Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Fanya Kazi Ya Daraja La Kwanza (Do A First Class Job)

Fanya Kazi Ya Daraja La Kwanza (Do A First Class Job)
Sasa natambua ya kwamba una kila kitu kikupasacho kushinda na unashinda na sikuzote utakuwa mshindi.
ONYO: Kamwe usikubali hukumu za watu wa kawaida kwani wewe si mtu wa kawaida.
Kumbuka:
1. Kujiweka katika nafasi ya watu muhimu inakusaidia kufikiri vitu muhimu
2. Fikiri ya kuwa kazi yako ni ya muhimu
3. Jikumbushe kila unapopata fursa ya kufanya hivyo ya kwamba wewe ni mtu wa daraja la kwanza.
4. Katika nyakati zozote za kimaisha , jiulize ‘Hivi ndivyo mtu muhimu anavyofikiri’ Kisha heshimu jibu utakalolipata.
U matokeo ya mazingira yako.
Fanya kuwa sheria juu ya kutafuta ushauri kutoka kwa watu wanaojua kukuzidi. Hii itakusaidia sana kubaki daraja la kwanza.
Watu hukupima kwa kuangalia ubora.
Fanyia mazoezi kuwa mtu wa viwango kwa kila ufanyacho kigezo kibaki ubora wa hali ya juu mpaka ifike mahali iwe sehemu ya maisha yako na kila mtu akikuona aseme huyu ni mtu wa viwango. Acha kabisa kukubaliana na vitu chini ya viwango.
Linapokuja suala la kuwaongelea watu, tafadhali ongelea mambo chanya tu yaa watu na si vinginevyo, maana hivyo ndivyo watu wa daraja la kwanza hufanya.
Kwa kila kitu ufanyacho hakikisha unailinda nafasi yako ya daraja la kwanza.
Jana wakati nataka kupanda daladala kuna kundi la watu lilijitokeza kuvamia mlango ili kuwahi viti. Mimi kwa kuwa najijua ni wa daraja la kwanza nikajitenga na hiyo purukushani na ilipoisha ndipo name nikaingia taratibu.
Inalipa kuijua nafasi yakao katika haya maisha. Tafadhali chagua kuwa mtu wa daraja la kwanza na hivyo hivyo matendo yako yakuelezee ya kwamba u mtu wa daraja la kwanza. Utafikia hatua kamwe hutaweza kuwa vinginevyo.
Kifupi namshukuru Mungu sana kwa huduma hii ya kufundisha na kuna mengi mazuri yanakuja.
Nikuombe kitu kimoja ‘KIZURI KULA NA MWENZAKO’. Naamini hukosi watu kumi wa kuwaelezea kinachoendelea karakana ya ubongo na pia usiache kuwaelezea masharti yaliyopo.
Wakikuelewa basi waadd maana u admin pia, huhitaji kunisubiria uniambie.
PAMOJA TUNAWEZA KUWA CHACHU YA MABADILIKO.
FANYIA MAZOEZI YA KUJIKUBALI NA KAMWE USIRUHUSU KUTOJIKUBALI KWANI KWA KUFANYA HIVYO UTAKUWA UNAJIADHIBU.
Weka mikakati na ingia kazini. Ukishindwa kupangilia mambo ya kufanya kufikia malengo maana yake umepanga kushindwa kufikia malengo yako (If yo do not plan, you plan to fail).
ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2018 NDIO IMEANZA. HIYO NI NAMBA TU NA HAINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.
NAWATAKIA KHERI NA BARAKA TELE KATIKA YA MWAKA 2018.
SEE YOU TO THE TOP WHERE IS NOT CROWDED.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...