Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mazingaombwe ni sehemu ya Maisha! Chagua yale yenye Manufaa kwako.

Wana Karakana ya Ubongo!
Jana niliongelea jambo moja kuhusu namna ya kusoma akili za watu kwa kutumia kitu nilichokiita mazingaombwe.
Kuna siri kubwa ndani ya kufanya mazingaombwe. Pia unahitaji ujuzi wa hali ya juu. Kwa maana hiyo wale wanaoifanya kazi hiyo hutumia muda mwingi sana kujifunza.
Huwezi kukurupuka na kujua siri hizo kwa siku moja. Siku hizi kuna Talk za Shows ambazo zinaonyesha siri za matukio mbalimbali ya mazingaombwe.
Hata watoto kwenye baadhi ya mashule wanafundishwa mbinu ndogo ndogo kwa njia ya Hesabu, sarafu na karata.
Mfano wanafundishwa namna ya kufanya sarafu itokomee kusikojulikana na pia ikaonekanie mahali pengine. Ni aina ya burudani kama hujui siri ya kinachofanyika.
Pia wanatumia karata kusoma ubongo wa mtu kumwambia karata aliyofikiria kwenye akili yake. Kuna wakati kama mtu sio mzoefu anaweza kukosea. Kwa hiyo unatakiwa umakini mkubwa.
Kwenye moja ya Talk shows, kuna mwana mazingaombwe mmoja ambaye anafanya mazingaombwe yake halafu anaonyesha mbinu zilizotumika ambazo wewe huzijui ili uelewe kilichoendelea.
Kuna rafiki yangu anatumia moja ya hizi Talk Shows kufanyia ubongo wake mazoezi. Akishaangalia mchezo mmoja. Anaamua kufikiria na kufanya ubongo wake uzionyeshe hizo siri kabla hajaziangalia. Lazima use na TV maalum inayoitwa TiVo ili usimamishe (pause) kwanza halafu ndo ukisharidhika uendelee. Aliniambia, amejikuta Mara nyingi anapatia kwa asilimia sabini. Hiyo ni maksi nzuri.
Kuna raha fulani unayoweza kuipata na pia kukuza ubongo wako unapoufanyia mazoezi. Hebu jaribu kufikiria Wazi la Leo litamalizia kwa kutaja Tarehe ngapi ni muhimu January 2018?
Bila shaka mazingaombwe yako yatakufikirisha kitu ambacho umekiona kwa namna moja au nyingine ulichokisoma.
Kujijengea tabia ya kusoma na kutafakari ulichokisoma inakomaza ubongo wako kukupa uwezo wa kufikiria na kutengua vitendawili, matatizo na pia majawabu ya vitu mbali mbali. Vyote hivyo unaweza kuvichukulia kama mazingaombwe.
Jenga tabia unapoona mtu anafanya kitu unachopenda kwa mfano kuendesha Farasi, penda kujifunza kwa kutumia akili kwanza. Je, unaweza kuruka kamba bila kamba? Hilo ni zoezi lenye ufanisi zaidi ya asilimia 70 ukilinganisha na kutumia kamba. Huoni hilo ni sehemu ya mazingaombwe unayoweza kufanya?
Fikiria zoezi gani jingine unaloweza kufanya likawa kama mazingaombwe?
Kama uko Dar unajua mazingaombwe unayoweza kufanya na Kocha wako kuanzia pale nje ya Geti la Muhimbili Tarehe 28 January kuanzia saa 8 mchana.
Kwa wale walioko mikoani, unaweza kumdhamini mtu mmoja au zaidi kupata T-shirt au Kofia.
Ni kwa jinsi unavyosoma na kujituma kwa kuyafanyia kazi haya nimekufundisha ndo utaanza kujishangaa mwenyewe jinsi ambavyo fursa mbalimbali zitaanza kujionyesha kwako.
Kuna wakati nilikuwa ninajiuliza nitaanza je kuwa Kocha? Nikaanza kichwani na hatimaye nikakutana na resources mbalimbali na wewe ukiwepo pia.
Huhitaji kusoma Vitabu vyenye maarifa ya Kujiongeza au Mazingaombwe ya namna hii ili uweze kufanya kitu, utajikuta unakutana na ajali njema kutoka kila upande wa maisha yako.
Hapa nataka kusisitiza kitu, ninachokisema siyo muujiza bali ni yale maandalizi unayoyafanya siku hadi siku.
Kuanzia Leo hakikisha unafanya mazingaombwe kabla ya kulala.
Panda kitandani baada ya kuhakikisha ubongo wako umeongezeka maarifa zaidi ya jana yake. Inawezekana. Akili ya Mwandishi Lameck Hulilo ambaye nimeona Vitabu vyake viwili humu ndani. Inawezekana Namba 1 na 2. Vitafute hivi vitabu vitakupa dopamine nzuri ya kuboresha mazingaombwe ya Ubongo wako.
Kuna faida na hasara za kutumia mazingaombwe yanayotumia akili zetu.
Nitawashirikisha kwa picha au video aina ya mazingaombwe yasiyofaa na ni wajibu wetu kufanya ukaguzi na kuyakimbia mawazo yenye kuleta aina hiyo ya mazingaombwe.
Hebu jipime ni mazingaombwe ya aina gani umeshajijengea uwezo wa kuyatenda.
Kwa malengo yako ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu, unajipima je kama uko njia sahihi?
Tuanze kwa kutumia magari mapya ya kisasa. Gari yetu Karakana ya Ubongo ni sehemu ya kushirikishana mazingaombwe yenye dopamine ya manufaa.
Tarehe 28.01.2018 tutafanya jaribio dogo la kuona namna ya kujifanyia mapinduzi.
Sina shaka hiyo Tarehe umeiona hapo. Kuna mahali nilikuuliza swali awali. Je, ulipatia?
Kila mtu ana fursa ya kufanya kitu. Karibu sana. Leta mawazo yako! Yanaweza kuja hapa au hata inbox.
Mungu ni mwema.
Long live Karakana ya Ubongo.
Mungu atusaidie tunapoendelea kujifunza pamoja.
Nikuombe tena kitu kimoja ‘KIZURI KULA NA MWENZAKO’. Naamini hukosi watu kumi wa kuwaelezea kinachoendelea karakana ya ubongo na pia usiache kuwaelezea masharti yaliyopo.
Wakikuelewa basi waadd maana u admin pia, huhitaji kunisubiria uniambie.
PAMOJA TUNAWEZA KUWA CHACHU YA MABADILIKO.

Maoni

  1. je ili niweze kuhfanikiwa kufanya ivo njia nzuri ni ipi?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...