika picha mbalimbali mfano aina ya gari unayoitamani kuimiliki. Utapopitia asubuhi kabla ya kuanza shughuli na usiku kabla ya kulala utakuwa unaisaidia akili kuweza kutafsiri kwa haraka na kukutengenezea matendo ya kuelekea kupata hicho kinachoonekana kwa njia ya picha.
Kwa nini picha. Akili zetu huelewa haraka sana picha kuliko namna nyingine yoyote ile. Hivyo tumia picha kadri uwezavyo.
b. Mipango Mkakati - Watu wengi huishi kwa matumaini ya kuwa siku moja maisha yatakuwa bora (One day Yes). Naomba usidanganyike, hupati maisha bora kwa matumaini bali kwa kuwa na mipango mkakati na yenye kutekelezeka.
2. Fanyia kazi malengo yako. Jasho ni Lazima. Hakuna vitamu kuvipata pasipo kutokwa na jasho (There is no sweet without sweat).
Hakikisha unapofanikisha lengo lolote bila kujali udogo au ukubwa wake ni lazima ujipongeze kwa kusherehekea. Waweza jipa outing kama ishara ya kukamilisha lengo.
Naomba usipuuzie hili. Ikiwezekana kila lengo liwekee na aina ya usherekeaji wake ukitimiza. Hili litakusaidia kuamsha hamasa ya kulifikia kwa haraka.
Kusherehekea kutimiza lengo ni ishara mojawapo ya ukomavu.
Kumbuka: Waweza mnyima mtoto mkate na ukweli ni kwamba hatakufa; Lakini maisha pasipo ndoto/malengo utakufa. Ni lazima kuendelea kuota/kuwa na malengo kila wakati.
Weka mikakati na ingia kazini. Ukishindwa kupangilia mambo ya kufanya kufikia malengo maana yake umepanga kushindwa kufikia malengo yako (If yo do not plan, you plan to fail).
ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2017 INAISHIA NA 2018 INAINGIA. HIZO NI NAMBA TU NA HAZINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.
NAWATAKIA KHERI NA BARAKA KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA.
SEE YOU TO THE TOP WHERE IS NOT CROWDED.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...