Duniani tunajifunza kila siku. Na ukikata shauri kujifunza kila siku na kufanyia kazi yale yote unayojifunza maisha yako yatakuwa yakibadilika siku baada ya siku. Unahitaji maamuzi magumu ili kubadilika.
Kama kuna jambo mojawapo muhimu unatakiwa kulijua kwa kina basi ni ile saa yako ya kwanza unapokua umeachia kitanda namaanisha asubuhi uamkapo na pia saa yako moja kabla ya kulala.
Ukiamka unakimbilia kufanya nini? Utafiti umeonesha ya kwamba wengi tumeathirika na jambo moja kukimbilia simu na kuanza kuangalia watsapp, face book, twitter, Instagram. Tunahitaji kubadili kwani si tabia njema. Saa moja ya kwanza baada ya kuamka kitandani ni ya muhimu sana kujua unaanza na kitu gani cha kwanza ila isiwe simu. Hapa ningefurahi kama kila mmoja angeliniambia akiamka tu anakimbilia kufanya nini? Najua itanichukua muda kupata mawazo mbalimbali lakini naamini kila mmoja anajua anachokimbilia mara aamkapo.
Hakuna kanuni ya kipi uanze nacho lakini kutokana na umuhimu wa saa moja ya kwanza kuwa na umuhimu sana juu ya mstakabali wa siku yako nzima basi ni vyema kuanza na chochote kati ya hivi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuianza siku ila kamwe usianze na kushika simu. Mambo machache unayotakiwa kuhakikisha unayafanya katika saa yako ya kwanza ni pamoja na:-
Nikuombe kitu kimoja. Idhibiti simu yako. Ikibidi wakati wa kufanya jambo linalokuhitaji utulivu na kuzingatia zima kabisa mpaka utakapomaliza ndio uwashe. Acha visingizio ati nikizima nitakosa taarifa mbalimbali. Hivi hizo taarifa zimekufikisha wapi?
Nisikuchoshe najua ili kufanikisha haya nikuelezayo huna budi kuwahi kulala na kuamka mapema yaani kabla ya saa 11 asubuhi uwe nje ya kitanda. Mwanzoni anza na alamu na baada ya siku 21 hutahitaji alamu tena kwani ubongo wa ndani utakuwa umekuelewa ya nini unahitaji na utaendelea kukutimizia. Huchukua siku 21 kuiandikisha tabia mpya.
Si kazi rahisi kwa kuwa ubongo umetengezwa katika mazingira ya kutuhurumia, hivyo kubadilika ni mpaka wewe mwenyewe uwe umejua umuhimu. Utaanza kwa kujilazimisha mpaka ubongo utakubali kukubadilishia tabia. Wengi huanza kwa hamasa siku tatu za mwanzo na kisha huacha.
Hakuna mwaka mpya kwa kuwa wewe ni yule yule na utabaki kufanya maigizo tu ati mwaka huu nitafanya hichi na hichi ila ni mihemko tu. Si jambo dogo la mwaka mpya na mambo mampya. Mwaka mpya utaleta umaana iwapo tu wewe utakuwa mpya kuliko mwaka jana. LAZIMA UBADILI UNAVYOCHUKULIA NA KUFANYA MAMBO. MADILIKO NI MUHIMU MAANA NDIO YATAKAYOLETA MATOKEO MAPYA NA SI MWAKA MPYA. MWAKA UKUKUTE UMEBADILIKA SANA. HAPO LAZIMA KITAELEWEKA.

- Anza kwa kumshukuru Mungu kwa kuiona siku nyingine nzuri na jisemeshe ya kuwa unakwenda kuiishi siku kana kwamba ndio siku yako ya mwisho kuishi hapa duniani na unataka kuacha historia ya kuwa siku ya mwisho ulifanya makubwa sana na kama ungepewa siku zingine ungeushangaza ulimwengu. Jiambie ya kuwa siku ya leo utajituma sana kuhakikisha hakuna ulichopanga kitakacho bakia paipo kukifanyia kazi. Endelea kujisemesha ya kuwa wewe u bora sana na utafanya kila jambo kwa ufanisi wa hali ya juu. Fanya hivyo kila siku. Futa kwenye ubongo wako msamiati wa kuahirisha.
- Anza na kutahajudi. Kama kuna moja ya jambo nyeti katika maisha ya mwanadamu basi ni kutahajudi maana hapa unampa nafasi Mungu aongee na wewe. Kama utaweza kutumia saa nzima kutahajudi utaharakisha sana safari yako ya mafanikio. Maana mara baada ya kutahajudi utapata mawazo mbali mbali na hakikisha unayanakili yote kwenye kijinoti buku chako (Brain Damping note Book).
- Anza kwa kujisomea kitabu chenye kukupa hamasa na kukufundisha mambo yatakayokusaidia kuboresha maisha yako. Sijui u mahiri katika eneo lipi – kikubwa hakikisha unaendelea kujiongezea maarifa katika hilo eneo lako kila siku. Kikubwa katika saa yako moja baada ya kuamka usiruhusu kuangalia TV na wala usichezecheze na watoto wala paka wala mbwa. Hakikisha umejitenga wewe peke yako katika utulivu wa hali ya juu. Ukiwa unajisomea hakikisha una mahali pa kuandika mambo ujifunzayo kwenye hicho kitabu.
- Anza kwa kusilikiliza audio au video kutoka kwa watu mashuhuri katika mafanikio kama Bill Gates, Jim Rohn, Les Brown, Max Well na wengine wengi.
- Hakikisha kila siku kabla ujaianza siku lazima utokwe na jasho. Hili ni tendo muhimu sana. Tokwa jasho kabla hujaanza siku. Vitu vitakavyo kusaidia kutokwa jasho ni pamoja na kurukaruka Kamba, kukimbia angalau km 2 hakikisha hazipungui. Hichi ni kiwango mahususi. Hivyo kimbia au tembea km 1 kwenda na kurudi km 1. Endesha baiskeli. Tendo hili hata upangeje siku yako ni lalazima kulifanya. Hii itakuhakikishia kuianza yako ukiwa na nguvu za kutosha kufanya maajabu.
- Kunywa maji ya kawaida ila ni vizuri sana kama utaweza ya vuguvugu – kiwango cha maji ya kunywa kitategemea na uzito wako. Kanuni ni kuchukua uzito wako kwa kgs na kisha gawa kwa 24 jibu ni kiwango cha lita za maji ambazo ni lazima uzinywe asubuhi kabla ya kuswaki. Kwa nini unasisitizwa kufanya hivyo:-
- Kwanza unatakiwa kujua 75% ya ubongo wako ni majimaji na hivyo maji ni lazima kwa mstakabali wa ubongo wako vivyo hivyo na mwili wako umetawaliwa na maji kwa sehemu kubwa. Na kumbuka kanuni ni kunywa maji kabla ya kuswaki.
- Maji huamsha viungo vya ndani tayari kwa utendaji wa siku.
- Maji ni dawa. Magonjwa mengi yaliyokuwa yakikusumbua siku za nyuma hutayasikia tena. Anza kubadili tabia kwa kuchagua kunywa maji badala ya soda au juice za mabox. Pendelea maji. Mimi nina miaka Zaidi ya kumi sasa sinywi kabisa soda. Maji ndio chaguo bora kuliko ila radha yake si ya kukuhamasisha ila faida yake mwilini ni lukuki.
- Ukinywa mfululizo baada ya siku 30 utashangaa hata ngozi yako itakavyoanza kuwa nyororo.
- Itakusaidia kusafisha figo. Ukikojoa angalia mkojo mwako – hakikisha kila siku ni mweupe. Usiruhusu kuwa wa rangi unajiumiza.
- Jizoeshe kufikiria na kujenga taswira ya maisha unayoyataka. Kwani mawazo yanayotawala kwenye ubongo hugeuka na kuwa sumaku ya kuvivuta uwazavyo. Tafuta video ya THE SECRET uiangalie.
- Saa yako moja ya kwenda kulala hakikisha unaitumia kupitia malengo yako kama unapicha za malengo yako tafadhali pitia hizo picha zote. Kumbuka akili hufanya kazi kwa haraka kupitia picha. Hebu kuwa na album ya malengo yako.
- Tumia saa yako moja kwa kufikiri. Jiachilie na anza ziara na ubongo wako ukiwa umetulizana au anza kufikiria suluhisho la tatizo linalokusumbua na utashangazwa na ubongo wako utakavyokupa namna mbalimbali za kutatua. Orodhesha hadi zifike ishirini na anza kuzitumia, ya kwanza isipofanya kazi nenda ya pili na ya tatu naamini hata kabla ya kufika ya 10 utakuwa umepata suluhu.
Nikuombe kitu kimoja. Idhibiti simu yako. Ikibidi wakati wa kufanya jambo linalokuhitaji utulivu na kuzingatia zima kabisa mpaka utakapomaliza ndio uwashe. Acha visingizio ati nikizima nitakosa taarifa mbalimbali. Hivi hizo taarifa zimekufikisha wapi?
Nisikuchoshe najua ili kufanikisha haya nikuelezayo huna budi kuwahi kulala na kuamka mapema yaani kabla ya saa 11 asubuhi uwe nje ya kitanda. Mwanzoni anza na alamu na baada ya siku 21 hutahitaji alamu tena kwani ubongo wa ndani utakuwa umekuelewa ya nini unahitaji na utaendelea kukutimizia. Huchukua siku 21 kuiandikisha tabia mpya.
Si kazi rahisi kwa kuwa ubongo umetengezwa katika mazingira ya kutuhurumia, hivyo kubadilika ni mpaka wewe mwenyewe uwe umejua umuhimu. Utaanza kwa kujilazimisha mpaka ubongo utakubali kukubadilishia tabia. Wengi huanza kwa hamasa siku tatu za mwanzo na kisha huacha.
Hakuna mwaka mpya kwa kuwa wewe ni yule yule na utabaki kufanya maigizo tu ati mwaka huu nitafanya hichi na hichi ila ni mihemko tu. Si jambo dogo la mwaka mpya na mambo mampya. Mwaka mpya utaleta umaana iwapo tu wewe utakuwa mpya kuliko mwaka jana. LAZIMA UBADILI UNAVYOCHUKULIA NA KUFANYA MAMBO. MADILIKO NI MUHIMU MAANA NDIO YATAKAYOLETA MATOKEO MAPYA NA SI MWAKA MPYA. MWAKA UKUKUTE UMEBADILIKA SANA. HAPO LAZIMA KITAELEWEKA.
Maoni
Chapisha Maoni