Mazingaombwe ya Bahari Mbili:
Wanakarakana ya Ubongo! Mwaka ni mpya bado. Leo ninaongelea mazingaombwe yanayotokea kwenye mazingira yanayotuzunguka.
Kuna Bahari mbili humu Duniani ambazo maji yake yanatokea Mto Jordan.
Bahari ya kwanza inaitwa "Dead Sea" kwa lugha ya wenzetu. Au Bahari Mfu kwa lugha yetu. Hii Bahari Mfu japo ni Bahari lakini imekaa kama Ziwa.
Inasemekana kwamba maji yake yana chumvi nyingi sana kiasi kwamba hakuna kiumbe chochote kile kinachoweza kuishi kwenye maji hayo. Hakuna cha Samaki wala Mamba wala Nyangumi, wala uhai mwingine wowote kama vile mimea ya Baharini vinavyoweza kustahimili hicho kiasi cha chumvi ya maji ya Bahari Mfu. Na ndo uhalisia wa hilo jina lake.
Wataalamu wanatuambia chumvi iliyomo ndani ya Bahari Mfu ni nyingi kiasi kwamba hata mwili wa binadamu unaelea kwa urahisi kabisa.
Kiwango cha hiyo chumvi ni mara kumi zaidi ya viwango vya chumvi vilivyomo kwenye maji ya Bahari nyingine unazozijua wewe.
Bahari nyingine inaitwa Galilee. Kwa bahati nzuri Bahari ya Galilee imo kaskazini mwa Bahari Mfu.
Cha ajabu na mazingaombwe yaliyoko hapo ni kwamba, Bahari zote mbili yaani Bahari ya Galilee na Bahari Mfu chanzo chake ni Mti Jordan. Lakini maji ya Bahari hizi mbili yana ladha tofauti kabisa. Tofauti kupita maelezo. Jiulize haya ni Mazingaombwe ya aina gani? Kuna siri gani?
Je, kuna uhusiano wowote na mazingaombwe yaliyoko kwenye maisha yetu? Hebu jiulize swali hapo? Chakachua akili yako uone kama majibu yetu yatafanana kabla ya kuendelea kusoma!
Fikiria kidogo hapa.
Bahari ya Galilee tofauti na mwenzake ina uhai na utajiri wa kila kitu kuanzia viumbe hai vya aina zote na pia mimea ya aina zote inayoota baharini.
Inasemekana Bahari ya Galilee kuna aina nyingi sana za samaki mbalimbali.
Sasa linganisha majawabu ya kufikiria kwako na haya mazingaombwe hapa:
Chanzo cha maji ya Bahari hizi ni kimoja, Mto Jordan. Bahari zote mbili ziko eneo moja, tena zinakaribiana. Lakini cha kushangaza Bahari moja inatoa baraka ya uhai kwa viumbe na mimea wakati nyingine ni mfu. Haina chochote, wala si lolote. Hoi inawezekana kivipi?
Hapa tujiulize siri ya aliyefanya haya mazingaombwe na kusababisha hii hali.
Nitakushirikisha video inayoongelea kuhusu kupokea na kutoa. Hata Bahari inayotoa inabarikiwa wakati ile isiyotoa kama Bahari Mfu inakufa.
Unakumbuka Tarehe 28 January 2018? Kuna mazingaombwe Kocha wako ninataka tufanye. Pia, kwa wewe uliye mbali unaweza kudhamini mtu kwa T-shirt au Kofia. Haijalishi umefanya au hujafanya lakini hiyo video itakuambia ni vitu gani watu wanajutia. Ni yale ambayo hatukuyafanya ndo mara nyingi tunayajutia tunapokuwa wazee au tunapokaribia kufa. Tutumie fursa tulizo nazo kufanya kitu. Na tuwe kama Bahari ya Galilee kwa wahitaji pale Muhimbili na kwingineko.
Nikufafanulie vizuri zaidi. Mazingaombwe ya hizi Bahari yako hivi:
Mto Jordan unapeleka maji yake kule Bahari ya Galilee na pia ile Bahari inaruhusu maji mengine yatoke kwenda sehemu nyingine. Kwa hiyo Bahari hii ya Galilee haipokei tu maji bali pia inatoa maji na kuruhusu yapite. Ni mlango wa maji ya Mto Jordan kupita. Kitendo cha maji ya Mto Jordan kupita pale kinaiacha Bahari ya Galilee ikiwa safi yenye afya kwa viumbe na mimea kuweza kuishi. Hilo ni zingaombwe la kwanza ambalo labda kama ulifikiria na kujiuliza hapo awali inawezekana tuko wote.
Je, zingaombwe la Bahari Mfu litakuwa je? Jiulize tena? Bila shaka hii Bahari inameza kila kitu. Hebu tuone! Hakuna utoaji. Ni kupokea tu.
Bahari Mfu imeponzwa na mazingira yaliyoizunguka. Haina mlango unaoruhusu maji ya Mto Jordan kutoka. Bahari Mfu inaishia kumeza kila kitu inachopokea. Haina pahali pa kutolea maji yanayokuja. Kinachotoendelea ni nguvu ya jua tu ndo inasababisha mvuke ambapo chumvi na taka taka nyingine zisizoweza kugeuka mvuke zinabaki na kusababisha Bahari kufa kama jina lake. Tuna Wataalamu wenye uwezo mkubwa na maarifa mengi. Ni kwa nini wameshindwa kujitolea kubadilisha hii Bahari na yenyewe iwe hai? Inatakiwa ianzie mahali.
Watu tunashindwa kufanya mazingaombwe ya kujitolea. Je, tunaweza kuanza na hili la Muhimbili? Tarehe ni 28 January 2018. Je, wewe unataka kuwa chumvi ya aina gani? Kama ni yenye manufaa fikiria, jianglie uone utafanya nini. Ukiamua kung’angania kile ulicho nacho utaishia kufunga hata milango ya vitu vingine kujileta kwenye maisha yako. Hapa ninaongea kama Kocha.
Hata kukaa na kuandika kitu kama hiki nimewekeza nguvu, akili na kutoa muda wangu pia. Sijazidisha chumvi ya kukuangamiza kwa sababu ninatumika. Mto Jordan ukiniletea maji ninatumia kiasi ninachohitaji na kuruhusu mengine kupita kwa ajili ya kubadili wengine.
Nikupe tahadhari, Bahari ya Galilee haina ubaguzi wa aina yoyote. Inagawa maji yake kwa kutumika kama mlango. Hiyo ndiyo siri ya haya mazingaombwe ya Bahari ya Galilee yanayosababisha itoe uhai kwa mimea na viumbe wa Baharini.
Dunia yetu ya leo ina ukame wa watu wa aina hii. Dunia yetu inahitaji watu wanaojitolea zaidi. Tunahitaji watu wanaotumika kuwa baraka kwa wengine. Kama Mungu anapitishia baraka kwako na ukaamua kuzishikilia utaishia kuwa chumvi.
Gari letu la Karakana ya Ubongo linataka kufika huko. Je, wewe una dhamira? Je, uko mahali sahihi? Dunia yetu inaanza kufa kwa ukosefu wa watu wanaojitoa. Fikiria, chukua hatua.
Maisha yetu:
Hebu jiulize! Je, maisha ni kujichukulia au kupokea tu?
Maisha yatakuwa na maana zaidi tukitoa hata kile kidogo ulicho nacho. Mfano nguo ambayo huivai tena. Kiatu ambacho huvai tena. Chochote cha aina hiyo.
Sote na tuige mfano wa Bahari ya Galilee. Tunayo bahati ya kujifunza na kupata utajiri wa maarifa, upendo na pia kusikilizana na kuheshimiana.
Ila usipojifunza kwa kitendo na kuwasaidia wenye uhitaji tutaishia mahali kama Bahari Mfu.
Mapenzi mema, heshima tulizo nazo na utajiri wa maarifa vitageuka kuwa mvuke kwa kuyeyushwa na jua. Masalia mengine yatabakia ndani mwetu kama tulivyoona mazingaombwe ya Bahari Mfu.
Kama tutaendelea kungangania mtizamo wa Bahari Mfu kwa kuendelea kumeza maji ya Mto Jordan na vingine vinavyokuja kwenye maisha yetu, matokeo yake yatakuwa ni mabaya sana. Hata kama tuna maarifa mengi kiasi gani.
Mazingira yanayotuzunguka siku zote yanasema kitu. Mazingira yanatuonyesha mazingaombwe kila siku. Huu mfano wa hizi Bahari unatosha kutushawishi tufanya kitu Tarehe 28.01.2018 ili tufungue milango ya Gari yetu Karakana ya Ubongo kufanikiwa mwaka wa 2018. Kazi kwetu.
Katika maisha yako binafsi, kuna Bahari, tengeneza milango ya maji kupita. Tengeneza utoaji wa baraka. Tengeneza matoleo ya kujenga kuta za nyumba za wengine wenye uhitaji.
Kuta za upendo, amani, furaha, raha na chochote kile unachokitamani katika maisha haya, weka mlango kimfikie mwenye uhitaji.
Hakikisha hupokei tu bali unatoa pia. Hapo kuna siri kubwa. Hapo nimekuonyesha kilichojificha ndani ya hayo mazingaombwe.
Fungulia mabomba yote ya maji yenye baraka ushuhudie mafuriko ya miujiza ndani ya Maisha yako
Jitengenezee hii tabia ya kuwa tap (kitasa cha bomba) badala ya kuwa top (kukaa juu). Hilo ndo zingaombwe langu la mwisho kwa Leo. Sit on the Tap rather than at the Top.
Kila mtu ana fursa ya kufanya kitu. Karibu sana. Leta mawazo yako! Yanaweza kuja hapa au hata inbox.
Mungu ni mwema.
Long live Karakana ya Ubongo.
Nikuombe tena kitu kimoja ‘KIZURI KULA NA MWENZAKO’. Naamini hukosi watu kumi wa kuwaelezea kinachoendelea karakana ya ubongo na pia usiache kuwaelezea masharti yaliyopo.
Wakikuelewa basi waadd maana u admin pia, huhitaji kunisubiria uniambie.
PAMOJA TUNAWEZA KUWA CHACHU YA MABADILIKO.

Maoni
Chapisha Maoni