Mikono Yako Inatumika Vizuri?
Kwa mara nyingine tena, narudia kukutakia Heri ya Mwaka Mpya 2018.
Mikono yangu inatumika ipasavyo kuandika Wazo la Leo.
Ukizingatia ile chupa ya Shampeni sasa iko tupu. Ule Mti wa Plastic uitwao Xmas Tree kwa lugha ya wenzetu
uliokuwa unawaka umeshazimwa!
Sina shaka mikono yako ilitumika kikamilifu. Huu ni muda muafaka wa kutafakari miezi 12 ijayo na jinsi mikono yako itakavyotumika.
Je, utatumika namna gani kusababisha angalau tone la mvua lionekane mwezi huu wa January 2018?
Utachambua zile nguo ambazo huvai tena?
Utazifua na kuzinyoosha ili uwapatie wahitaji? Huwa Mungu anabariki kazi za mikono yetu.
Mimi Kocha wako nataka tufike mahali. Ninataka baraka za Mwenyezi Mungu zishukie Karakana ya Ubongo.
Mungu akipenda Januari 2018 gari letu Karakana ya Ubongo liwe linaanza kuelekea safari ya kutekeleza malengo yake.
Je, uko tayari kutumia mikono yako vizuri?
Kama tulivyoona kupitia Kalenda yetu, tuna malengo matatu kama ifuatavyo:
1) Kutoa Newsletter December 2018.
2) Kuchapisha Vitabu viwili, kimoja kitatoka June na kingine December 2018.
3) Kuwa na Warsha au Semina mbili, moja kufanyia June na nyingine December 2018.
Kama inavyoonekana hapo, kazi ni kubwa. Tayari watu wangu wanafanya kazi kuanzia zile za ndani ambazo hazionekani na wala hazitaonekana; hadi mpaka zile ambazo zitakazoonekana kupitia Kalenda yetu ya mwaka 2018.
Kazi ambazo hazionekani ni pamoja na maandalizi ya tovuti itakayobeba maarifa na vitu mbali mbali tutakavyotumia kujifunza ili tuweze kutoka mahali A hadi mahali B tunakotaka kufika.
Mathalani wewe ni mtu wa daraja la kwanza, natambua umeshajiwekea malengo ya mwaka 2018. Hizo zitakuwa ni kazi as mikono yako.
Kwa kutumia mtizamo mpya niliowapa siku za karibuni, tunahitaji kupangilia malengo yetu yavae tabia husika inayorahisisha malengo yetu.
Uzalishaji kwa lugha ya kigeni productivity ni kitu kinachoeleweka kwa urahisi kama tunajenga tabia stahiki ili mambo yawe yanatendeka vizuri na kwa ufanisi hadi kufikia mlango wa mafanikio yetu. Wala usipate shida kunielewa.
Kama malengo yako umeyaandika kwa kutumia vizuri mikono yako basi endeles kuongozana nami.
Kama bado, safari yako na iishie hapa.
Tafadhali kaa chini, utumie mikono yako kuandika malengo yako ili uweze kuongozana nami utakapokuwa tayari.
Kwa walioandika malengo, huu ni muda wa kutengeneza mfumo wenye akili ambao utakusaidia kuvaa tabia stahiki kufikia malengo yako.
Mpaka hapo, ninaamini tuko wote. Ninahitaji umakini wako zaidi kuanzia hapa.
Mtaalamu Charles Duhigg, Mwandishi wa Kitabu cha Nguvu za Tabia alipendekeza hatua tatu za kufanya ili kujenga tabia stahiki.
Unataka nini? Una lengo gani? Kusoma zaidi?
1. Chagua kitu unachopenda kiwe sehemu ya tabia yako. Mfano: weka kitabu mahali ambapo utakiona kabla ya kulala ili usome kurasa chache kabla ya kulala.
2. Chagua zawadi ambayo itakupa nguvu na msukumo wa kutenda. Mfano: Ahadi ya kuandika summary kwa Wasomaji wa Karakana ya Ubongo ili wajifunze ulichosoma.
3) Tekeleza ulichodhamiria. Kuwa mtu wa kiasi ili usijikwamishe katika ujenzi wa tabia mpya unayoijenga. Ukiona kurasa 10 ni nyingi anza na kurasa 2 au 3 ukishazoea utajikuta tabia inajengeka.
Ni kama ile hadithi ya Pavlov na Mbwa wake. Anampa chakula halafu anagonga kengele kila siku. Ikatokea siku kengele imegongwa bila chakula.
Mmbwa akajipeleka sehemu yake anapowekewa chakula akaambulia sahani tupu.
Zawadi yake haikuwepo. Hiyo ndo nguvu ya tabia.
Tabia ni mfano mzuri unaoweza kutuletea
mageuzi makubwa sana katika maisha yetu ya kila siku.
Hebu tufanye marejeo ya matumizi yetu, tunaweza je kutengeneza kipato `kipya` bila matumizi yetu kuongezeka? Hapo ni suala la kujitazama zaidi.
Jawabu letu pia linaweza kuwa ni kujenga tabia za kuacha au kupunguza matumizi yasiyo ya lazima (wants vs needs) mfano ni anaza kama sigara, pombe, kuishi maisha ya juu kuliko uwezo wa kipato na kubaki na matumizi ya lazima na muhimu tu.
Kuna tabia nzuri sana walizo nazo matajiri wengi ambazo baathi ya watu wa kawaida hawana.
Mfano ni ununuzi wa mahitaji kwa bei ya jumla. Tabia ya kununua vitu kwa bei ya jumla inaokoa fedha nyingi sana ukifanya utafiti. Kwa mwaka tajiri anaweza kutumia hela kidogo sana kuliko mtu wa kawaida au hata maskini na bado akawa amefaida ubora wa kila alichonunua; naongelea huduma au mahitaji ya daraja la kwanza.
Ni tabia inayoweza kuongeza kipato chako bila hata kuchukua mkopo wala kupandishwa mshahara au Cheo kama umeajiriwa.
Huu ni mwaka mpya 2018, hebu tujipange upya kwa kutumia rasilimali tulizo nazo na pia kuleta mabadiliko kwa jamii iliyotuzunguka.
Je, tuna nini ambacho hukitumii mikononi mwako?
Nguo zote mikononi mwako unazitumia kwa manufaa sahihi?
Tunawezaje kufanya ukaguzi binafsi tujue mahitaji yetu? (Needs vs Wants).
Tunawezaje kugundua kitu cha kufanya kwa tofauti mwaka huu?
Hebu tuangalie watu walivyofungua fursa zao kwa vile vitu walivyokuwa navyo bila wao kujua thamani ya walichoshikilia mikononi mwao.
1) Fimbo:
Musa kwenye Biblia aliulizwa umebeba nini mkononi mwako?"
Akajibu akisema " fimbo". Akaagizwa ayapige maji ya bahari, nayo yakagawanyika na wana wa Israel wakapata njia ya kujikomboa.
Vivyo hivyo, Elisha mtu wa Mungu aliwahi kutumia kijiti alichokata baada ya kuuliza mahali shoka la kuazima lilipodondokea mtoni.
Akaitupa ile fimbo mahali alipoonyeshwa na lile shoka likaelea na likachukuliwa. .
Je, umeshikilia fimbo gani mikononi mwako?
Kabati lako la nguo lahitaji fimbo lifungue baraka za wengine kuvaa na kupendeza?
2) Mwanamke Wa kwanza alionyesha vitu alivyokuwa navyo kwenye kikapu chake alichobeba mikononi mwake.
Mikate miwili na samaki watano tu. Vilibarikiwa vikalisha zaidi ya wanaume 5,000. Hapo wanawake na watoto hawajahesabiwa bado.
Wa pili alikuwa ni Mjane mwenye madeni baada ya kufiwa na mumewe.
Akaulizwa maswali ya msingi:
"Nikufanyie nini?
Niambie; una kitu gani nyumbani?"
Akajibu kwa kusema, hana kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.
Vilibarikiwa na kwa maajabu vyombo vyake na vya majirani vikajaa mafuta.
Yule Mjane akaambiwa atumie mafuta na watoto wake. Mengine akayauze ili alipe deni aliloachiwa na mumewe.
Hapo inaashiria nini? Mikono mitupu hailambwi?
Labda tujiulize, kazi za mikono yetu zinatupatia chochote?
Kila kitu kinawezekana kulingana na nyakati na majira. Tuamini na tuchukue hatua ya kujipanga upya kwa vile tulivyo navyo mikononi mwetu.
Mfano, teknolojia imeondoa mipaka iliyokuwepo kati ya maisha yako binafsi na kazi yako. Unategemewa kupigiwa simu muda wowote, kuitwa kazini muda wowote, kufanya kazi muda mrefu zaidi hata ikibidi uende nayo nyumbani n.k
Hali kama hii inaonekana kutupendeza na ndo maana tunafanya hivyo. Mathalani ndo malengo tunayojiwekea hatuna budi kuyakubali mazingira tuliyojikuta tumo. Baada ya hapo tuanze kujenga zile tabia zinazofaa.
Vitu tunavyofanya, maisha yetu, watu waliotuzunguka na ushirikiano tunaotoa au kupewa bila kujali kama tunafikia malengo yetu au la ni vitu vya kuangalia upya.
Ni muda wa kuangalia upya aina ya miradi tunayoifanya ili tusiishie kunufaika binafsi bali tunufaishe na jamii kwa mapana yake.
Inatokea wakati mifumo fulani: mfumo wa maisha unatuhusu watu kuwa na ndoto kubwa. Pia, mfumo wa aina hiyo unanufaishwa na upatikanaji wa hela za ujanja ujanja unaosababishwa na maendeleo ya Teknolojia.
Yanapokuja mabadiliko ghafla na kubadilisha hiyo hali, watu wanajokuta kile kilichowapatia hela kwa urahisi kimebadilika.
Piga ua, mambo siyo. Tutatumia mbinu gani?
Tuanze kwa kutumia magari mapya ya kisasa. Gari yetu Karakana ya Ubongo ndo iko kwenye maandalizi.
Tarehe 28.01.2018 tutafanya jaribio dogo la kujipima.

Maoni
Chapisha Maoni