Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Nidhamu

Nidhamu ni kutenda kile ulichoahidi utakitenda.
Hivyo nidhamu si adhabu bali ni mafunzo na ni kwa wale tuu wenye kutekeleza bila kujali hali ikoje ndio wenye kufanikisha.
Kitu kimoja kinachowatenganisha waliofanikiwa na wasio fanikiwa ni kwamba; Waliofanikiwa wanatambua umuhimu wa kuwa na nidhamu na siyo kwa siku moja tu bali kwa muendelezo iwe ni kwa kujisikia au kutojisikia ni lazima kitendo husika kifanyike.
Mwanadamu kwa asili ni mvivu. Na kielelezo kikubwa ni ile kauli isemayo SIJISIKII.
Ndugu yangu mpendwa naomba nikupe ushauri wa bure – Mafanikio ni vita. Mapambano ni lazima. Sijawahi ona mtu aliye kwenye mapambano asipate maumivu au kujeruhiwa na hata kupoteza maisha wakati mwingine lakini hajilazi chini ati hajisikii kuendelea na mapambano.
Mapambano yanaendelea mpaka ushindi upatikane na kikubwa ni kwamba mauvivu, majeraha na hata vifo kwa baadhi ya wapiganaji hutoa mafunzo ya nini kifanyike ili yaliyotokea yasijitokeze tena.
Ndio maana nasema nidhamu ni mafunzo tosha. Kama unataka mafunzo ya jinsi ya kufanikiwa basi – YALE YOTE ULIYOJIFUNZA KUYATENDA AMBAYO MWANZONI ULIKUWA HUYATENDI AU ULIYATENDA MITHILI YA UGONJWA WA KIFAFA YAANI SIKU NYINGINE UNATENDA NA SIKU ZINGINE HUTENDI.
NDIVYO ILIVYO KWA MGONJWA WA KIFAFA KWANI KUNA WAKATI ANAANGUKA NA KUNA WAKATI HAANGUKI.
SASA AMUA KWA DHATI KUYAFANYIA KAZI TENA SI KWA MSIMU BALI KWA MUENDELEZO BILA KUJALI MAZINGIRA NI MAZURI AU MABAYA. UWE UNAJISIKIA VIZURI AU LA. KANUNI NI KUTENDA KWA MUENDELEZO NA HISIA HAZINA NAFASI (DISCIPLINE AND CONSISTENVCY ONLY).
Mambano haya ni lazima yaambatane na mambo makuu 3:-
1. Kufanya kazi kwa kujiongeza. Kama umezoea kufanya kwa masaa 8 basi fanya kumi. Tena yawe masaa ya kufanya kazi na si ya kuhesabu ya kuwa ulianza saa 2 na ikifika saa 10 unaondoka ati umetimiza masaa 8.
Haitakiwi kuwa hivyo kwani kuna wakati ulipumzika kwa saa moja. Muda huo hautakiwi kuhesabika kama ni muda wa kazi.
Pia uliruhusu watu wakutembelee ofisini/eneo la kazi/uzalishaji na kusogoa kwa takribani lisaa limoja. Muda huo hauhesbiki.
Uliacha kufanya kazi na kuingia watsapp kwa nyakati tofauti na pia facebook na email. Ukijumlisha yote bila kuingiza Instagram, twitter na vingine vingi sema ukijumlisha ni masaa 2 kwa ujumla wake.
Hivyo saa 1 ya mapumziko + saa 1 ya kusongoa + masaa mawili mitandao ya kijamii = Masaa 4.
Hivyo ukianza kazi saa 2 + masaa 4 uliyopoteza + masaa 8 ya kazi = unatakiwa uwepo sehemu ya kazi kwa masaa 14 ndipo itamaanisha umefanya kazi masaa 8.
Hivyo ukiingia kazini saa 2 asubuhi unatakiwa utoke saa 4 usiku ndio utakuwa umetimiza masaa 8 ya kazi.
Naamini tumeelewana.
2. Wekeza – kifupi kuwa na vyanzo mbalimbali vya kimapato. Tumia kanuni ya utumwa. Mtumwa ni mtu ambaye apende asipende ni lazima afanye kile bwana wake anahitaji.
Sasa katika safari ya kuwekeza tunatumia kanuni ya utumwa yaani kila pesa ikiingia mkononi mwako 10% - 30% kwa kuanzia lakini lengo ije ifike siku utenge 99% na uweze kuishi kwa 1% tu. Kiwango hichi utakacho kitenga kiifazi iwe mfano bank basi wasisitize unahitaji account ya malengo mfano ya mwaka mmoja au miwili au mitatu uamuzi unabaki kuwa wa kwako. Nini kitaamua muda wa wewe kuendelea kuweka pesa?
Kikubwa lengo la kuweka pesa lisukumwe na thamani ya mradi ulioupanga kuanzisha.
Tuchukulie 10% yako ya mapato kwa wastani ni Tshs. 50,000. Hivyo kila mwezi utahakikisha 50,000 hivyo itakuhitaji utumie miaka 17 na miezi 7 kutimiza lengo. Huu ni mfano tu. Ila itategemea kiwango cha mradi unaoplani kuuanzisha na unacho tunza kila mwezi.
Nashauri kwa anayeanza atumie mgawanyo ufuatao:
AKIBA 30%
MATUMIZI 40%
DHARURA 10%
MSAADA 5%
SADAKA 5%
DHAKA 10%
JUMLA 100%
Narudia pesa ya AKIBA huruhusiwi kuitoa hata kama umefiwa.
Ukiongea na bank wanaweza kukukopesha 80% ya akiba yako lakini haimaanishi watapunguza akiba yako. La hasha. Akiba itabaki palepale nawe utahitajika uendelee kulipia mkopo na huku uendelee kuhifadhi % uliyojichagulia. Nashauri fuata pendekezo hilo hapo juu.
Kitendo hiki kwa wengine wanakiita kujilipa kwanza.
Hivyo kupitia utaratibu huu ni kwamba kila baada ya muda flani utakuwa umeanzisha mradi na baadaye utaanza kununua hisa.
Ushauri wangu kwa anayeanza ununuaji wa hisa aanze na umoja fund kupitia utt. Hawa ndugu wako vizuri kwa mtu anayeanza.
Mwaka huu nitamleta mtaalamu wa masuala ya hisa afundishe kwa undani ili kila mmoja wetu aweze kuelewa.
3. JUHUDI/KUJITUMA – Uwapo kazini usilegeze mkono. Kaza mkono na fanya kazi kwa bidi kana kwamba kesho haipo tena.
Bahati siku zote huwafuata watu wanaojituma na si vinginevyo. NO SWEET WITHOUT SWEAT.
Mambo hayo matatu ndiyo kwa ujumla wake tunayaita maisha ya kujitoa (SACRIFICE).
Na kuna msemo usemao SACRICE NOW ENJOY LATER yaani jitoe sasa ili ufurahie maisha baadaye. Wahenga husema ishi kama mtumwa sasa ili uje kuishi kama mfalme siku za mbeleni.
Kujipenda na kujiheshimu hudhihirika pale tu mtu anapoonesha ni mwenye nidhamu binafsi.
Vitu vyote huonekana vigumu mwanzoni kabla ya kuanza kuviona rahisi.
Fanyia mazoezi nidhamu binafsi kwa siku 21 mfululizo na utafanikiwa kuendelea. Hii imethibitishwa na wanasaikologia.
Kifupi namshukuru Mungu sana kwa huduma hii ya kufundisha na kuna mengi mazuri yanakuja.
Nikuombe kitu kimoja ‘KIZURI KULA NA MWENZAKO’. Naamini hukosi watu kumi wa kuwaelezea kinachoendelea karakana ya ubongo na pia usiache kuwaelezea masharti yaliyopo.
Wakikuelewa basi waadd maana u admin pia, huhitaji kunisubiria uniambie.
PAMOJA TUNAWEZA KUWA CHACHU YA MABADILIKO.
FANYIA MAZOEZI YA KUJIKUBALI NA KAMWE USIRUHUSU KUTOJIKUBALI KWANI KWA KUFANYA HIVYO UTAKUWA UNAJIADHIBU.
Weka mikakati na ingia kazini. Ukishindwa kupangilia mambo ya kufanya kufikia malengo maana yake umepanga kushindwa kufikia malengo yako (If yo do not plan, you plan to fail).
ONYO: KAMA HUTOBADILIKA HAKUNA CHA KUBADILIKA. NI KWELI 2018 NDIO IMEANZA. HIYO NI NAMBA TU NA HAINA MAANA YOYOTE. KIKUBWA NI WEWE.
NAWATAKIA KHERI NA BARAKA TELE KATIKA YA MWAKA 2018.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...