Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tabia Na Lengo

Tabia yetu sisi ni matunda ya vile vitu vidogo vidogo tunavyofanya kila siku.
Ufanisi tulio nao siyo chochote zaidi ya tabia zetu. Mafanikio hayaji kwa siku moja bali ni tabia zetu ndo zinatuvusha kutoka eneo moja A kuelekea eneo lingine B.
Katika maisha yetu ya kila siku tunaweza kupata changamoto katika kujenga tabia zetu kwa sababu ya vikwazo na visingizio mbali mbali.
Jinsi ya kuondoa vikwazo na visingizio hivyo ni lazima kuangalia nidhamu zetu, motisha tulizo nazo na pia jinsi tunavyojijengea malengo na tabia zetu.
Unapojiwekea malengo unakuwa unachukua hatua nzito na ya maana katika kupangilia maisha yako.
Kupangilia kwa kuandika malengo na utekelezaji wa malengo ni vitu ni tofauti.
Kujijengea tabia fulani ni hatua muhimu zaidi ya kukusaidia kusonga mbele.
Kwa mfano nina lengo la kusoma vitabu kumi mwaka 2018. Hilo ni lengo zuri.
Mfano wa pili ni kujifunza tabia ya kusoma kurasa kumi au zaidi kila siku. Hiyo ni tabia.
Ukilinganisha malengo na tabia ya hii mifano yetu utagundua kwamba tabia ina nguvu ya kukufikisha mbali zaidi. Kivipi?
Ukijenga tabia ya kusoma kurasa kumi au zaidi kila mwaka unaweza kuzidi lengo lako la vitabu kumi kwa mwaka. Unaona je hilo?
Ukifanyia kazi malengo yako bila kujijengea tabia mahsusi ya kutenda, unaweza kujikuta mwaka umeisha na umesoma vitabu 7 tu. Au hata chini ya hapo maana hakuna tabia uliyoiruhusu ikupe mwongozo maalum.
Lazima kuchukua hatua za kugeuza malengo yako kuwa tabia. Tunaona tofauti ya tabia na malengo kwa mapana zaidi.
- Tunataka kujifunza ujasiriamali. Tunaweza kuamua kujifunza kwa miezi sita (lengo) au tunaweza kuamua kutenga lisaa limoja kila siku kujifunza mambo ya ujasiriamali (Tabia)
- Tunahitaji kusoma vitabu zaidi. Twaweza kujiwekea lengo la kumaliza kitabu kimoja kwa mwezi (Lengo) au
tukasoma kurasa 10 kwa siku (Tabia)
- Foleni inaweza kutuzuia kuona watoto kila asubuhi maana unajikuta umeondoka kabla hawajaamka na ulirudi wameshalala. Tunaweza kuamua kutengeneza muda wa lisaa limoja kila siku kuona watoto(Lengo) au tukachagua piga ua tuwahi kula nao chakula cha jioni. Tunaweza kuacha mazoea ya kufanya kazi ili kukwepa foleni au kupitia mahali happy hour kusubiri foleni ipungue (Tabia)
Lea kuchukua hatua madhubuti tujielewe, tuelewe majukumu yetu, na pia jinsi tabia zilivyo na nguvu ya kubadilisha maisha yetu, tunaweza kujitengenezea miujiza na kufanya maisha yawe matamu sana. Ni kwa kubadilisha mifumo na ratiba zetu pekee ndo tutaweza kuogelea kwenye mafanikio tunayoyahitaji.
Tukijifunza tabia zetu. Tukabadilisha zile mbaya kuwa nzuri ndivyo tutakavyoweza kufikia malengo yetu kwa unafuu zaidi. Usishangae hata mzigo wa maumivu ya kufikia malengo yako yakatimia.
Malengo yako ni muhimu katika juhudi ya kufika unakoelekea. Ila tabia zako zikishazoeleka unakuwa kama ndege isiyohitaji rubani.
Mfano mzuri ni kunawa uso au kupiga maswaki asubuhi. Huhitaji kuambiwa tena kama mtoto mdogo maana imeshakuwa ni tabia yako.
Hapa Karakana ya Ubongo tumeshatoa ratiba ya matukio ya mwaka 2018.(Angalia Kalenda yako kwa maelezo zaidi)
Kuna matukio matatu makubwa ambayo ni:
1) Annual Newsletter ambayo unatoka December 2018
2 Kutoa vitabu viwili vizuri vyenye kuelimisha, mwezi wa Sita na Kumi na Mbili
3. Kuendesha Warsha mbili mwezi wa Sita na Kumi na Mbili
Pia kuna tukio maalumu dogo kwa kutupima lakini kubwa kwa kuipatia Gari yetu Karakana ya Ubongo mwanzo mzuri.
Ni sisi wenyewe tutaamua kama gari yetu ichukue mfumo wa ndala kutoka sehemu A kwenda sehemu B. Pia tunaweza kuigeuza iruke kwa kutembelea mabawa yake huku mwili ukiwa umetulia(static) kwa mfumo wa Helikopta. Au itembee kwa kuruka kwa kutumia mwili huku mabawa yametulia(static).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Akili Hisia (emotional intelligence).

Lea mtizamo wa kisayansi, akili hisia ni ule uwezo wa mtu kuweza kutawala anachokiona kwenye mazingira aliyomo. Hii inaamanisha kwamba aweze kutawala mazingira kwa kutumia akili ya hisia zake na wale waliomzunguka. Mtu atawezaje kuelewa kwa kutumia hisia, ishara zinazoonekana kwenye mahusiano mbalimbali bila kuambiwa sentensi au hata neno moja? Utawezaje kutawala hisia zako na za watu wengine katika mazingira uliyomo? Kuna hatua sita za kuchukua ili akili hisia zako zikupe mafanikio unayoyatafuta. #1. Hatua ya kwanza ni wewe mwenyewe kujitambua. Kujitambua ni kitu muhimu kabisa linapokuja suala la akili hisia au emotional intelligence (EQ). Hebu tujiulize ni kwanini? Bila akili hisia hatuna namna yeyote ya kujitathmini kwa vile vipaji ama tulivyo navyo, tusivyo navyo au tunavyohitaji kujifunza ili tuweze kufanikiwa katika mambo yetu mbalimbali. Utaishia kuwa kama kipofu, maana hutaona chochote katika mazingira yaliyokuzunguka. Utapata shida kubwa kutumia mikono isiyoonekana. Aki...

Timiza Malengo Yako na Joel Nanauka.

Ninamshukuru Mungu sana kuweza kuwa na waandishi mashuhuri wa kitanzania ambao wanaweza andika vitabu kwa lugha ya Kiswahili na kusaidia watanzania wengi zaidi. Kitabu cha Timiza Malengo ni kitabu cha aina yake na kamwe si cha kukosekana kwenye maktaba yako. Kama kuna kitu familia yako inabidi ikushukuru basi ni hichi kitabu. Mimi ni msomaji sana wa vitabu na niseme tu ukweli kitabu hichi ni hazina tosha na hakikisha unapata nakala yako. Wahenga walisema tusiandikie wino wakati mate yapo. Nilichokifanya ni kukupatia sehemu ya hichi kitabu kutoka ukurasa wa 29 hadi 40 neno kwa neon ujisomee na useme mwenyewe je uko tayari kukikosa hichi kitabu? Tafadhali fuatana name nikinukuu kitabu cha Joel Nanauka kwa idhini yake kama ifuatavyo:- NJIA MBILI ZA KUTAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO: Siku moja wakati Tiger Woods anahojiwa na mtangazaji akamwabia ‘’It seems like you like golf so much’’ (Inaonekana kuwa unaipenda gofu sana).Tiger Woods akamjibu, ‘’Not only I like golf but I am golf,’’ a...

CONSCIOUS NA SUB-CONCIOUS MIND

Wazo La Leo Hongera sana mwanakarakana ya ubongo kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Leo nimeona vyema nizungumzie maana ya maneno ambayo tumekuwa tukiyasikia mara kwa mara. Conscious na Subconscious. Kwanza unatakiwa uelewe "sub" maana yake nn, hii ni prefix...ikiwa na maana ya "below" something, sio negative or opposite that something. Kwa hiyo maana ya "conscious mind" ni kujitambua na subconscious mind means: internal sense of being ambayo consious mind haiwezi decipher, i mean kukupa maono halisi, wakristo wanaita nafsi, mfano mzuri wa activities za subconscious mind ni ndoto Conscious mind-ni kutumia akili wakati tendo fulani linafanyika. Hii inatokea pale mtu anapokuwa hana uzoefu wakati anafanya jambo/tendo fulani, kutokana na kutokuwa na uzoefu inabidi atumie uzingativu wakati wa kutekeleza jambo/tendo husika. kwa mfano mtu anayej...