Mikono inayoonekana niliyo nayo ni miwili tu. Leo nataka nifanye mazingaombwe ya ukocha, tafadhali ambatana nami.
Mikono yangu isiyoonekana inaweza ikawa mingi au michache. Ninaendelea kujipima kama kocha. Je, kuna chochote ambacho umekifanya kwa utofauti na ukaona matunda na faida ya Gari yetu ya Karakana ya Ubongo?
Nitafurahi kama utanipa mrejesho sahihi. Unaweza kuutoa hapa au hata inbox.
Kwa kawaida, bado mwaka ni mpya na ninaendelea kukutakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2018.
Mwaka ambao tunabadilisha malengo yetu kiutendaji yawe mazuri kutekelezwa kwa kujenga tabia stahiki.
Mazingaombwe yangu ya leo ni uvumbuzi wa aina yake kwa ajili ya ku-copy na ku-paste yenye faida.
Mifumo yetu, masoko yetu na ugunduzi ni vitu ambavyo inabidi kuvitengeneza.
Jana nimeona Mwana-Karakana aliyejitambulisha ni Mwalimu wa Piano japo ana shahada ya ugavi na manunuzi. Nikajiuliza ni kitu gani kimemsukuma ajitambulishe wakati sijatuma siku nyingi ile meseji ya namna ya kujitambulisha.
Nikafanya utafiti wangu ambao naubatiza jina la mazingaombwe. Nikagundua aliyemkaribisha alijiongeza na kumpa siri ya ku-copy na ku-paste utambulisho wake maana amefuata format yetu akaondoa visivyomhusu, akaacha vinavyotakiwa na kuongeza anachokifanya na mwisho wa siku aka-paste.
Mazingaombwe hayakukamilika vizuri maana watu wangu wa first class hawakumkaribisha huyu Mwalimu wa Piano kwa watoto.
Nikajiuliza kama mimi Kocha kosa ili nibebe hizo lawama? Labda!
Tofauti ya mazingaombwe ninayofanya kwenye Wazo la Leo sifichi mbinu ninazotumia kama wale wahusika halisi wa Mazingaombwe unayoyajua wewe.
Ninataka nikusome unachofikiria hapo ulipo kwa kufuata maelekezo haya.
Kumbuka pia hili zoezi la Mazingaombwe nawe pia utaishia kujua mbinu na siri kubwa isiyoonekana katika mazingira ya kawaida kama ulikuwa hujui au hujakutana na kitu cha aina hii. Na tuanze.
Hatua ya kwanza:
Fikiria namba yoyote kuanzia 1 hadi 10. Mfano hiyo namba utakayofikiria tuiite Y kuiwakilisha namba husika.
Hatua ya pili:
Zidisha kwa mbili (× 2)
Jibu lako ongeza 8 (+8)
Toa ile namba uliyofikiri ( - Y)
Piga ua, hapo jibu siku zote litakuwa 4. Ndo mazingaombwe yenyewe hayo.
Hatua ya tatu:
Chukua jawabu lako (4) ukalioanishe na Alphabet ya Wazungu.
4 = D
Hatua ya nne:
Chukua herufi inayofuata:
5 = E
Hatua ya Mwisho:
Taja jina la Nchi na Mnyama anayeanza na hizo herufi D, E na rangi ya huyo Mnyama.
Jibu: A Gray Elephant from Denmark.
Mazingaombwe ya kusoma ubongo wa mtu huhitaji hata kuwa Mwanachama wa Karakana ya Ubongo.
Hapa ni suala la kutafuta mbinu za kucheza na saikolojia za watu.
Anayefanya mazingaombwe siku zote anakuwa ameficha jibu lake kwenye akili yako.
Anatumia mbinu ya maswali anayo kuuliza kukupumbaza usione anachokifanya huku akiwa anakupa burudani.
Suala la msingi, anatumia mbinu ila unaweza kumgundua ukitumia jicho lako la tatu ambalo ni Ubongo kama nilivuokuonyesha hapo.
Tuje kwenye mifumo, masoko na uvumbuzi.
Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo vikitumiwa vizuri vinaleta mapinduzi ya aina mbali mbali.
Mimi leo hii najiuliza utafanya mapinduzi gani ukimaliza kusoma Wazo la Leo?
Labda uko Tanga au Mbeya hutaweza kufika Muhimbili.
Je, unaweza kumdhamini mtu apate T-shirt na kofia?
Una ushawishi kwenye kampuni yako kufanya chochote tupate udhamini?
Ni mazingaombwe gani unaweza kufanya kufurahisha hawa wenye uhitaji?
Je, utatumika namna gani kusababisha kitu chochote kitokee ambacho mazingaombwe yangu hapa hayajakionyesha ili mwezi huu wa January 2018 tuone mapinduzi?
Vivyo hivyo hebu piga picha ya December 31, 2018. Kama mambo yafuatayo yatakuwa yamefanyika kwa ufanisi:
1) Newsletter ya Karakana ya Ubongo iko mikononi mwako.
2) Vitabu viwili kutoka Karakana ya Ubongo viko mikononi mwako
3) Umehudhuria Warsha au Semina mbili, zilizoendeshwa na Karakana ya Ubongo.
Kama inavyoonekana hapo, kazi ni kubwa. Lakini tukitumia mfano wa Mazingaombwe, ili uwe mzuri katika shughuli ya burudani ni lazima upate nguvu inayoitwa dopamine ambayo ni kemikali inayosababisha msisimko unaopatikana kiurahisi kabisa kwenye kucheza muziki, michezo ya kompyuta, madawa, n.k
Ukifanya vitu hivyo unasababisha kuongezeka kwa kemikali inayoitwa dopamine katika ubongo wa wako, jambo ambalo litakusababishia kuwa na hisia ya kuwa salama ambayo mwishowe inaweza kusababisha madhara kama mazingira uliyomo hayakulindi.
Dopamine inasababisha tunarudia tabia fulani fulani kama hizo nilizozitaja awali.
Mifano mingine inayosababisha kemikali ya dopamine itiririke ni chakula na tendo la ndoa.
Watu tunapenda kula hata kama miili yetu haihitaji kile tunachokula au kunywa.
Hizi tabia mbili za kupenda kula na ngono kisayansi zina maana kubwa maana zinatusaidia kuishi na kuendeleza utamaduni wa kizazi chetu kisiangamie.
Sasa baada ya kuona mazingaombwe ya dopamine, ni muhimu tujue namna ya kutumia mikono isiyoonekana kufanya mambo makubwa.
Wana mazingaombwe wanafanya kazi kubwa ya kujifunza kazi yao hiyo.
Wanajua vizuri namna ya kuitumia hiyo kemikali ya dopamine kwenye bongo zao.
Katika mambo yatakayotiliwa mkazo hapa Karakana ya Ubongo siku za usoni ni hilo, maana tutajua ni kwa nini watu wanaishia kuitafuta hiyo dopamine kule kusikotakiwa na jinsi ya kuwasaidia badala ya kuwakomboa na saa nyingine kuwapeleka magerezani na mahospitalini.
Kuna ukweli kwamba bila ya hiyo kemikali ya dopamine hatuwezi kupata motisha ya kufanya baathi ya mambo.
Dopamine inakufanya uweze kuwa makini katika maamuzi na ubunifu wako.
Ila kiwango cha dopamine kikizidi mwilini haswa pale tunapokitafuta kwenye vitu vilivyo nje ya utaratibu wake inasababisha tunalewa na hata kupoteza network na hekima ya kufanya maamuzi muhimu.
Njia moja nzuri sana ya kuyashinda majaribu ya dopamine ni shughuli za kutembelea mahospitalini na kusaidia watu wenye uhitaji.
Huko unapata fursa za kujifunza makosa yaliyofanywa na wengine ili usiyarudie.
Kuna baadhi ya tabia za watu wanaofanya mazingaombwe ambazo ni hatarishi lakini kwa sababu wanafanya mazoezi ya muda mrefu wanajikuta wamejijengea hizo tabia kama vile kupiga mswaki au kunawa uso.
Mathalani wewe ni mtu wa daraja la kwanza, mimi Kocha wako ninajiaminisha tunaambatana na huyo Kocha wako na tunapiga hatua.
Kwa kutumia mitizamo mipya tunayopeana kila siku kupitia Wazo la Leo na mengineyo mengi makubwa na mazuri yaliyoko njiani, tunahitaji kujipanga vizuri ili kila mazingaombwe tutakayokutana nayo tuwe na utayari wa kuona kwa lile jicho la X-ray yaliyomo ndani kabisa. Dopamine isiishie kutuletea madhara yasiyofaa katika maisha yetu.
Tabia ni mfano mzuri unaoweza kutuletea mapinduzi makubwa sana katika maisha yetu ya kila siku.
Hebu angalia malengo yako ya muda mfupi kama umeamua kujipa hiyo kemikali ya dopamine kwa kutumia simu yako ya mkononi!
Inategemea na kile inachokifanya kama kuna manufaa kwako. Je, unasoma na kufanya kazi? Au ni games na addictions nyingine?
Kwa malengo ya muda marefu, unajipa dopamine kwa kutumia simu kuelekeza kujifunza mambo mapya ya kuboresha maisha yako?
Tuanze kwa kutumia magari mapya ya kisasa. Gari yetu Karakana ya Ubongo ni sehemu ya kushirikishana mazingaombwe yenye dopamine ya manufaa.
Tarehe 28.01.2018 tutafanya jaribio dogo la kuona namna ya kujifanyia mapinduzi. Kila mtu ana fursa ya kufanya kitu. Karibu sana.
Narudia tena leta mawazo yako! Yanaweza kuja hapa au hata inbox.
Mungu ni mwema.
Long live Karakana ya Ubongo.
Kifupi namshukuru Mungu sana kwa huduma hii ya kufundisha na kuna mengi mazuri yanakuja.
Nikuombe kitu kimoja ‘KIZURI KULA NA MWENZAKO’. Naamini hukosi watu kumi wa kuwaelezea kinachoendelea karakana ya ubongo na pia usiache kuwaelezea masharti yaliyopo.
Wakikuelewa basi waadd maana u admin pia, huhitaji kunisubiria uniambie.
PAMOJA TUNAWEZA KUWA CHACHU YA MABADILIKO.
FANYIA MAZOEZI YA KUJIKUBALI NA KAMWE USIRUHUSU KUTOJIKUBALI KWANI KWA KUFANYA HIVYO UTAKUWA UNAJIADHIBU.
Weka mikakati na ingia kazini. Ukishindwa kupangilia mambo ya kufanya kufikia malengo maana yake umepanga kushindwa kufikia malengo yako (If yo do not plan, you plan to fail).
ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2018 NDIO IMEANZA. HIYO NI NAMBA TU NA HAINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.
NAWATAKIA KHERI NA BARAKA TELE KATIKA YA MWAKA 2018.
SEE YOU TO THE TOP WHERE IS NOT CROWDED.

Maoni
Chapisha Maoni