Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mikakati 6 Muhimu Ili Kujijengea Kujiamini

1. Kila siku ni vyema kujikumbusha ya kwamba ulishafanya mambo mazuri siku za nyuma. Hebu tafakari yote mazuri ambayo uliweza fanikisha kuyatimiliza.
a. Kikubwa mawazo yako, nguvu zako na muda wako vyote elekeza katika yale uliyokwisha wahi kuyafanikisha. HILI SI JAMBO LA KUPUUZIA HATA KIDOGO.
Nashauri kufuata yafuatayo:-
• Kuwa na mpango kazi wa siku. Weka vipaumbele yaani mambo yote yenye muhimu kuliko mengine ndiyo uanze nayo. Mfano unapopangilia kukutana na watu, kupitia miradi, na mengine mengi tu unayokusudia kuyatenda ni vyema kuyapanga kwa kuzingatia uzito wa kila jambo.
Kikubwa mipango ya siku inayofuata ifanyike usiku kabla ya kulala.
• Kuchukua Hatua/Kutenda/Kufanyia kazi mipango mkakati – Tumia muda wako vizuri kwa kuanza na mambo yote muhimu maana utakuwa umeonesha katika mpango kazi wako.
Inashauriwa uwe unashughurikia malengo ya siku 60 kila mara.
Nini maana yake? Kikubwa mipango yako isitoke nje katika kufikia malengo ya siku 60 na hapa ni lazima ujilazimishe kufikia haya malengo. Inawezekana kabisa wewe wekeza mawazo yako kukamilisha malengo yako ya siku 60.
• Kujifunza –Kuza uelewa wako kupitia kujisomea, usikilizaji wa cassete/audio/video, Maongezi na kocha wako ana kwa ana kila baada ya muda fulani
• Kupumzika –Ondoa uchovu na msongo wa mawazo ya siku kwa kutahajudi, kusikiliza music na kupata muda na familia
• Fikiri – Pata muda wa kutathimini siku yako ilivyokwenda. Pitia malengo yako, yatengenezee picha kwenye ubongo. Anza kuyaona malengo yako kupitia ubongo. Pata mawazo mapya. Ni vyema ukawa na mahali pa kuandika.
MWENENDO WAKO UTAAMUA HATIMA YAKO.
KUJENGA MAHUSIANO BORA NI TABIA NA SIKU ZOTE HULETA MATOKEO MAZURI AJABU.
2. Soma Biographies na Autobiographies.
Tuanze na Biography – Maelezo ya kina juu ya maisha ya mtu. Maelezo haya ni zaidi ya mambo ya msingi juu ya maisha yake kama vile elimu, kazi, mahusiano na kifo. Hupambanua uzoefu wa mtu kutokana na matukio hayo ya kimaisha. Hii itakusaidia sana kujiimarisha unapopata muda wa kusoma maisha ya mtu mfano Mandela, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wengine wengi. (detailed description of a person's life. It involves more than just the basic facts like education, work, relationships, and death; it portrays a person's experience of these life events)
Pili ni Autobiographies – Haya ni maandishi aliyoandika mtu mwenyewe juu ya maisha yake (a self-written account of the life of a person). Kujifunza kupitia uzoefu wa watu imedhirika kuwa ni moja ya njia bora sana katika kujifunza.
Nakushauri tembelea maktaba kuu ya Taifa na ikibidi kuwa mwanachama uweze kufaidika na biographies na autobiographies za watu mbalimbali.
Maisha pasipo changamoto ni uongo.
Kubali tafsiri halisi ya maisha ambayo ni kupanda na kushuka kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote yule. Hakuna aliyesamehewa kupanda na kushuka.
Usione kufanikiwa kwa mtu, hujui nyuma ya pazia. Kupanda na kushuka ndio maisha yenyewe.
Kujiamini kwako huongezeka pale unapokabiliana na changamoto za maisha.
Ukweli ni kwamba huwezi shinda changamoto zote, lakini ukiwa chanya utashinda changamoto nyingi zaidi ya kawaida.
3. Kuwa mtu wa shukrani. Jenga tabia ya kushukuru angalau watu wawili kwa wiki kwa namna maalum kama vile kuwanunulia kadi ya shukrani, kuwa tumia ujumbe au kuwapigia simu ya kuwashukuru.
Hii haimaanishi wiki nzima utakaa kimya pasipo kushukuru watu, la hasha, Shukrani iwe ni moja ya vazi lako la kila siku.
4. Jitume na jilazimishe kutimiza malengo yako ya muda mfupi.
Hakuna njia bora zaidi katika kujijengea kujiamini kama kuhakikisha mambo yanatokea/yanakamilika.
UNAHITAJI KUPOTEZA WAKATI MWINGINE KABLA HUJAPATA UNACHOKITAKA.
USIOGOPE NDIO MCHAKATO WENYEWE KATIKA KUTIMIZA MALENGO. SIKU ZOTE NI KUJIFUNZA NA KUFANIKISHA.
5. Jenga mtandao wa kuaminika kusaidiana wa watu 5 hadi 6. Si kazi rahisi kupata watu sahihi (wasio wanafiki). Kuwa mwangalifu. Ndugu na marafiki huingia katika kundi hili.
Jua kwa hakika ni ndugu yupi na rafiki yupi ni wakweli yaani hawaoni tabu kukuambia ukweli lakini kwa upendo ili kukuimarisha. Ukiweza kupata watu wa jinsi hiyo tafadhali shikamana nao. Maisha ni kuwa na team nzuri. Huwezi fanikisha mambo kivyako vyako tu. Labda kama ni mambo madogo madogo.
6. Jitendee kitu kila wiki usiache kufanya hivyo. Tafuta namna utakavyosheherekea mafanikio yako ya wiki.
Vipi unadhani hustahili kujifanyia hivyo? Kama jibu lako unasema hustahili basi anza na hatua ya kwanza tena na fuatilia hadi hatua ya sita.
SAFARI YA KUJIAMINI HUANZA NA MAFANIKIO YA WIKI. JIFUNZE KUJIPONGEZA WEWE MWENYE. MAISHA TUYAFURAHIE NA KUCHAPA KAZI.
Kifupi namshukuru Mungu sana kwa huduma hii ya kufundisha na kuna mengi mazuri yanakuja.
Nikuombe kitu kimoja ‘KIZURI KULA NA MWENZAKO’. Naamini hukosi watu kumi wa kuwaelezea kinachoendelea karakana ya ubongo na pia usiache kuwaelezea masharti yaliyopo.
Wakikuelewa basi waadd maana u admin pia, huhitaji kunisubiria uniambie.
PAMOJA TUNAWEZA KUWA CHACHU YA MABADILIKO.
FANYIA MAZOEZI YA KUJIKUBALI NA KAMWE USIRUHUSU KUTOJIKUBALI KWANI KWA KUFANYA HIVYO UTAKUWA UNAJIADHIBU.
Weka mikakati na ingia kazini. Ukishindwa kupangilia mambo ya kufanya kufikia malengo maana yake umepanga kushindwa kufikia malengo yako (If yo do not plan, you plan to fail).
ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2018 NDIO IMEANZA. HIYO NI NAMBA TU NA HAINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.
NAWATAKIA KHERI NA BARAKA TELE KATIKA YA MWAKA 2018.
SEE YOU TO THE TOP WHERE IS NOT CROWDED.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...