Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mazingaombwe ya Kukopi na Kupesti

Mazingaombwe ya Kukopi na Kupesti Yanahitaji Ufanye Uchunguzi (Experiment).
Wewe uko wapi sasa?
Uko ndani ya Gari ipi?
Mdogo mdogo Gari ya Karakana ya Ubongo inasogea.
Hatuhitaji kujiongezea dopamine iliyo nje ya mwili ili upate stimu ya kusonga mbele.
Inawezekana kuwa mjanja bila dopamine ya vitu kama kulewa na madawa ya kulevya.
Watu wengi wenye magonjwa mbali mbali yanayosumbua sana wanahitaji kuacha kujiongezea dopamine kienyeji.
Tusipobadilika sisi wenyewe hakuna kitu chochote nje yetu kitakachodubadilisa. Hata ujiongezee dopamine kiasi gani.
Ni suala la kujijengea tabia stahiki kama vile kwenda kitandani kulala ukiwa vizuri zaidi ya jana yako (Go to bed smarter than yesterday).
Mwandishi maarufu wa Tanzania ambaye ameandika kitabu cha Kusudia Kuwa Wewe, Bwana Lameck A. Hulilo huwa anapendelea kusema:
‘Inawezekana. Hebu jitafutie hicho kitabu uone jinsi unavyoweza kufanya mazingaombwe ya kuwa ulivyokusudiwa kuwa bila ku-kopi na ku-pasti walivyo wengine. Bila kutumia vitu vya kukuongezea stimu yenye madhara kwa mwili na kuvuruga kemikali ya dopamine inayovuruga maamuzi yako kutoka mtu wa kiasi kwenda mtumiaji wa pombe, vyakula, ngono na anasa nyingine kupitiliza.
Hebu fikiria unabahatika kwenda mahali. Unakuta kuna MC makini kwa Mazingaombwe ya kusherehesha. Dopamine za kujipa mwenyewe kama vyakula na vinywaji ndo usiseme. Watoto wa Mujini wanasema kata Mti panda Mti. MC anakufurahisha kiasi cha kutosha. Wewe unafanya ku-copi halafu bila mazoezi yoyote unaamua kwenda ku-pasti kwa mwenzio nyumbani.
Je, kama unajua ku-copi mazingaombwe si bora ujue na ku-pasti basi? Kwanini usiwe Mjanja ukafanya uchunguzi (Experiment)? Mazoezi kwanza? Kama dopamine imekutawala shida inaanzia hapo. Huwezi jua hata ufanye nini?
Leo kuna mwana-Karakana anaomba nimpe ujumbe wa kualika watu wawili ambao ameona wanafaa kuja humu. Ninajua kwa muda tuliotumia kuelimishana hilo siyo tatizo kabisa. Tuna watu wanaoweza kutushirikisha ujumbe wa kitu cha kusema kwa wale tunaotaka kuwakaribisha. Nani afanye hilo zingaombwe?
Sasa turudi kwa Msema Chochote au MC wa Mazingaombwe kwenye shughuli. Alijisemea hivi:
Siku nzuri za maisha yangu ni zile nilizokuwa nikiishi na Malkia wa mwanaume mwingine.
Watu wakanyamaza kimya wakisikiliza anachotaka kusema.
Akaendelea kusema na kumtaja huyo Malkia akidai alikuwa ni Mama yake Mzazi.
Baba yake mzazi ndo alikuwa huyo mwanaume mwenzake. Jamani! Watu wakacheka sana kwa furaha huku wakimshangilia kwa makofi na vigelegele.
Jamaa mmoja akajiongeza kwenda kumfanyia mkewe mazingaombwe bila ya kufanya mazoezi kidogo (experiment).
Madhara ya dopamine ikizidi mwilini bila shaka huwa hukufanya kama mwehu vile. Unachezea Zingaombwe la Kata Mti Panda Mti? Ogopa! Ila - Inawezekana kuwa mtu wa kiasi. Ni kujiwekea lengo na kutengeneza tabia stahiki.
Jamaa akasema......mke wangu! Unajua..... nilikuwa na siku nzuri sana katika maisha yangu kabla hatujaoana kwani nilikuwa naishi na Mke wa mwanaume mwenzangu.........
Wakati akiendelea kufikiria alichosema MC, maneno yakamkimbia!..... mkewe akakosa subira akamfikiria jinsi ambavyo sivyo. Akajiongeza kivingine. Puuu! Jamaa akarushiwa simu usoni! Paji la uso likachanika. Mara damu hiyoooo! Nani mwenye makosa? Hii ni habari ya kweli.
Hebu fikiria kidogo hapo.
Mawasiliano ni kitu muhimu sana.
Kama unaowasiliana nao, wakielewa vizuri ujumbe wako, mrejesho wa kile kinachotakiwa unakuwa mzuri sana. Nimefurahishwa na baathi ya mirejesho au feedback za wana-Karakana siku za karibuni.
Japo waliituma mirejesho yao inbox inaelekea mawasiliano yetu yanakwenda kwa maelewano mazuri sana. Kilichobakia ni vitendo.
Tuko wanachama karibu 160 humu mpaka sasa. Ninajiuliza tufanye nini kuelekea kufikia malengo ya Tarehe 28.01.2018?
Jamaa aliyepigwa na simu angejiongeza kidogo angefanya kwanza mazoezi.
La sivyo angesimulia story jinsi ilivyokuwa. Angefanya kunukuu lile zingaombwe la MC na mkewe asingemrushia simu kama angeshindwa ku-pasti kama ilivyomtokea.
Wewe unalionaje hilo suala?
Unapokuwa unafanya mambo yako na watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kuwasiliana pia unaishia kuambulia kitu na zaidi kupata mafanikio makubwa kama utajiongeza kwa kufanya uchunguzi (experiment).
Jifunze kwenda hatua moja zaidi.
Je, ni jinsi gani au njia ipi itumike kutufikisha huko? Tunahitaji zana zipi ili tukifanya ku-copy kwenye mafunzo yetu tunayoyapata humu kwenye Karakana ya Ubongo au popote tuweze ku-pasti na kutumia bila kusahau kuwa Bahari isiyo na chumvi? Hakuna anayetaka kuwa Bahari Mfu.
Mazingaombwe yetu yatakuwa yanatupa manufaa kama tunachojifunza tunakifanyia kazi.
Kazi ya Kocha ni sawa na kumwagilia bustani iliyoko jangwani. Ili maji yatumike vizuri inabidi kila tone liende kwenye mche unaomea. Hapo maji hayatapotea bila sababu.
Ili hayo maji yatumike vizuri ni lazima ukae kwenye kifungulia maji (on the Tap).
Ukitumia mashine ya kurusha maji utakuwa juu ya hali ulipo ya kimazingira (on top of the situation) lakini bado itakuwa ni shida. Hakuna ufanisi. Maji mengi yatapotea bila sababu ya msingi.
Kumwagilia jangwa maji bila malengo maalumu ni kucheza pata potea. Hata kama utatengeneza mfereji kutoka Baharini. Bado kazi itakuwa ni kubwa sana. Kule Israel japo ni jangwa wamefanikiwa kutumia drip irrigation......wanamwagia kwa teke-linalotujia (technology) kwa kumwaga tone moja baada ya jingine pale kwenye shina au mimea unaohitaji maji.
Elimu ni Bahari. Tumeona kuna Bahari hai zenye viumbe na mimea tele. Tumeona pia Bahari Mfu. Zenye chumvi pekee. Hakuna cha viumbe hai wala mimea. Je, maarifa unayoyapata unayageuza Bahari ipi? Maji yaliyoko ndani yako yanatoa zawadi ya uhai kwa wenye uhitaji? Au ndo umeamua kuyageuza chumvi?
Unaweza kufanya kitu.
Mimi Kocha wako nimejifunza kitu kutoka kwa Mwandishi wetu Lameck Hulilo. Anatuasa tutumie vizuri tulicho nacho. Kila mtu awe tajiri au maskini amepewa masaa 24. Mungu hajampendelea yeyote muda. Ila ni kwa kujiongeza pekee tunaweza kufanya siku ikawa na masaa 28. Hilo nalo ni zingaombwe lingine la kuongelea tukipata fursa.
Haijalishi kama wewe ni Bahari yenye chumvi au ni jangwa lenye ukame usiovumilika. Kuna mazingaombwe ambayo yakifanyika mabadiliko ni lazima.
Tuanze na kile kidogo tulicho nacho. Tunaweza kutenga muda wa kuongea na watu wawili hadi kumi tukawakaribisha kwenye Gari yetu ya Karakana ya Ubongo.
Tunaweza kutafuta nguo ambazo hatuzitumii ama zetu wenyewe au marafiki zetu tukawapa wenye uhitaji. Pia unaweza kutoa ufadhili wa T-shirt na kofia kwa wale watakaofika siku ile.
Kikubwa ninachotaka kukuasa leo ni ‘FIKIRIA KUTOA KWA WENGINE NA SIO KUPOKEA TU’
Umasikini kimsingi unatokana na fikra na sio vile tulivyonavyo.
Jiulize, hivi katika maisha yako ni kweli huna kitu unachoweza kumsaidia mwingine?
Usikae mkao wa kupokea tu kila wakati,jipange na uwe na mawazo ya kutoa kila wakati,
Ukifanya hivyo utaongeza nguvu yako ya ubunifu na utakuwa umetuma maelezo kwenye ubongo uliofichika (sub-consious mind’ ya kuwa wewe ni mtu uliyeona tayari hatima yako.
Angalia kama kuna nguo unaweza kuwasaidia wenye uhitaji, au viatu ama hata chakula ama pesa pia.
Kumbuka hakuna aliyeng’ara na kufikia ndoto yake duniani kwa kujilimbikizia mwenyewe na kuwa mchoyo.

ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2018 NDIO IMEANZA. HIYO NI NAMBA TU NA HAINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.
NAWATAKIA KHERI NA BARAKA TELE KATIKA YA MWAKA 2018.
SEE YOU TO THE TOP WHERE IS NOT CROWDED.
Ninakushukuru sana kwa kuweza kunifuatilia na nikuombe kuwa huru kunipigia, au kuniandikia, maana najisikia vizuri sana ninapoweza kuwa msaada kwa mtu. Mimi ni mtumishi wenu. Na kwa vile umeamua mwenyewe kuwemo humu basi huna budi kuhakikisha tunajadili kwa pamoja na kufikia suluhisho muafaka kwa maisha yetu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...