Bado tunafurahia mwaka mpya kwa namna ya kipekee kabisa.
Nikiwa Kocha ninapenda kufanya kitu kinaitwa "walk the talk."
Kuna Wataalamu wanasema ili kujenga tabia ni lazima urudie rudie kufanya kitu angalau siku zisizopungua ishirini na moja (21).
Ila kwa wale wenye nia na dhamira nzito inachukua masaa ishirini (20) kujitengenezea tabia fulani.
Mikono isiyoonekana itatumikaje kwa siku hii ndani ya Wazo la Leo?
Ukizingatia jana Nilikuuliza swali, " Je, mikono yako inatumika vizuri?"
Bado ninajijengea tabia kama Kocha niweze kutumia mikono yangu inayoonekana na pia ile isiyoonnekana.
Nimefurahishwa na Mwana-Karakana huyu aliyetumia mikono ya kuandika yafuatayo:
"Mimi leo nina watu wawili watajiunga kwenye kundi hili"
Ninaweza kusema kwamba mikono yake ni sehemu ya mikono ya Kocha wenu isiyoonekana. Je, wewe una mikono mingapi isiyoonekana? Je, inafanya kazi vizuri?
Tafakari! Chukua hatua pia.
Ninaamini kama umetafakari vizuri utagundua mimi kocha wako nilishakupa mikono ambayo haionekani lakini unayo. Je, unaitumia vizuri?
Unashangaa na kujiuliza mikono ipi tena?
Kocha mzuri ni yule anayekujengea uwezo.
Jiulize, kwa nini kila mtu humu ndani ni Admin?
Hiyo ni kwa sababu kila Mwana-Karakana aweze kutumia mikono yake mwenyewe kufanya anachotakiwa kufanya. Mimi kama kocha nimejiwekea lengo la kuwa na mikono isiyoonekana 2000 siku za usoni. Mikono elfu mbili ni watu 1000.
Ninajiuliza! Je, wewe unaweza kujitafutia mikono isiyoonekana 20 ndani ya Karakana ya Ubongo? Hao ni watu kumi ambao sina shaka watakuwa ni daraja la kwanza kama wewe.
Kizuri kula na nduguyo.
Kuna jambo moja la ajabu kuhusu binadamu: Tunao wakati mgumu sana kuona na kutambua vile vitu visivyooneka japo vipo na vinafanya kazi kwenye maisha yetu.
Hivi siku nikikuta Wana-Karakana wamefikia 1000 nianze kushangaa na kusingizia Wachawi wamefanya mambo yao kisa sikutumia mikono yangu ku-add wanachama?
Nini maana ya kuumba vitu upya? Ni kuwa na mawazo mapya siyo?
Nini maana ya mawazo mapya?
Ni kutenda kwa utofauti zaidi ukijilinganisha na juzi na jana.
Kama hii mikono isiyoonekana inatenda mambo makubwa namna hii!
Je, tukiamua kujitoa ndani ya magereza yaliyomo kwenye vichwa vyetu itakuwaje?
Hilo ni somo zuri sana la tarehe 29.01.2018 baada ya kufanya tathmini ya lile jaribio la kwanza la kupeleka nguo na vitu vya aina hiyo pale Muhimbili. Kumbuka ni 28.01.2018.
Kupima na kuona huduma ya kitu kisichoonekana ni kazi ngumu kwa macho ya kawaida.
Hebu fikiria Daktari anayesaidia watu wasiugue kwa kutoa kinga!
Hebu fikiria yule Daktari anayetibu!
Anayetoa kinga kazi yake haionekani kwa jicho la kawaida.
Anakuwepo tu. Anayebeba sifa kubwa na kusifiwa sana ni yule anayeonekana akitibu.
Wako wote?
Nitatoa mfano mwingine makazini mwetu!
Kisichoonekana huwa hakipewi thamani stahiki.
Maofisa wengi na wale ma-meneja tulio nao makazini ambao wanajua kutumia mikono isiyoonekana ni watendaji wazuri sana japo hawatambuliki na ni mara chache sana utawaona wakipewa zawadi.
Watu wa aina hiyo wanafanya mengi kuokoa muda na bidii au juhudi za watu wengine tena kwa ufanisi mkubwa.
Japokuwa ubunifu wao unaonekana kwa shida, ni mara chache sana wanasaidiwa wafikie malengo yao mazuri hadi wanapoondika kwa sababu yoyote ile ndo pengo linapoanzia kuonekana.
Kwa nini pengo ndo litufanye tuone umuhimu wa mtu au watu?
Jibu lake ni rahisi sana.
Tuna tabia ya kuwa wavivu wa kufikiria.
Kazi ya ubongo ni kuunda kwa kutumia mawazo yaliyopo tayari. Ubongo hauwezi kuleta mawazo mapya bila kuufundisha mbinu za kuleta mawazo mapya(new ideas)
Ubongo ni kama Kamera inayokupiga picha na ukajiona ulivyovaa.
Karakana ya Ubongo ni zaidi ya hapo. Unaijua kazi ya X-ray ? Inapiga picha mpaka kule ndani kabisa ikionyesha mifupa, viungo, mishipa n.k
Mambo yanayotokea ndani ya mwili yanawekwa wazi.
Kazi kwako. Unahitaji jicho kama la X-ray kuona mikono isiyoonekana ikifanya kazi. Mara nyingi huwa kuna vitu tunavipuuza lakini ni vya kufanyia kazi.
Katika kujitoa na kujitolea kufanya shughuli kama ile ya Karakana ya Ubongo unaweza kudhania hiyo kwenda Muhimbili au hata kupeleka nguo ni kwa ajili ya wale wenye uhitaji pekee. La hasha.
Ushiriki wako ni fursa nzuri ya kutengeneza ubongo na akili yako iwe kama X-ray.
Nakushauri ujaribu, kwa kuanza kidogo kidogo na utashangaa unajifungulia milango ya ajabu.
Utashangaa unajiongezea mikono isiyooneka. Utajipatia miguu ya ziada isiyoonekana. Miujiza bado ipo na inatokea kila siku kwa wenye macho ya X-ray.
Huwa tunapata wakati mgumu sana kutambua mambo yanayoendelea kwa kuyasubiria yajitokeze. Hiyo ni sahau. Lazima ujiongeze kwa kutengeneza tabia fulani ambazo zitakupaisha kuelekea huko kwenye miujiza. Kujitoa na kujitolea ni muhimu.
Ndiyo maana mimi Kocha wako nataka tufike mahali.
Ninataka baraka za Mwenyezi Mungu zishukie Karakana ya Ubongo.
Mungu akipenda Januari 2018 gari letu Karakana ya Ubongo liwe linaanza kuelekea safari ya kutekeleza malengo yake.
Je, uko tayari kutumia mikono yako isiyoonekana?
Miguu yako isiyoonekana?
Chochote ulicho nacho kisichoonekana?
Kama tulivyoona kupitia Kalenda yetu, tuna malengo matatu kama ifuatavyo:
1) Kutoa Newsletter December 2018.
2) Kuchapisha Vitabu viwili, kimoja kitatoka June na kingine December 2018.
3) Kuwa na Warsha au Semina mbili, moja kufanyia June na nyingine December 2018.
Kama inavyoonekana hapo, kazi ni kubwa.
Tayari safu yangu ya uongozi ambayo haionekani wanafanya kazi kubwa sana.
Hawa watu ni mikono na miguu yangu na pia sehemu ya akili yangu usiyoiona hata kwa kusoma Wazo la Leo.
Bahati nzuri, unaweza kuamua kuwa chochote kisichoonekana katika harakati za kutumia jicho la kawaida na ukafanya kitu mwaka huu wa 2018.
Mathalani wewe ni mtu wa daraja la kwanza, natambua umeshajiwekea malengo ya mwaka 2018.
Hizo zitakuwa ni kazi za mikono yako inayoonekana. Je, una mikono mingapi isiyoonekana inakusaidia?
Ule wa Kiroho unajulikana.
Kwa kutumia mitizamo hii mipya tunayojifunza kila siku , tunahitaji kupangilia malengo yetu yavae tabia husika inayorahisisha malengo yetu.
Dr Bukaza Chachage, msomi anayependa kujiongeza aliwahi kusema ya kwamba, jambo moja la kujifunza ni kwamba "huna kesho wala jana. Na kwa leo hii, unayo sasa hivi tu." Na akatamani "tufanye kila kitu ukijua hivyo," mwisho wa kumnukuu.
Madhara ya Mikono Isiyoonekana
Kazi ya kuwa Kocha ni ngumu na ina makwazo mengi.
Ili uwe Kocha mzuri ni lazima uwe na uwezo wa kuona mikono isiyoonekana na mengine kama hayo kutoka kwa watu wako.
Zaidi ya hapo ni lazima kutumia jicho la X-ray kuona matatizo na changamoto za watu wako bila kusahau kuyatatua wakati yakiwa madogo kama kichuguu kabla hayajawa kama mlima Kilimanjaro.
Nikiweza kufanya hivyo nitakuwa nimefikia wito nilioitiwa kufanya hapa Duniani.
Baadhi ya Makocha wazuri kabisa waliopo huwa hatuoni wanachokifanya na hatuna sababu za kuwashukuru.
Sababu ya msingi ni kwamba hatuna macho ya kuona zile cheche walizozima ambazo zingeleta moto wa hatari. Sisi tuko tunadhania kazi inafanywa na yule anayezima moto kisa tunamuona na maji yake akizima moto.
Kazi ya zima moto ni ngumu na kubwa. Mfano mdogo ni kitu kinaitwa "fuse" huwa kinakata umeme unapozidi kiwango kinachotakiwa kupita.
Kifaa hicho kidogo kisichoonekana ninaweza kukifananisha na Kocha.
Kocha anayefanya kazi baada ya madhara kutokea ndiye anasifika vizuri na pia hata kama ukimya wake wa kutokuchukua hatua ya tahadhari amesababisha lililotokea kwa uzembe wake mwenyewe, hilo huwa halionekani.
Kocha wa kwanza wa mtu ni mtu mwenyewe. Mimi ni kocha wa huyo Kocha wako ambaye ni wewe.
Nitakayokuambia, kocha wako akakutia uvivu usitende au ukatenda kizembe usipate ulichotarajia ninaweza kubeba lawama kiasi.
Ila sehemu kubwa ya lawama inakuangukia.
Kuzuia moto ni bora zaidi ya kuzima moto.
Kinga ni bora lakini haipewi umuhimu unaostahili.
Ndo maana biashara zote ambazo zinahusiana na kuzuia au kinga kama vile bima, coaching ni sawa na uendawazimu. Ni kazi ngumu.
Ndiyo maana utakuta watu hutumia njia za mkato kufikia watu kwa kuonyesha vile vinavyoonekana pekee.
Kwa ni baadhi ya magazeti yanaweka udaku kurasa za mbele?
Je, umeshajikuta unanunua kwa sababu kichwa cha habari kinavutia halafu ndani hakuna kitu?
Au ulichokitarajia sicho? Kazi kwako
Kuna haja ya kujifunza kuonyesha manufaa ya kile kisichooneka ili tuweze kutambua siri nzito iliyofichika ndani ya ulimwengu wa kiroho. Unaweza kudhania kwa kutokuchukua hatua ndo kitu kizuri zaidi cha kufanya lakini ni lazima kufanya kitu.
Kuna watu wenye maono makubwa. Na kuna watu wenye uwezo wa kutendea kazi maono yao. Inabidi ujue nafasi yako ni ipi.
Kama inakuwa vigumu kuijua nafasi yako anza kwa kujitolea mahali.
Hata kama utafanya bure, mikono isiyoonekana itakuwa kazini kumalizia pale unapolega lega.
Shida nyingi humu Duniani zinasababishwa na watu wasiochukua hatua pale ilipobidi wafanye hivyo.
Mtu anakuwa na la kusema ili azime moto mahali lakini anaacha moshi uendelee kutoka.
Utagundua hayo mabenki yaliyofungiwa juzi yalikuwa yalete majanga.
Hatua za dharura zimechukuliwa ili kuzima moto.
Kuna hatua stahiki ambazo zinafaa kuchukuliwa ili tuache tabia zisizofaa na kujenga tabia zinazofaa.
Je, tunaweza kukaa chini kuangalia moto ukiwaka tusifanye chochote?
Wewe unafanya nini mwezi huu wa January tofauti na miaka yote iliyopita?
Kuna watu hawana mavazi. Tunaweza kuunganisha nguvu tukafanya kitu.Tarehe inafahamika. Uko tayari?
Tabia rahisi ya kujijengea ili uweze kuyapata yote niliyoongelea na mengine mazuri na makubwa zaidi ni kufikiria mbele ya pua. Unapofikiria mbele ya pua na kujipanga kama mimi ninavyofanya kwa ajili ya Gari letu Karakana ya Ubongo, nikisaidiwa na mikono yenu isiyoonekana kama Kocha mwenzangu aliyeko ndani yako atakuruhusu utakuwa ni muujiza wako wa kwanza kwa mwaka 2018.
Nimefurahishwa kuweza kufanya kazi ya ziada ili uweze kuwa na macho yanayoona vile visivyoonekana.
Kwa hiyo usiache kumkumbuka hata yule Mwalimu wako wa shule ya Msingi aliyefanya kazi ya ziada kwa mikono yake isiyoonekana ndo amekufanya ufike hapo ulipo.
Muda tulio nao ni sasa. Jana haipo wala kesho haipo.
Unaweza kuibadilisha kesho yako kwa kuitumia Leo yako kwa sasa kutengeneza na kupalilia vile vitu vinavuofanya kazi kwa ufanisi bila hata kuonekana.
Gari yetu Karakana ya Ubongo ndo iko kwenye maandalizi.
Tarehe 28.01.2018 tutafanya jaribio dogo la kujipima.
Mimi Kocha nitajipima.
Mwana-Karakana jipime.
Kazi kwetu.

Maoni
Chapisha Maoni